Hivi Nyerere aliwahi kugombana na Kanisa Katoliki au Protestanti?

Kibao ni ngapi kitarakimu!?..u akuta shule za Tanga mjini miaka ya 60-80 wanaofaulu wengi ni wakiristo,mchezo ndiyo huo nchi nzima,kwanza serikali haikujenga shule ili kudhibiti idadi ya wasomi,na hapo waislam ndiyo waathirika wakubwa,usifikiri jakaya kuanzisha shule za kata ilikua kupenda tu kujenga shule Bali kusaidia pia waislam wapate fursa ya elimu ili kesho pasiwepo upogo uliopo
 
Mbona unatema sana povu, nimeuliza swali, jibu swali, hayo ya sasa unaweza kuyazungumzia wewe sio lazima mimi
 
Katuachia katiba mbovu,vita ya Uganda ilitugharimu pesa nyingi,

Katiba mbovu Kwa mazingira yapi?. Mazingira na hali ya kipindi kile ni tofauti na sasa, hivyo ni jukumu lenu sote kurekebisha katiba kulingana na wakati tuliopo. Vita ya uganda iligharimu pesa kiasi gani? Ripoti ya CAG ya sasa umeisoma au umesikia ubadhirifu uliotukuka!!. Ulitaka nduli achukue ardhi ya babu na bibi zako, ulikua ni uzalendo wa hali ya juu maelfu ya watu wa kipindi kile kuipigania nchi ili vizazi vyako na vyangu vipate maeneo ya kutosha kwa ajili ya wao na wajukuu wao. Kuwa na shukrani bwana mdogo kama maisha yamekushinda usimsingizie baba wa taifa ni miaka karibuni 35+ hayupo madarakani!!
 

Tarakimu gani maalim!!. Kwa maandishi yako tu kwa kuyasoma naona kabisa naeingia nae katika mjadala hana elimu cha kwanza!! Pili huna ujualo bali unaandika ujinga lakini tatu shule za kata si zipo kwani wanasoma waislam pekee?. Kama hukusoma ni wewe, wenzio walisoma na mpaka sasa wanasoma.
 
Kuna padre mzungu, nadhani ilikuwa toka Peramiho monasteri, alikamatwa na nyara za Serikali. Akakamatwa. Baraza la Maaskofu likapeleka ombi la kumwombea msamaha kwa Mwalimu Nyerere. Mwalimu Nyerere alichukia sana, akawakatalia. Akaamuru nyara zilizokamatwa zibakie nchini, na Padre alifukuzwa nchini mara moja.
 
Intellectual mjinga na mpuuzi kama yule?
Ni mwendawazimu tu ndiyo anaweza kumsema vibaya Mwalimu Nyerere.

Hakuna kiongozi yeyote ambaye amewahi kuwa, na huenda atakayekuja ambaye alikuwa na dhamira njema kama Mwalimu Nyerere, wala alitekuwa super intelligent aliyeishi kwa principles na kuheshimu taratibu kama Mwalimu Nyerere.

Mwalimu Nyerere kwa wakati aliokuwa ameongoza, angekuwa mtu mwenye tamaa, au mtu mwenye upendeleo na ubaguzi, angefanya bila kubugudhiwa na yeote.

Nafasi yake katika Taifa hili katika ubora, itaendelea kusimama, japo kama mwanadamu mapungufu na makosa ya hapa na pale hayaepukiki. Na yeye aliwahi kusema wazi kuwa wakati wa uongozi wake, kuna makosa walifanya, lakini kinachomshangaza ni Taifa kuyaacha mazuri waliyoyafanya na kuyakumbatia makosa waliyokuwa wameyafanya.

Mwalimu Nyerere angekuwa ni mtu kutafuta utukufu wake, angekufa akiwa Rais maana hakukuwa na pressure yoyote yenye nguvu ya kumtaka aondoke madarakani.
 
Ni mjinga pekee ambaye hawezi kuona mchango wa Mwalimu Nyerere katika kuwakomboa waislam kielemu.

Kulikuwa na shule ngapi ziluzokuwa zinamilikiwa na taasisi za kiislam wakati nchi inapata uhuru?

Ni shule ngapi za taasisi za kiislam zilitafishwa ili watoto wote wa jamii zote na dini zote wasome bila ya kujisikia wanyonge?

Watu ambao waliumizwa na utaifishaji wa shule ni taasisi za Kikristo maana ndio waliokuwa na shule nyingi.

Mtu anaweza kumchukia Mwalimu Nyerere kwa sababu zake lakini siyo kwa dhamira yake ya kujenga jamii yenye umoja na usawa. Na mema haya makuu hakika jina lake litaishi daima.
 
Rasilimali za kujenga hizo shule hazikutokana na michango ya kanisani, zilitokana na rasilimali za Nchi

au unadhani walichukua kodi Vatican kuja kujenga huku ?
Shule zimejengwa kwa hisani ya watu wa Roma.

Muone aibu hata kile chuo cha morogoro mmepewa bure, tafuteni vya kwenu
 
Acha ujinga,kwa nini aliivunja eamws iliyojikita kujenga taasisi za elimu na afya!?
 
Huwezi kuingia mgogoro na waajiri wako!!

Hao ndio waliomuajiri asimamie transmission ya Tanganyika baadae TANZANIA!alikua loyal kwao hasa katoliki na CCM!!

Huyo unaemtaja kua alikua na mgogoro na kanisa huoni hayupo!!?
 
EAMWS ilimilikiwa na WaIslam wahindi,waafrika walikuwa wakitumika pasipo kutazama maslahi ya nchi zao.

BAKWATA ni mali au chombo cha WaIslam wazawa kuendelea kulilia taasisi ya wahindi ni ishara ya ukosefu wa akili.

Ikiwa BAKWATA imeshindwa kutimiza wajibu wake tatizo si kuondolewa au kufutwa taasisi ilivyokuwa mali ya wahindi bali ni juu ya WaIslam wenyewe kuketi kitako na kutazama namna bora ya kutatua tatizo lenyewe na si kulilia taasisi za kibeberu.
 
Nyerere alikuwa kiongozi shupavu kosa lake kubwa ni Muungano feki.
Kosa lake kubwa ni kuingia kichwa kichwa kutumia rasilimaki za nchi kusaidia ukombozi wa nchi za kusini mwa Afrika na vita vya uganda. Pale aliferi sana.
 
Kosa lake kubwa ni kuingia kichwa kichwa kutumia rasilimaki za nchi kusaidia ukombozi wa nchi za kusini mwa Afrika na vita vya uganda. Pale aliferi sana.
Kwahiyo wewe huoni jinsi wakojani wanavyofaidi huu muungano magumashi.
 
Ilikuwa na wanachama wa aina zote, wa kiasia na kiaf, Waafrika wakiwa wengi
Ila viongozi wake wa juu kama vile Rais, makamu na katibu wake walikuwa Waafrika, actually viongozi karibu wote walikuwa Waafrika, so unaposema ilikuwa ikimilikiwa na wahindi ni kwa namna gani
 
Wavaa kobazi bhna si uyo alie taifisha shule za roman hili na nyie mpate kusoma kidogo muondokane na kuvaa kobazi
Ni mtu mjinga na mpuuzi ndo anayeweza kuandika mambo ya kijinga na kipuuzi kama haya! Wewe ni miongoni mwa watu wajinga na wapuuzi kwenye hili jukwaa. Na wala hujui chochote kwenye hii nchi!
Nachukizwa sana na hya mambo ya kujadili dini za watu.
 
Ni mtu mjinga na mpuuzi ndo anayeweza kuandika mambo ya kijinga na kipuuzi kama haya! Wewe ni miongoni mwa watu wajinga na wapuuzi kwenye hili jukwaa. Na wala hujui chochote kwenye hii nchi!
Nachukizwa sana na hya mambo ya kujadili dini za watu.
Ume andika upuuzi .Enjoy the ignore button Boom [emoji870]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…