Hivi Nyerere aliwahi kugombana na Kanisa Katoliki au Protestanti?

Iliwahi kutokea mara moja. Na Nyerere alilisema wazi. Japo haukuwa mgogoro kati ya Serikali na Kanisa, bali mtendaji mmoja wa Kanisa.

Kuna padre mzungu alikamatwa na nyara za Serikali, meno ya tembo, akisafirisha kwenda nje.

Baada ya kumatwa, Kanisa lilimwomba Rais amsamehe. Mwishowe alisamehewa, lakini alinyang'anywa mali hiyo isiyo halali, na alifukuzwa nchini.
 
Wewe acha ubishi wa kijinga Watanzania waliosoma kwenye hizo shule walisoma bure enzi hizo na hata matibabu walipata bure kutokana na michango ya Wazungu.Mwafrika alikuwa bado hajajua umuhimu wa COST SHARING.Na kama ulizaliwa baada ya 1990 huwezi jua kule tulikotoka utabaki tu kubwabwaja na stori zako za kijiweni.
 
Nyerere alitaifisha mali za Kanisa kibao, mashule, hospitali n.k

Punguani hawawezi kuliona hilo. Mashule mengi ya Kanisa yalitaifishwa na Serikali ili watu wa dini nyingine nao wasome katika shule hizo wakiwa na amani ya mioyo yao, lakini punguani wanaojificha kwenye udini hawawezi kuliona hilo.
 
Rasilimali za kujenga hizo shule hazikutokana na michango ya kanisani, zilitokana na rasilimali za Nchi

au unadhani walichukua kodi Vatican kuja kujenga huku ?

Kama hunui kitu ukae kimya. Usipende kuropoka mambo usiyoyajua.

Mashule, hospitali na makanisa, vyote wakati huo vilijengwa kwa pesa zilizochangwa na waumini wa makanisa mbalimbali ya mataifa ya Ulaya. Hailiwa kpdi ya watanzania wala sadaka za waumini maskini wa Tanzania.

Ni siku za karibuni sana, ndiyo vitu hivyo vimeanza kujengwa kwa michango ya waumini.
 
Watu wanapumbazwa, nao wanakubali. Umeeleza vizuri sana. Maisha baada ya kifo, ni ya roho pekee yake. Roho haihitaji chakula kwa kuwa chakula ni kwaajili ya mwili. Roho haihitaji nyumba wala gari. Roho haihitaji mke kwa sababu tenaldo la kukutana, tena linaitwa kukutana kimwili, ni la mwili, na siyo roho. Halafu wewe mtu na akili yako unaambiwa ukifa utapewa mabinti warembo mabikira, na wewe unaitikia!! Una akili wewe kweli? Tangu lini Roho ikawa na bikra!

"Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa", inadhihirika wazi.
 
Julius kuna makosa mengi aliyafanya kipindi cha utawala wake ndio yanayotugharimu mpaka leo
Mwongo. Yataje tuyajadili. Unapokosa hoja unabaki na hizi dhana za kuimbishwa tu kama kasuku.
 
Kwahiyo kumbe DINI ni kilainishi cha kuleta ukoloni Africa? Nasubiri jibu wallah.
Dini ilisaidia sana kuleta ustaarabu Afrika.Bila ukoloni bado tungekuwa na maisha mabaya tena tungekuwa Watumwa wa Waarabu.Tumshukuru mkoloni kwa kutuletea maendeleo.
 
Mali gani za Waislam zilizodhulumiwa na kutaifishwa?
Nilisoma mahali
hospitali kubwa na shule za madhehebu ya Kikristo vilitaifishwa. Lakini hospitali za Agha Khan, Hindul Mandal hazikuguswa. Wenye kuelewa mambo haya je hayo niliyosoma yana ukweli wowote?

Baada ya sera ya ujamaa kuwekwa kando kwa sababu zozote zile madhehebu mangapi yamejitutumua tena kujenga hospitali kubwa na hata taasisi za elimu kiwango cha vyuo.
 
Hilo ni swali la msingi sana.
 
siyo kweli, zile fedha zilikuwa zinatoka serikali kuu enzi ya ukoloni. Ilikuwa inafanya allocation ya certain percentage na kuwakabidhi kanisa kujenga mashule na huduma za jamii. Nilishawahi kukumbana na documentary fulani ilikuwa inaongelea hivyo vitu na ilikuwa ni system yao kwa makoloni yao yote ya Uingereza.
 
Mambo ya imani yana maswala mengi sana ya kushangaza, kama hayo uliyoeleza hapo.
Na wakati huo huo, inaelezwa Mungu ndiye muweza wa yote. Kwa maana hiyo pia inamfanya mtu aamini kwamba Mungu huyo huyo atayawezesha hata hayo wanayotamani wakiwa huko peponi!
Mungu huyu mwenye uwezo wote; akaona ni vizuri binaadam aliowaumba yeye, wamwabudu kwa njia mbalimbali kupitia dini zao(?)..., wengine wawe wakristo, na wengine wawe mabudha, wahindu, waislam,n.k.,. Na katika dini zote hizo, patokee tena vikundi mbalimbali; waislamia, wasuni, wasabato, baptist, walokole na.k.n.k., na inapolazimika hawa watu wagombane kwa sababu za hizi dini zao za kumcha Mungu yule yule, ambaye anaweza kila kitu, anajuwa kila kitu; kama mtoto, anapotungwa mimba, hata kabla, kwamba mtoto huyo siku moja atakuwa peponi au jehanam...

Kuwa na Imani ni vizuri, na kumtukuza Muumba wako ni jambo zuri sana; kama ilivyo kuishi maisha na binaadam wenzako kwa maelewano mazuri. Mimi naamini, Mungu huyu mwenye huruma nyingi kwa viumbe wake, kamwe hawezi akageuka na kuwa katiri, anayechukizwa kila mara na kutaka kuangamiza binaadam aliowaumba.
Nitaishi maisha mazuri duniani kwa kutenda mema kwa uwezo wangu alionijaalia Mungu mwenyewe, na mwisho wa siku, atanipokea peponi pamoja na madhaifu mengi aliyoniruhusu kuwa nayo.
Nitatumia mafuzo nilikojiunga na dini, lakini 'dogma' za huko zote hazina maana kubwa kama zisivyokuwa na maana za wale wengine katika imani zote zinazodai kufundisha aliyowapa Mungu wayafundishe wao kwa binaadam, na kujiona wao ni bora zaidi ya wengine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…