Hivi Wanasayansi wa Nyuklia wa Iran wamekosea Nini kustahili kuuawa na Israel?

Hivi Wanasayansi wa Nyuklia wa Iran wamekosea Nini kustahili kuuawa na Israel?

Hivi ushabiki wa kipuuzi kama huu huwa unawasaidia nini?

Mara huyu anaililia Iran, mara huyu anaililia Israeli....

Hili taifa Lina watu wapuuzi sana.
 
Mkuu kauli ya nchi ya Iran kuifuta Israel kwenye USO wa dunia. alafu aliyetamka kauli hiyo anataka kutengeneza mabomu ya nyukilia. Na anafadhil vikundi unavyopambana navyo. Je utamwacha tu ukikenua meno?.
Anachokifanya Russia kwa Ukraine
ndicho anachokifanya Israel kwa Iran
Sasa ngoja tuone kama wataua na elimu zao au fikra zao!! 😄😄😂
 
Sasa Mkuu unamlalamikia nani humu JF?😀😃
Wanasema ukitaka kuua nyoka unapiga kichwani siyo kwingineko!
Ndiyo hivyo Israel kuua Scientists ni kuua programe nzima ya shughuli za kinuklea!
Lakini lengo siyo Nuklea programe za Iran,hilo linatumika kama kigezo lengo ni kuangamiza utawala wa Iran ambao ni tishio kwa Israel.
 
Nawa

Na waziri wa ulinzi wa israel kaesema watampondo njoka kichwani na kumchuna ngozi yake
 
Hapana ndugu Israel imeundwa kwa target ya kushambulia Uislam na hata Netanyahu alipo hutubia bunge la America alikuwa ana quote bible zenu.

Swali kwanini UK, France, USA, Serbia, Italy., Germany na hata Jordan wakimbilie kumlinda? Tupe reason kama si udini. Jordan yule mfalme ana damu ya kizungu kama si Kiyahudi.
Mkuu nikwambie kitu kuhusu Hawa viongozi Kuna wakati wanapotafuta engo ya uhalali Wana quote maneno ya Mungu kupata uhalali au kupata sapoti ya Imani husika aliyoi quote. wanaongoza kwa Aina furani ya ujanja na Hila na ndipo mwisho wa Nia zao wanaishia kuchafua Imani za watu wakati mlengo wao ni tamaa ya utawala tu.
Na wanajua ni rahisi sana kumtawala mtu mwenye Kumuamini MUNGU sababu wanajua Wacha MUNGU ni watu wanaopenda Kufanya MAPENZI YA MUNGU
 
Magaidi hawaruhusiwi kumiliki nuclear duniani na haitawezekana Kwa Iran kumiliki nuclear, magaidi ni marufuku kumiliki nuclear
 
Ndoto za kushiba ugali upo chini ya mti wa mawese tabu sana Israel hawezi kwenda hi vita na Iran zaidi ya mwezi au miezi 3 akijitahidi sana, atainua mikono hata asaidiwe vipi na US na Europe
20250616_142231.jpg

Endeleeni kutulisha matango pori!
 
Kusema la ukweli kabisaa haka kamsemo kasipuuziewe....... kichaa hakibidhiwi rungu kudadeki
 
Iran hata asipokua na nuclia akitaka kuifuta Israel kwenye ramani anaitandika tu si umeona kinachotokea. Hili suala la Nuklia ni sababu tu inatafutwa ili kuiangusha utawala wa Iran.
Wewe ndiyo unaamini hivyo lakini ukiangalia Iran bado sana kuifuta Israel.
Kwenye vita watu huwa hawapigi ovyo ovyo ili mradi tu. Zinapigwa sehemu muhimu tu hasa wale viongozi na sehemu muhimu kama hospital, jeshi na maghala ya silaha na ukiiangalia Israel ana uwezo wa kuifuta Iran
Yale makombora 100 yamepiga ovyo ovyo tu.
Angalia kama nchi unapoteza watu muhimu wenye akili unategemea utakuwa na taifa lenye uwezo? Si kila mtu mwenye akili
 
Ndoto za kushiba ugali upo chini ya mti wa mawese tabu sana Israel hawezi kwenda hi vita na Iran zaidi ya mwezi au miezi 3 akijitahidi sana, atainua mikono hata asaidiwe vipi na US na Europe
Sawa kobazi mkuu. Iran inabid amshukuru sana Putin
Upo wizara gani Iran?
 
Hakuna zaidi ya ubabe wa marekani na Israel. Makubaliano ya two state solution yalishafikiwa. Kwanini sasa Israel hataki Palestine iwe na taifa lake huru?
Wapalestina wenyewe walishakataa mapendekezo mengi tu yaliyofikiwa hapo kabla ikiwemo na hiyo 2 state solution.

Imagine Israel ina historia ya kupigana na nchi 3 kwa wakati mmoja, ina historia ya holocaust, halafu wewe unatumia vikundi vya kijeshi kutaka kuiangamiza na wakuu wako wakiwa madarakani wanatamba kuifuta Israel kwenye ramani ya dunia.

Halafu unafanya juhudi kuwa na silaha za nyuklia. Unataka hao waisraeli wakae tu wakisubiri waone itakuwaje?

Tangu wakati wa Ahmadinejad Iran amekuwa akitaka kuifuta Israel na raia wake wana chant Death to Israel, Death to Israel. Hapo Israel ana haki ya kukufanya chochote.
 
Hii tabia ya Israel ya kujisikia kutaka kumuua yeyote inaemtaka haipaswi kuendekezwa na Dunia iliyostaarabika.

Iran ina Haki ya kuendeleza tafiti za sayansi ya nishati ya nuclear, hata silaha za Nuklia. Hii siyo Haki ya Iran tu bali hata Tanzania inayo.

Inapotokea nchi Moja inaipangia nchi nyingine hii siyo sawa jambo hili lidhibitiwe.
Iran anayo Haki ya kutumia Nuklia hata kutengeneza silaha za nuclear, ndio mbona wao wanazo.
Sio kila haki inatekelezwa. Hata South Africa ilikuwa ina nyuklia ikabidi izikabidhi kwa Marekani na kutojihusisha tena na hayo mambo. Botha na Mandela walipewa tuzo za Nobel kimchongo kwa kukubali kwao kuachana na mambo ya nyuklia.
 
Hii tabia ya Israel ya kujisikia kutaka kumuua yeyote inaemtaka haipaswi kuendekezwa na Dunia iliyostaarabika.

Iran ina Haki ya kuendeleza tafiti za sayansi ya nishati ya nuclear, hata silaha za Nuklia. Hii siyo Haki ya Iran tu bali hata Tanzania inayo.

Inapotokea nchi Moja inaipangia nchi nyingine hii siyo sawa jambo hili lidhibitiwe.
Iran anayo Haki ya kutumia Nuklia hata kutengeneza silaha za nuclear, ndio mbona wao wanazo.
Unajifanya haujui? Na mnaanza kulia lia sasa hivi. Si mlisema Israel hawezi kitu kwa Iran!? Na hapo wameingia vitani wakiwa tayari wamepigana vita na Ma-proxies wenu wa Hezbollah, Hamas na Islamic Jihad kwa mwaka na nusu, tena huku wakishikwa mkono mmoja kwa maana ya masimango, vikwazo toka kwa UN, Qatar ikichochea propaganda kupitia Al Jazeera, Democrats ya US, France, UK, Spain, Canada, Australia, Russia na China. Na bado anawapa kichapo
Hao scientists ni sehemu ya Military Technical staff; ambao inazuiwa kuwa target ni viongozi wa siasa. Hata hivyo shetani Khamenei amejiweka mwenyewe kwenye list ya kuwa targeted kwa kuwa ametoa amri ya iran kushambulia maeneo ya raia.
Tuliwaambia nyinyi islamists kuwa hakuna utawala huko nyuma uliokamia kuliangamiza taifa la Israel ambao ulifanikiwa. LAKINI SHINGO ZENU NGUMU KAMA FARAO
 
Iran Ina wataalamu lukuki kama haujui.
Ndio maana ukimuua huyu utashangaa yule kachaguliwa muda sana.
Wenzako wameshaandaa mfumo wa kurithishana majukumu muda sana.
Kwani hao wanasayansi wameanza kuuliwa mwaka huu?
Kila mwaka wanauliwa ila Iran Bado inasonga mbele kiutaalamu wa nuclear .
Ni kweli kwamba Iran ina idadi kubwa ya wataalamu wa nyuklia waliobobea, lakini operesheni zinazofanywa na Israel dhidi ya wanasayansi waandamizi wa Iran zimekuwa na athari kubwa, zimesababisha kucheleweshwa kwa kiasi kikubwa, na huenda zikaweza kuzima kabisa juhudi za Iran za kutengeneza silaha za nyuklia. Kama operesheni hizo zisingekuwepo, huenda Iran ingekuwa tayari imefanikiwa kufikia hatua ya kuwa taifa lenye silaha za nyuklia. Hapa tunazungumzia mkakati wa makusudi wa kuzuia au kulemaza jitihada hizo kabla hazijazaa matunda.
 
Mkuu kauli ya nchi ya Iran kuifuta Israel kwenye USO wa dunia. alafu aliyetamka kauli hiyo anataka kutengeneza mabomu ya nyukilia. Na anafadhil vikundi unavyopambana navyo. Je utamwacha tu ukikenua meno?.
Anachokifanya Russia kwa Ukraine
ndicho anachokifanya Israel kwa Iran
Shida kobaz watakuzingha
 
Back
Top Bottom