Hivi wenzetu mnaoweka status WhatsApp mnafaidika nini? Mna utoto mwingi sana

Yani ufungue wasap yako mwenyewe, bila kushurutishwa ufungue status za watu, zikukere, uje utufungulie thread..kweli?? Nimelia sana.
 
Gentleman,
kwani wanaume nao wanajibetua viuno na matako juu kama wanawake kwenye hizo status? Inaruhusiwa kweli?

halafu ile style ya kujibetua kiuno si ndio ile ile wanaitumia wakipanda bodaboda?

hivi na wanaume kamili nao wanaruhusiwa kupinda migongo wanapotumia usafiri wa bodaboda kweli?🐒
 
Ungewafata huko huko wasapu, Kuandika masimango hapa imekaa "Kike kike" sana💣

Naomba kuwasilisha
 
Mwenye akili ni yule aliyebuni huo mtandao. Wewe endelea kupambana na hali yako. Isitoshe hakuna anayeweza kuona status yako ya WhatsApp kama sio rafiki yako.
 
Heh, kama hupendi hakuna sababu ya kuchukia watu wanavyopost, au kumwona mjinga mwanaume anayepost status,
Una lack of education kama sio exposure kimojawapo...
 
Mtu ni anatumia simu yake
Bando ni la kwake
Muda ni wake
Na anachopost ni chake na kinamhusu yeye mwenyewe

Mleta mada nataka nikuulize hivi,kwani unataka kupangia watu maisha na jinsi wavyotumia vitu vyao?

Huwa wanakuforce kuview status Zao?

Na je,baada ya kuview huwa unapungukiwa nini?
 
Kuna huyu rafiki yangu huwaga anapost wasanii au wachezaji wa yanga siku zao za kuzaliwa huwa namuuliza una namba zao anasema hana, nabakigi kimya maana huwezi kumshauri mtu na bando lake na simu yake.
Shida yenu huwa mnataka watu waishi jinsi mnavyoishi nyinyi.
Kila mtu ni ana interests na preferences zake

As long as hicho kitu anachofanya hakikuadhiri usihangaike nacho
 
Umetisha, mm nimefuta all social media imebakia hii JF, na whatsap na youtube..

Ila bado mara moja moja naweka status, na mara nyingi nikilewa hahaha ila nikiwa mzima naonaga aaah ujinga tu.
 
Kunywa piliton kiongozi, kisha jipige kifua jiambie hata wewe hauko matured ndio maana unaumizwa na mambo ya watu wasiokuhusu.

WhatsApp status ni njia ya mwasuliano kama ilivyo hii JF na platform zingine. Unapoona WhatsApp status ya mtu, hata kama wewe haitakugusa ila amini kuwa aliyepost kuna watu ana communicate nao na sio wewe. Ukiona mtu anapost mambo ya mpira basi ana cycle yake anaifikishia ujumbe, hivyohivyo wanaopost siasa, vichekesho, biashara nk.

Ukubwa sio tu namba kwa maana ya miaka, hapana, ukubwa ni pamoja na kujua kuwa kila mtu ana namna yake ya kupata furaha yake. Usichokipenda wewe kuna mwenzio ndio kinachompa furaha. Mtu akijipost yy na familia yake jua hio ndio furaha yake sasa kwanini akatushe furaha yke kwa sabau yako, mtu ambae hukumnunulia sim wala bando?

Jaribu kukua, acha makasiriko, acha kuumia kwa mambo yasiyokuhusu, na utaishi kwa furaha
 
Ukweli lazima uwe ukweli. Naunga Mkono hoja
 

Kwa maoni yangu lakini: Ni tabia za kike mwanaume kuweka vitu status au kuangalia status za watu, umbea umbea hivi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…