Hivi wenzetu mnaoweka status WhatsApp mnafaidika nini? Mna utoto mwingi sana

Hivi wenzetu mnaoweka status WhatsApp mnafaidika nini? Mna utoto mwingi sana

Mimi sio Mpenzi wa Kuweka WhatsApp status wala Profile sijaweka ila Naheshimu wanaweka Status kwani ni Njia mojawapo ya Convey information pia kwa sasa mimi sipendi Kupiga Piga simu kuuliza kama mtu bado anaishi sasa kupitia WhatsApp status unajua tu mtu fulani ni mzima bado
 
Inategemea na biashara unayofanya, Pia na aina ya watu ulonao, kama circle yako ni ya watu wa hovyo huwezi ona umuhimu wake.

Siyo kila kitu ambacho wewe hukipendi ni ujinga, kuna vitu vikikupita accept kwamba siyo mikato yako.

Aina hii ya watu una Mute status zao haziwezi appear kwenye updates. Binafsi niligombana na wife kisa sikupost picha za harusi wala engagement 😆😆😆
Mimi sipendelei status maana sina cha kuweka lakini nina jamaa yangu anabiashara ya kuuza vifaa vya electronic kwakweli anaitendea haki status na anapata wateja wengi sana kupitia bidhaa zinazo onekana status labda kwa upande wa biashara nimeona zinawafaa sana
 
Mimi sio Mpenzi wa Kuweka WhatsApp status wala Profile sijaweka ila Naheshimu wanaweka Status kwani ni Njia mojawapo ya Convey information pia kwa sasa mimi sipendi Kupiga Piga simu kuuliza kama mtu bado anaishi sasa kupitia WhatsApp status unajua tu mtu fulani ni mzima bado
Ila kuna ujinga mwingi sana
 
Naomba kuuliza labda sielewi maana mimi ni wa simu zile za kukoroga
Unamanisha Whatsapp au Facebook
Kama ni facebook nakuunga mkono.Mtu anakula pilau anarusha kila mtu aone.Akila matembele haweki.
Mtu anapanda ndege anaweka kila mtu aone lakini akiwa kwenye gari la mkaa haweki
Mtu akiwa kwenye gari kali hata kama sio lake anaweka unakuta hata mkao wake sio anaendesha
Mtoto ana birthday ya miaka miwili anaweka hajui anavunja faragha ya mtoto
Zamani wakati facebook inaanza nilikuwa na tabia hiyo nime sha mature enough nimegundua ni ujinga wa mwisho.
Jamaa mmoja aliondoka na familia yake kwenda beach wakaja wezi kiulauni wakavunja nyumba yake wakaiba wale wezi wakakamatwa na majirani wakapigwa kibano wakaulizwa mlijuaje mwenye nyumba hayupo na familia yake wakajibu alirusha kwenye facebook yake vile tunajua idadi ya familia yake na hana mbwa tukaamua kwenda kwa kujiamini.
Ninavyojua Whatapp inaitwa end to end ecrypted yaani ni wewe na unayewasiliana naye tu labda mjumvi anieleweshe.Huwezi ona whatapp ya mtu hadi uwe na namba yake na uki refresh ukimtumia ni wewe na yeye tu.
Naomba kurekebishwa
Ndio maana wanasiana siku hizi wako twiter au x hii imakaa vizuri zaidi na ule mtandao wa Linkein
facebook wanaita imekuwa yeboyebo siku hizi
 
Kuna ambae eti niliona ameweka status ya kumpongeza Trump kwa kuchaguliwa tena kuwa Rais wa marekani, nikajiuliza Trump anajua hata kama kuna nchi inaitwa Tanzania kweli?
Kuna mambo ya ajabu sana
 
Mimi sio Mpenzi wa Kuweka WhatsApp status wala Profile sijaweka ila Naheshimu wanaweka Status kwani ni Njia mojawapo ya Convey information pia kwa sasa mimi sipendi Kupiga Piga simu kuuliza kama mtu bado anaishi sasa kupitia WhatsApp status unajua tu mtu fulani ni mzima bado
Hiyo ya profile picha kuna jamaa alikuwa hapendi kuweka picha kabisa, siku amefariki ilipatikana picha moja tu walimpiga masela akiwa ameshika sungura anafurahi anakunywa.
 
mmiliki wa mtandao wa whasapp anaweza kukushtak unachafua brand yake.unda app yako achana na app za watu.itakusaidia kutozdisha ugonjwa wa kisukari.au uwezo wa kubuni ni 0% upo na mdomo pekee.
 
tena sasa unalikuta Baba zima kabisa nalo linaweka status. Inasikitisha sana
 
Japokuwa nakuunga mkono kwa kiasi fulani, pia mm Hua siweki status Ila nawaheshimu wote wanaoweka status mana hainipunguzii chochote kwenye maisha yangu.

Mtoa mada punguza u-primitive
 
Japokuwa nakuunga mkono kwa kiasi fulani, pia mm Hua siweki status Ila nawaheshimu wote wanaoweka status mana hainipunguzii chochote kwenye maisha yangu.

Mtoa mada punguza u-primitive
Kwa nini huwa hauweki status?​
 
Kwani hiyo "Status" ndiyo nini?
Haina kiswahili chake?
Usijekuta nasi wakongwe tumeweka au kuwekewa bila kujua atiiii...!!!?
 
Back
Top Bottom