Hizi ndege za ATCL zimemkosea nini Lissu? Mbona anaziwazia mabaya tu?

Mrudishieni mguu wake ndo atawaacha. Mlimpiga mguu naye anataka usafiri wetu aondoke nao
 
..hakuna mwanasiasa na mwanaharakati ametumia taaluma yake kuwapigania Watanzania kama Tundu Lissu " Simba wa Tanganyika. "
Ofcourse alitumia elimu yake kuita ripoti inayotetea maslahi ya nchi "taka taka"
 
Hivi wewe una elimu gani?
 
Nanyie amewakosea nini mbona mlitaka kumuua?
 
Punguza unafiki na uchawa.
Wananchi maskini hatukuhusika kumshambulia Lissu Kwa risasi,

Yeye adai mashauri ya kijinai Si faida za kiuchumi Toka kwenye Kodi zetu.

Mwisho wa siku hata pesa za matibabu alichangiwa na wananchi maskini.
 
Nanyie amewakosea nini mbona mlitaka kumuua?
Kina nani hao maana mpaka sasa tunasikia tuhuma tu.

Hata huyo mzungu ambaye kamfanya kama reference nae kasikia tu.
 
Sheria inaruhusu, attachment of property
Sasa Lissu mmoja tu asa abishe umma wa Watanzania kulipishwa kufidia HASARA aliyopata?

Mimi sishabikii ubaya aliofanyiwa Lissu, namaanisha kuwa, akifanyacho Lissu kutushtaki Watanzania ni sawa na kuchoma nyumba Ili kuua nyoka aliyeingia ndani ya nyumba.

Twende taratibu.
 
Ukitaka adui aliyekuumiza piga panapouma sana hasa anaowapenda au anachokipenda zaidi.
Sisi Watanzania maskini wavuja JASHO hatukuhusika kumshambulia Lissu,

Wahusika watafutwe kijinai na wafungwe,

Habari ya kutumia Kodi zetu kumlipa fidia ya mabilioni Mimi siliafiki.
 
..ripoti zile ni takataka kweli.

..si umeona jinsi makampuni ya mabeberu yanavyotupiga kwa mafaini kutokana na maamuzi yaliyofanyika kwa kuongozwa na upumbavu wa ripoti zile?
Umeandika mada zaidi ya moja kwa wakati mmoja.

Zitenganishe kwanza halafu urejee tujadiliane kwa mapana yake.
 
Soon mtatajana wenyewe, dhulma haidumu, haki itacheleweshwa tu ila lazima itashinda.
Sasa mkuu wewe unaona ni sawa kabisa nchi isiwe na shirika lake la ndege??
 
Sisi Watanzania maskini wavuja JASHO hatukuhusika kumshambulia Lissu,

Wahusika watafutwe kijinai na wafungwe,

Habari ya kutumia Kodi zetu kumlipa fidia ya mabilioni Mimi siliafiki.
Kuna aliyeonesha nia ya kuwatafuta wahusika?Acha afanye litakalomsuuza moyo wake.Naamini kila akiziona hizo ndege anaona sura ya mbaya wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…