Hizi ndege za ATCL zimemkosea nini Lissu? Mbona anaziwazia mabaya tu?

Ni sehemu ya Mali zinazojongea ndani ya JMT ,hivyo rahisi kukamatika na kuuzika

Tundulisu kashawafunga bao la kisigino mana bao la mkono halipo kisheria lakisigino ruksa
 
Ndio maana wananchi hawamuungi mkono kwenye upuuzi wake mwenyewe anaita maandamano!
 
Ndio ni u inafsi huo,

Walioumizwa CHADEMA ni wengi,

Watanzania walioumizwa ni wengi,

Angefungua shauri akijumuisha wote waliotekwa na kuumizwa, hapo angeo ekana anapigania maslah ya Watanzania, Si binafsi .
Bila shaka unajua Lissu hawajibiki kumpigania mtu yeyote. Akiamua kujipigania mwenyewe sawa tu. Huwezi kumhukumu.

Ni bora uibane serikali iwatendee haki raia wake; isiwaumize badala ya kuhangaika na Lissu.
 
Ndio shida ya wafuasi wa CDM

Kesi ipo kwenye ‘employment tribunal’ hiyo ni ‘alternative dispute resolution’ (ADR) sio mahakama. Na ADR process uwa zipo kwenye mkataba wa biashara au ajira. Ndio maana hata IGA mmeshindwa kuelewa ni nini zaidi ya kusikiliza hadithi za Mwabukusi.

Kesi inayoenda mahakamani inaitwa Litigation.

Sasa nini tofauti ya ADR na litigation google, kabla ya kutaja mambo ya mahakama kwenye issue ambayo mahakama aihusiki.

Yaani Lissu ana audience ya kuamini kila upuuzi anao ongea.
 
Bila shaka unajua Lissu hawajibiki kumpigania mtu yeyote. Akiamua kujipigania mwenyewe sawa tu. Huwezi kumhukumu.

Ni bora uibane serikali iwatendee haki raia wake; isiwaumize badala ya kuhangaika na Lissu.
Namuongelea Lissu kama kiongozi wa CDM, sio Lissu kama baba wa familia yake.
 
Namuongelea Lissu kama kiongozi wa CDM, sio Lissu kama baba wa familia yake

Namuongelea Lissu kama kiongozi wa CDM, sio Lissu kama baba wa familia yake.
Alipopigwa risasi kati yako na familia yake nani alipata hasara ? Ukivunjwa miguu, atakayetaabika kuuguza na kugharamia ni familia yako au washangiliaji wa mitandaoni. ?
 
Hazijamkosea tu Lisu bali waliozinunua wamewakosea sana wananchi wote masikini sababu hasara inayotokana na hizi ndege kama ripoti za CAG zinavyosema kila mwaka ni laana kwa taifa. Ndege zimegeuzwa kichaka cha watawala kupiga pesa bila kujali matatizo ya wananchi hasa huko vijijini ikiwemo ubovu wa barabara, huduma mbovu za afya, elimu na maji.
 
Alipopigwa risasi kati yako na familia yake nani alipata hasara ? Ukivunjwa miguu, atakayetaabika kuuguza na kugharamia ni familia yako au washangiliaji wa mitandaoni. ?
Alipopigwa risasi tulipata HASARA Watanzania wote. Nchi nzima tulihuzunika, tukamwombea na wengi walishiriki kujitolea matibabu sababu ni kiongozi wa wananchi.

Hapa anayeongelewa ni TUNDU Lissu kama kiongozi, sio Lissu kama mume wa mke wake na baba wa watoto wake.

Usichanganye mambo hayo.
 
Mashaka yako kwa wauaji na watekaji.
 
Katoa reference ya nchi isivyo na tabia ya kulipa madeni, unawaziaje vibaya chuma kisichoongea? Kaongelea wanaokimiliki
 
Tena ikiwezekana Lisu afanye mchakato akamate na bandari au Ngorongoro ili mkose cha kuuza.
 

Hujawahi kumtetea hata paka anayepigwa na watoto. Wakati Lissu amewekwa ndani na serikali mara kadhaa kwa kuwatetea wachimbaji madini kabla hajawa mbunge, na kesi alizifunguliwa ni zaidi ya 11 akiwa na baada ya ubunge. Awe mtetezi vipi zaidi ya uhai wake. Toshekeni na damu za watu. Akiwatetea anawekwa ndani, akijitetea au kudai haki yake unageuza kibao, zinakutosha ?
 
Ukiwa na dharura utajua faida ya hizo ndege.
 
Ndege zetu sisi au na yeye ndege zake ? Sometimes nashindwa kuelewa karne hii kipaumbele ni kipi..., Nadhani tatizo MIMI imekuwa ndio kipaumbele zaidi ya SISI
 
vitu vya dhuluma wacha zikamatwe tu huko zinaendeshwa kihasara tupu kwa kodi zetu
 
Weka mihemko pembeni tujadili HOJA,

Katika suala la mkataba wa Dp world, wote tulipinga mkataba wa ndani kuamliwa na mahakama za nje, na Lissu alipinga jambo Hilo,

Sasa iweje katika madai yake kutaka tena kufungua case mahakama za nje ya Nchi Ili ndege zetu zikamatwe?

HOJA Iko hapo, Uzalendo wa Nchi u wapi?
 
Kama kuna haki zake azikamate tu
Ndege ni mali ya walipa kodi hapo anakuwa anawakomesha walipa kodi kwa kuzikamata

Maana yake hata akiwa Raisi walipa kodi itabidi wakamuliwe ili alipwe yeye kuwakomesha walipa kodi ambao hawahusiki kabisa na hilo tukio

Sidhani kama kisiasa yuko makini.Kuwa atakamata ndege za walipa kodi
 
Mlipeni gharama za matibabu na fidia.

Ungekuwa wewe ungekaa kimya? Bora angekufa asingeshuhudia maumivu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…