Hizi ndio nchi ambazo Marekani na Israel hawawezi kuthubutu kuingiza pua zao kushambulia kijeshi

Umetishaa
 
Hoja yako ipo sahihi ila sio sahihi sana
 
Unaongea kwa ushabiki sana, mimi sipo kwenye ligi ya kushabikia ubabe wa upande wowote
Nachukia uonevu unaofanywa na nchi nyingine kwa taifa lolote.... Na ukweli ni kuwa Israel na Marekani zimefanya uonevu mwingi sana ambao siushabikii, ila kama wewe unaamini wao ndio wahanga wanaoonewa basi ni sawa
 
Hivi nyie mazombi mnaisigi taarifa mnapata nyie tu. Iran katwangwa bada nae kumkorofisha pakista. Kajibiwa kawa mpole
 
Hata marekani si wameshambuliwa kambi zao huko iraq juzi hapa wamepigwa kambi zao huko Jordan
Ni iran pekee anaeweza kufanya haya kuliko mwengine yeyote
 
Hivi nyie mazombi mnaisigi taarifa mnapata nyie tu. Iran katwangwa bada nae kumkorofisha pakista. Kajibiwa kawa mpole
Kama alivyokua mpole Americant baada ya magaidi wake kufyekwa kule Jordan wakiwa wanafanya ugaidi
 
Hivi nyie mazombi mnaisigi taarifa mnapata nyie tu. Iran katwangwa bada nae kumkorofisha pakista. Kajibiwa kawa mpole
Kaka kuwa mtu mzima kidogo.
Mwenzako kaleta habari pale uliisoma??
Acha ubishani wa kitoto.
Pakistan alidai kushambulia maficho ya washika silaha Boluchistan.
Mie huwa sipendi kubishana hupenda majadiliano.
 
Iran juzi amepigwa na Pakistani tena ndani ya ardhi yake, akakimbilia kuomba msamaha.
Mkuu Pakistan yenyewe imetoa kauli kuwa imepiga armed group site in Boluchistan.
Na Boluchistan inachangiwa na Iran na Pakistan.
Hivyo sio mpaka wa Iran pekee.
Pakistan hakutoa madai kuwa kalipiza kisasi kama mnavyodai .
Na aliyeitisha kikao cha usuluhishi ni Pakistan sio Iran.
 
Kushambulia ukiwa mbali hiyo hata Israel inafanyika kwa kushambuliwa na hezbullah, au Marekani kushambuliwa na vikundi vya itikadi kali.

Nazungumzia kuingia kabisa katika ardhi kijeshi kama ilivyofanyika Ukraine, Iraq, Libya nk.
Mkuu si Iran inataka kuifuta Israel kwenye Ramani ya dunia. Nini kimemshinda?
 
Hakuna ushabiki hata chembe. Labda wewe ndo unaandika bila kuangalia uhalisia unaosababisha Israel ionekane ina kiburi cha kuchokoza wenzake.

Uchokozi wa Israel unatokana na kiburi cha misaada ya kijeshi inayopewa kutoka Marekani na baadhi ya nchi za magharibi.

Kama wangeiacha ijitegemee yenyewe kama Iran, North Korea au Venezuela basi leo hii Israel ingekuwa taifa la kinyonge na la kawaida tu kama Misri, Ugiriki na nchi nyingine ambazo hazitegemei badget ya kijeshi kila mwaka kutoka Marekani.

Ni kama Makonda miaka zaidi ya mitatu alikuwa mpole na mkimya kama mimi na wewe kwa sababu ya kukosa backup ya wakubwa nyuma yake. Lakini leo hii amepewa shavu na mkuu wa nchi, sasa hivi kageuka mbogo mpaka kwa wakuu wa mikoa, mawaziri fulani, na wabunge wa chama chake wanamgwaya.

So ukiwa na bacup hata ukiwa hauna nguvu watu watakuogopa tu kwa sababu ya kulindwa na mwenye nguvu. Hivyo ndo ilivyo kwa Israel ya leo, bila backup ya Mmarekani, UK na EU ni nyepesi sana kivita, kiuchumi na mambo mengine mengi tu. Tuache ushabiki maandazi hauna maana.
 
Asante Mkuu, ndio ukweli
Watu wanafikiri vita ni piga ua yameisha ila kuna athari kubwa sana
Hili hata mimi silipingi mkuu, japo kuna wale wenzangu na mimi walipoona kambi za Marekani zinashambuliwa kule Iraq na Syria wakaanza kufikiri kwamba jibu la Marekani itakuwa ni kuivamia Iran kijeshi kitu ambacho ni dhahiri kuwa wanaota mchana kweupe huku wanatembea.
 
Hata marekani si wameshambuliwa kambi zao huko iraq juzi hapa wamepigwa kambi zao huko Jordan
Ni iran pekee anaeweza kufanya haya kuliko mwengine yeyote
Ni Iran pekee pale Mashariki ya kati ndo vijana wake wana uwezo wa kushambulia kambi za jeshi za Marekani na wakati huo huo wakashambulia ardhi ya Israel. Nchi moja tu ambayo haina backup yoyote ya badget ya kijeshi kutoka popote ila inadhibiti ujinga wote unaoendelea pale Mashariki ya kati.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…