Hizi ndizo tabia za mabinti kutoka familia njaa/maskini

Hizi ndizo tabia za mabinti kutoka familia njaa/maskini

Mwanamke anaeandika hivi tu, Hana sifa za akuwa mke.
Sema hivi mwanamke anayeandika hivi hana sifa za kuwa mke wako maana wapo wanaume wenzio wengi tu wameoa wanawake wenye mitazamo kama hii na ndoa zimedumu halafu hata asipokuwa na sifa za kuwa mke wao kwani wewe ni nani na unaongea kama nani?
 
@Edelyn,
Absolutely true, lazima ndoa ziwasumbue. Baba sio kujitambulisha tu kila wakati kama nyau. Akitimiza majukumu yake sawasawa kwahiari yao watakuita baba na mke anakuwa malkia kuita King of the state haoni shida. Tuwaombee tu kizazi chetu.
 
Kwa kweli
 
Hapana usiseme unawakimbia hao watu sema unayakimbia majukumu yako

Mkuu, mdada kama hawezi hata kujinunulia vocha huyo ni mzigo tena mzigo mzito. Ingekuwa enzi za mababu tungeuliza anajua kulimaa?

Binafsi mwanamke asiye na kipato huwa sijishughulishi naye namwacha apite tu sababu enzi za mababu tungemuita mvivu.

Huwa sipendi tabu kabisa nikiwa kwenye mahusiano.
 
@Edelyn,
Mkuu kama haya ndiyo yapo kwenye ubongo wako hakika huwezi kuyafurahia mahusiano.
 
Mkuu, mdada kama hawezi hata kujinunulia vocha huyo ni mzigo tena mzigo mzito. Ingekuwa enzi za mababu tungeuliza anajua kulimaa?

Binafsi mwanamke asiye na kipato huwa sijishughulishi naye namwacha apite tu sababu enzi za mababu tungemuita mvivu.

Huwa sipendi tabu kabisa nikiwa kwenye mahusiano.
Mwanaume uliambiwa utakula kwa jasho lako ila mwanamke hakuambiwa hivyo kumhudumia mwanamke ni jukumu lako na ndo maana akaambiwa akutii na akuheshimu

Usidhani aliambiwa akutii na akuheshimu hivi hivi tu wakati haujamuumba wala haujamzaa aliambiwa akutii na akuheshimu kutokana na wewe kumhudumia kifedha kama ambavyo unahudumia watoto wako

Majukumu ya mwanamke yanajulikana ni kufanya kazi za nyumbani na kukulea wewe pamoja na watoto wenu na majukumu yako yanajulikana ni kutafuta pesa na kumhudumia mke wako na watoto wenu

Ndo maana mwanamke anaambiwa katika swala la malezi mtoto wake wa kwanza ni mume wake vivyo hivyo hata katika swala la huduma mtoto wako wa kwanza ni mke wako sasa ukitaka mkeo akusaidie kutafuta pesa ina maana na wewe utakuwa unamsaidia kufanya kazi za nyumbani si ndiyo?
 
Kila mtu ana mtazamo wake toa wewe hoja yako unataka mahusiano yaweje je mwanamke ndo afanye majukumu mengi kuliko mwanaume?
Mke mwema
10Mke mwema kweli, apatikana wapi?
Huyo ana thamani kuliko johari!
11Mumewe humwamini kwa moyo,
kwake atapata faida daima.
12Kamwe hamtendei mumewe mabaya,
bali humtendea mema maisha yake yote.
13Hutafuta sufu na kitani,
na kufanya kazi kwa mikono yake kwa bidii.
14Yeye ni kama meli za biashara:
Huleta chakula chake kutoka mbali.
15Huamka kabla ya mapambazuko,
akaitayarishia jamaa yake chakula,
na kuwagawia kazi watumishi wake.
16Hufikiria kununua shamba, kisha hulinunua,
na kulima zabibu kwa faida ya jasho lake.
17Huwa tayari kufanya kazi kwa nguvu
na kuiimarisha mikono yake.
18Hutambua kwamba shughuli zake zina faida;
hufanya kazi hata usiku kwa mwanga wa taa yake.
19Husokota nyuzi kwa mikono yake mwenyewe,
kwa vidole vyake mwenyewe husuka nguo zake.
20Huufungua mkono wake kuwapa maskini,
hunyosha mkono kuwasaidia fukara.
21Hawahofii watu wake ijapo baridi ya kipupwe,
maana kila mmoja anazo nguo za kutosha.
22Hujitengenezea matandiko,
mavazi yake ni ya zambarau ya kitani safi.
23Mume wake ni mtu mashuhuri barazani,
anakoshiriki vikao vya wazee wa nchi.
24Mwanamke huyo hutengeneza nguo na kuziuza,
huwauzia wafanyabiashara mishipi.
25Nguvu na heshima ndizo sifa zake,
hucheka afikiriapo wakati ujao.
26Hufungua kinywa kunena kwa hekima,
huwashauri wengine kwa wema.
27Huchunguza yote yanayofanyika nyumbani mwake,
kamwe hakai bure hata kidogo.
28Watoto wake huamka na kumshukuru,
mumewe huimba sifa zake.
29Husema, “Wanawake wengi wametenda mambo ya ajabu,
lakini wewe umewashinda wote.”
 
Kuna mmoja jana kaja kaondoka na tisheti yangu da nime mind kinoma
Siju hawasikii noma.kuna 1 kaja kakuta boxer kibao sijazivaa ziko stok na singlend kajisevie et nzur nimezipenda.napenda boxer za kiume!daah!
 
@Edelyn,

Niliambiwa 'Nitakula kwa jasho' sikuambiwa 'utalisha kwa jasho'. Swala la kutii na kuheshimu ni amri ya Muumba kwa mwanamke.

Sasa kama mwanamke atasubiri kulishwa na mwanaume ndio amtii na kumweshimu nadhani hiyo itakuwa si heshima na utii bali kujipendekeza ili tu aweze kulishwa.
 
blackstarline, Mkuu hayo maandiko nayajua vizuri sana ila ninachoweza kusema ni kwamba wanaume mnayakumbukaga maandiko kwenye maswala yanayohusu wanawake tu ila maswala yanayowahusu wanaume mbona huwa hamyakumbuki maandiko?

Mngekuwa mnafuata maandiko msingekuwa mnachepuka na kuona ni kawaida kama wewe haujawahi kuchepuka na hautakaa uchepuke maishani mwako ndo uniambie hizo habari za kuwa mke mwema kumbuka siyo kila mwanaume anastahili mke mwema bali ni mume mwema tu ndo anayestahili huyo mke mwema
 
Niliambiwa 'Nitakula kwa jasho' sikuambiwa 'utalisha kwa jasho'. Swala la kutii na kuheshimu ni amri ya Muumba kwa mwanamke.

Sasa kama mwanamke atasubiri kulishwa na mwanaume ndio amtii na kumweshimu nadhani hiyo itakuwa si heshima na utii bali kujipendekeza ili tu aweze kulishwa.
Mbona wanaume mnafanya vitu kutegemeana na tabia za wake zenu basi acheni na wanawake wafanye vitu kutegemeana na matendo ya waume zao yaani hautaki kumhudumia mkeo halafu unataka yeye akutii?

Basi ndo maana ndoa nyingi siku hizi wanaume wanalalamika kuwa wake zako hawana utii na kwa mtazamo huo wataendelea kulalamika kila siku hakuna mwanamke anayependa kufanya majukumu mengi kuliko mume wake halafu bado akaendelea kuwa chini ya mume wake
 
Mkuu hayo maandiko nayajua vizuri sana ila ninachoweza kusema ni kwamba wanaume mnayakumbukaga maandiko kwenye maswala yanayohusu wanawake tu ila maswala yanayowahusu wanaume mbona huwa hamyakumbuki maandiko?

Mngekuwa mnafuata maandiko msingekuwa mnachepuka na kuona ni kawaida kama wewe haujawahi kuchepuka na hautakaa uchepuke maishani mwako ndo uniambie hizo habari za kuwa mke mwema kumbuka siyo kila mwanaume anastahili mke mwema bali ni mume mwema tu ndo anayestahili huyo mke mwema
Unajua kama mwanaume ni tofauti na mwanamke? Na hii elimu ya wazungu waliyotuletea ya 50 50 ni ya uongo wanataka tusielewane. Hivi leo ni ngumu kupata mahusiano imara! Nahii inaletwa na hiyo 50 50 kwa sababu wote tunakuwa tumepoteza lengo la mahusiano yetu, mwanaume akiwa nakipato kikubwa ni shida! Mwanamke akipata ndiyo balaa zaidi.
 
Sijaona uhusiano wowote kati ya huo mfumo wa 50/50 na mwanaume kuchepuka
 
Sijaona uhusiano wowote kati ya huo mfumo wa 50/50 na mwanaume kuchepuka
Kuchepuka ni swala lingine! Na pia sio wanaume wote wanao chepuka, wanao chepuka wana roho ovu hii roho ikikuingia mtu hata apewe nini ataendelea tu.
 
Kuchepuka ni swala lingine! Na pia sio wanaume wote wanao chepuka, wanao chepuka wana roho ovo hii roho ikikuingia mtu hata apewe nini ataendelea tu.
Sasa na wanaume kama hao nao wanakwambia eti wanataka wapate wake wema kama anayezungumziwa kwenye biblia yaani kuna watu wana masihara kweli
 
Back
Top Bottom