Kama kweli unataka kujua ilitakiwa umtafute anayejua akufundishe
Quran imeletwa Kwa lugha ya kiarabu na kiswahili ni mtoto wa lugha ya kiarabu Yani 95% ya misamiati ya kiswahili ni kiarabu hivyo kiswahili akina uwezo wa kutafsiri Kwa ufasaha lugha ya kiarabu
Ila maana halisi ya hiyo Aya ni hii yapa
Sema:Anayemfanyia uadui Jibrail(anajisumbua),hakika yeye(Jibrail) ameiteremsha (Qur’an) moyoni mwako,kwa idhni ya Mwenyeezi Mungu,inayosadikisha yale yaliyokuwa kabla yake,na ni uongofu na bishara ya waumini”.
Lakini pia kama kweli unataka kujua nani aliyekuwa anamletea mtume Muhammad hiyo Quran mbona Aya nyingine zipo nyingi tu ambazo hazina lugha ngumu Kwa Nini usizisome hizo
Quran 16:102 -
Sema: Ameiteremsha hii Roho takatifu kutokana na Mola wako Mlezi kwa haki, ili awathibitishe wale walio amini, na kuwa ni uwongofu, na ni bishara kwa Waislamu.