1. Kama umesoma fasihi utaona kwamba maandiko matakatifu na lugha inayotumika kwenye uandishi wa sheria ni lugha tofauti na lugha inayotumika katika uandishi wa vitabu vya sayansi, jiografia, historia au hata kilimo. Maandishi yenye maudhui ya hekima/maana iliyozama huwasilishwa kwa kutumia 'figures of speech' (misemo iliyobeba maana nzito zaidi ya kilichoelezwa) na huhitaji kufasiliwa. Ndiyo maana misemo ya hekima hutumia methali au nahau katika uwasilishaji wake wa ujumbe kwa hadhira husika. Kwenye uandishi wa sheria utakutana na misemo kama: "Judges like Caesar's wife must be beyond reproach" au "Justice must not only be done, it must also seen to be done" au "The accessory does not lead, but follows its principal" au "Where two clauses in a will are repugnant one to the other, the last in order shall prevail" au "He who is first in time has the strongest claim in law" etc. Style hii ya uandishi huwezi kuikuta katika disciplines nyingine. Hali kadhalika Biblia imeandikwa kwa style yake ambayo huwezi kuikuta katika uandishi wa kawaida. "Tufanye mtu kwa mfano wetu" ni style ya uandishi inayoonyesha "ukuu wa Mungu" (majestic/royal language). Katika sheria Judge anakuwa addressed "His lordship/Your lordship" wakati katika ku'address' watu wengine hatutumii lugha ya namna hii. Au pia Rais anakuwa addressed "His/Her Presidency/Excellency" lakini Rais ya Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) au wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) au Dodoma hatutumii "His/Her Presidency/Excellency". Baadhi ya lugha kama Kifaransa rafiki au mtu unayelingana naye cheo au umri unamsalimia "Comment ca va" (sawa na kusema "hujambo")? (katika umoja). Kama unayemsalimia ni mkubwa kwa umri au cheo unamsalimia "Comment les vous" (sawa na kusema "hamjambo")? (katika wingi). Katika lugha ya Chichewa (Malawi) kumsalimia mtu unayelingana naye umri/cheo utasema "mulibwanji?" (sawa na kusema "hujambo"? (katika umoja). Lakini kama anakuzidi umri/cheo utamsalimia "alibwanji" (sawa na kumsema "hawajambo?" (katika wingi).
2. Simulizi la Nuhu pia lina style yake uwasilishaji. Kila character katika uandishi ana style yake ya uandishi, lakini katika yote ni simulizi linaloonyesha kwamba katika yote mwisho wa siku ni Mungu ndiye anayesimama kama mshindi - kwamba nguvu za asili zinaonyesha mwisho wa siku Mungu ndiye mshindi na katika ushindi huo maisha mapya huanza. Kama umesoma literature utakumbuka matumizi ya masimulizi ya 'tragedy' au mambo yanayotisha/kuogopesha lengo lake ni nini? Ni kujenga ujasiri/kuonyesha kwamba wale wanaoweza kustahimili matatizo au magumu ya maisha ndiyo huibuka washindi, wakati wanaokata tamaa wanashindwa hata kabla ya kuanza safari yao.
3. Biblia imeandikwa katika tamaduni mbalimbali ambazo baadhi zilitumia vita kama njia ya kufikia malengo yao (kuwashinda washindani) na funzo tunalolipata katika masimulizi kama haya ni kwamba kama sisi tunaona kwamba anayeshinda katika vita ndiye jemedali/mpampanaji, Mungu ni zaidi ya huyo jemedali/yeye ndiye mshindi wa washindi. Kama unakumbuka Yesu alikuwa akiwafundisha wanafunzi wake kwamba msimwogope "mtu anayeua mwili", bali yule anayeweza "kuua mwili na roho" - maana yake ni kwamba ukiwaona watawala dhalimu usiwaogope kwa sababu hawana uwezo wa kuangamiza roho yako, bali ukimwogopa Mungu ina maana utaendelea kuishi kwa sababu wale wengine hawawezi kuangamiza roho yako.
4. Ukisoma Biblia ni sawa na mtu anayejiangalia kwenye kioo. Ukijiangalia kwenye kioo utaona sura yako, pamoja na kitu chochote kilicho karibu nawe. Biblia ni Neno la Mungu, na imeandikwa katika muktadha wa jamii za waandishi au hadhira yao, yaani ni mambo gani pia yalikuwa katika maisha yao: kama yalikuwa ya furaha yataonyeshwa (kula na kunywa) na kama yalikuwa ya vurugu (mapigano/kulipiza kisasi) na hii ina maana kwamba hata katika jamii zetu tumezungukwa na mambo mengi ya furaha au huzuni ambayo ni sehemu ya yale tunayoyafanya au fanyiana sisi kwa sisi. Ujumbe wa waandishi usingefika kama wasingeandika mambo yaliyokuwa yakitokea katika maisha yao. Mfano, ukisoma 'Kitabu cha Amos' utakuta unyama uliokuwa ukifanywa 'mtu ananunuliwa kwa bei ya kanda mbili', 'baadhi ya watu walikuwa wakichunwa ngozi', hii ni kuonyesha jinsi jamii ilikuwa imekubuhu katika kutenda maovu dhidi ya watu wenzao kwa sababu ya uchu wa mali, lakini pamoja na hayo yote Amosi aliwaasa watu wake kumtegemea Mungu, kwamba hayo yote yatapita na mwisho wa siku Mungu ndiye atakuwa mshindi.
5. Katika Kitabu cha Ayubu, mwandishi anataka kuonyesha pia kwamba hata uteseke vipi kama ukiweka imani yako kwa Mungu (ukiwa na imani thabiti) hakuna atakayeweza kukuungamiza. Shetani kuwa pamoja na 'watoto wa Mungu' ni sawa na pale wanafunzi wake walipomwambia Yesu kuhusu watu wasio na imani na wakamwambia kwamba je angetaka wakaombe moto ushuke kutoka mbinguni uwaangamize? Lakini yeye akasema "hapana, iacheni ngano ikue pamoja na magugu" na siku ya kuvuna, mvunaji ndiye anayeweza kuona vizuri ipi na ngano bora na yapi ni makapi au magugu na ataweza kutenganisha vizuri. Katika maisha yetu pia tunaona mambo mengi yako sambamba na mabaya na wakati mwingine haya mabaya si kwa level ya uovu, lakini hata hivyo yote yanatufundisha kwamba ubaya au uovu hauwezi kuushinda wema. Na ndiyo maana waliomuua Yesu walidhani wamemwangamiza/wamemumaliza kabisa! Lakini alifufuka akiwa na nguvu/uwezo zaidi wa hata kuweza kupita kwenye mlango uliofungwa bila kufunguliwa - yaana ana mwili ambao haufungwi tena na laws of nature, uwezo ambao hao waliomuua hawana. Hivyo, soma Biblia kwa lengo la kupata ujumbe na siyo kukwama kwenye matukio. Mfano, 'mwezi ukiwa bado mchanga' kabla haujaonekana vizuri mtu akiwahi kukuonyesha kwa kidole "mwezi ule..." usibaki ukiangalia kidole chake, jaribu kufuatisha kidole kule anakokuelekeza ndiko utakapopata huo mwezi na siyo kwenye kidole chake. Hata matukio yaliyo kwenye Biblia yana lengo moja la kutuelekeza/yanatupa ujumbe fulani ambao inabidi tuutafakari na siyo kubaki kwenye hayo matukio, maana tukifanya hivyo hatutapata ujumbe uliokusudiwa.