Hizi ni stori za kwenye Biblia ambazo zimeniacha na maswali sana

Hizi ni stori za kwenye Biblia ambazo zimeniacha na maswali sana

Mimi ni mkristo na ninaamini Mungu yupo na anatenda. Ila kuna mambo ukisoma kwenye biblia lazima ujiulize maswali mengi sana yanayokosa majibu. Leo nitashea nanyi mambo ambayo naona kama yana ukakasi;

1. Kwenye Mwanzo 1:26 imeandikwa kuwa Mungu alisema tuumbe mtu kwa mfano wetu. Nimejiuliza ina maana uumbaji ulifanywa nae kwa kushirikiana na wengine? Hakuwa peke yake? Hao wengine kina nani?

2. Mwanzo 6 - 10 kuna stori maarufu ya Nuhu. Hii ni stori ina ukakasi zaidi. Nikiandika maswali yote niliyojiuliza uzi utakuwa mrefu. Ninashauri mkaisome ili tuifungulie uzi wake.

3. Kutoka 11:5-6 kuna maandiko yanayosema kuwa wazaliwa wa kwanza wote wa wamisri kwa upande wa binadamu hadi wanyama watauwawa na Mungu mwenyewe ili waisraeli wapewe ruhusa ya kwenda nchi ya ahadi. Kiukweli haya yalikuwa ni mauaji ya halaiki kwa wasio na hatia. Unaambiwa hadi mzaliwa wa kwanza wa mbuzi, kuku, ng'ombe, mbwa na farasi waliuwawa. Kwanini isingetumika njia nyingine hao waisraeli wakaondoka?

4. Kitabu kizima cha Joshua kimejaa stori za mauaji matupu. Ikumbukwe Joshua alichukua nafasi ya Musa kwenye kuwaingiza waisraeli nchi ya ahadi baada ya kifo cha Musa. Nchi waliyoahidiwa ilikuwa tayari ina wakazi wake ambao ilibidi wauwawe wote ili kuwapisha waisraeli. Hivi ilishindikana vipi kufanya kama alivyofanya Mama Samia kuwatoa wamasai Ngorongoro na kuwapeleka Msomera kwa amani kabisa bila kumwaga damu? Kama leo 2024 bado kuna maeneo duniani hayajakaliwa na binadamu ilikuwaje enzi za Joshua? Ukisoma kitabu cha Joshua utaona kila sehemu waliyopita walikuwa wakiua wenyeji watakaowakuta. Kulikuwa na sababu zipi za msingi za mauaji haya yote?

5. Ayubu 1:6-12 utaona stori ya shetani alipojiunga na wana wa Mungu kupita mbele ya Mungu kumwabudu hadi Mungu akashangaa imekuwaje shetani akawa eneo lile? Baada ya hapo Mungu na Shetani wakakubaliana kwenda kumjaribu Ayubu kwa sharti la kutogusa mwili wa ajabu (kumuua). Katika yale majaribu watoto wa Ayubu waliuwawa na shetani. Naweza kusema ni mauaji yaliyokuwa na approval toka juu. Ilikuwa kazi maalum. Je, sio kwamba wawili hawa hukutana na kukubaliana baadhi ya mambo? Sio kwamba kuna kazi za shetani zina kibali maalum?
Swali la kwanza nalijibu kama ifuatavyoo hapo mungu alikuwa anaongea na yesu kwa sababu alikuwa ashaviumba viumbe vya kiroho tayari
 
Wewe bibilia haujui, nita weka ushahidi hapa uta kimbia mwenyewe first of all bibilia ni maneno ya utashi wa Paulo 3 :15 wagalatia, kwa hyo humo kuna full matango po

Wewe bibilia haujui, nita weka ushahidi hapa uta kimbia mwenyewe first of all bibilia ni maneno ya utashi wa Paulo 3 :15 wagalatia, kwa hyo humo kuna full matango pori
Ila quruan ndio imeshuka kutoka juu mbinguni? basi sawa
 
Ukweli unaujua halafu unashindwa kuuthibitisha,si ndio ujinga wenyewe,wewe sema umekaririshwa huko Sunday school
Ukweli naujua kuwa Biblia ni kitabu cha KIROHO. Sababu zake ni utimizo wa unabii ulioandikwa. Darasa hili ni kubwa. Lakini nimekutaka unipe mbadala wa Biblia.
 
Biblia ipo kiroho zaidi. Huwezi elewa baadhi ya maandiko mpaka umaanishe kumfuata Kristo.
“ili wakitazama watazame, wasione; Na wakisikia wasikie, wasielewe; Wasije wakaongoka, na kusamehewa.

— Marko 4:12

Kwa kukusaidia machache:
1. Tumfanye mtu kwa sura na mfano wetu: kumbe yupo Mungu Baba, Yesu Kristo na Roho Mtakatifu

3. Hapo kwa wazaliwa wa kwanza, kibinadamu ni wazaliwa wa kwanza ndiyo, lakini Mungu alikuwa anashughulikia miungu ya Wamisri inayompa kiburi farao. Hapo ilikuwa vita ya Mungu na miungu. Kumbuka Waisraeli walikuwa ni wazaliwa wa kwanza kwa Mungu kabla ya mataifa mengine yote.

4. Hapo kwa Joshua, kumbuka huko nyuma aliangamiza wanadamu wote na kubaki Nuhu tu sababu ya maovu mengi ya wanadamu. Kumbuka Sodoma na Gomora. Kumbuka Ninawi. Toka Adam atende dhambi, ndiyo mwanzo wa mauaji, mwanzo wa kuondoka amani duniani. Biblia inasema hakuna amani kwa wabaya. Na Yesu hakuja kuleta amani duniani bali upanga ili mtu achukiane na ndugu yake. Halafu akaleta amani yake ya kipekee tofauti na hizi amani za kidunia. Joshua aliwaua wote waliokataa kufanya shirika na Israel, na waisrael walikatazwa kuoana na watu wa maraifa mengine kwani wangewafanya Israel waabudu miungu mingine. Hata sasa tunaishi duniani Mungu akiwa na huruma lakini huruma ya Mungu haipo kwa wafu. Aliyekufa katika dhambi hakuna msamaha tena, ukomo wa huruma ya Mungu.

5. Kuhusu Ayubu. Kwani kwanin Mungu kamwacha shetani kwa muda. Hapo mwanzo Shetani alitaka kuabudiwa kwa kushawishi malaika wenzake kuwa Mungu ni dikteta. Mungu akamwacha ili kudhihirisha je, madai ya Shetani ni kweli au uongo. Akamwacha kila malaika na kila mwanadamu afanye machaguzi aidha ya kusimama na Mungu au kumwamini Shetani. Leo watu wote tunaoana Shetani ni mwongo. Tafuta kitabu cha Yashari (the book of jashar) na kitabu cha henoko (The book of enock). Utaona mengi humo
 
Angalau kwa biblia ila Kuna kitabu hiko Kuna Aya hadi leo inanifikirisha sana na sielewi kwanini wafuasi wake wanakaza shingo kukiamini

Qu'ran 2:97
Sema: Aliye kuwa ni adui wa Jibril, basi huyo ndiye aliye iteremsha Qur'ani moyoni mwako kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, inayo thibitisha yaliyo kuwa kabla yake, na ni uwongofu na bishara njema kwa Waumini.

Nani ni adui wa Jibril? Jibu ni shetani
Kwanini shetani ateremshe Quran na tunaambiwa kuran ni tukufu?

Hili swali haitatakea nikapata jibu la kuridhika
2:97 Say (O Muhammad): "Whoever is an enemy to
Jibril (Gabriel) (let him die in his fury), for indeed
he has brought it (this Qur'an) down to your heart
by Allah's permission, confirming what came before
it (i.e. the Tawrah and the Injil) and guidance and
glad tidings for the believers.
The scholars of Tafsir agree that this Ayah (2:
97-98) was revealed in response to the Jews who
claimed that Jibril (Gabriel) is an enemy of the
Jews and that Mikhail (Michael) is their friend.
 
Ukomo upo sikatai, lakini Allah ametanabaisha kupitia quraan hatma ya mwanadamu baada ya kufa , tena kimeeleza kwa upana wake na kimetoa tahadhari kwa watu , kimeeleza Uzito wa siku kwa mifano mingi tu, siyo hiyo tu kimeeleza binaadamu katokeaje , maisha ya tumboni mwa mama yake mpaka anakuja kuwa mtu yaani mimi na wewe, hakika quraani haijaacha kitu , na kitabu kisichokua na shaka,
Note hakuna kitabu cha dini iwe Buddha, taos, ukristo nk ambacho kimisema habari hizi hata Wanasayansi wenyewe wanajua habari za quraan na wakishindwa kupatajibu basi wakiinda ktk quraan wanashangaa wanakutana na majibu lukuki, pia kusomewa quraan hakutokubadilisha Iman yako

ndio hiyo iliyosema kuhusiana na mabikira 72 sio?
 
Angalau kwa biblia ila Kuna kitabu hiko Kuna Aya hadi leo inanifikirisha sana na sielewi kwanini wafuasi wake wanakaza shingo kukiamini

Qu'ran 2:97
Sema: Aliye kuwa ni adui wa Jibril, basi huyo ndiye aliye iteremsha Qur'ani moyoni mwako kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, inayo thibitisha yaliyo kuwa kabla yake, na ni uwongofu na bishara njema kwa Waumini.

Nani ni adui wa Jibril? Jibu ni shetani
Kwanini shetani ateremshe Quran na tunaambiwa kuran ni tukufu?

Hili swali haitatakea nikapata jibu la kuridhika
Kuna muda unaweza ukaona umetoa hoja nzito kumbe umeongea zaidi ya pumba za mabua ya mahindi, umeandika nini? hiyo aya aliyekwambia inatafsiriwa hivyo ni nani? kwenye kiarabu kuna vitu vinaitwa dhwamiri hizi zimetumika zaidi kwenye Qur'an, basi hiyo aya inasema hivi:-

"{ قُلۡ مَن كَانَ عَدُوࣰّا لِّجِبۡرِیلَ فَإِنَّهُۥ نَزَّلَهُۥ عَلَىٰ قَلۡبِكَ بِإِذۡنِ ٱللَّهِ مُصَدِّقࣰا لِّمَا بَیۡنَ یَدَیۡهِ وَهُدࣰى وَبُشۡرَىٰ لِلۡمُؤۡمِنِینَ }
[Surah Al-Baqarah: 97]

Aya hii iliyeteremka kwaajili ya mayahudi maana wao ndio husema kuwa jibriyl ni adui yao katika malaika tangu enzi ya musa swala na amani ziwe juu yake, na aya hizi mbili zimeshuka kuwatahariza kuwa kama wao ni maadui wa jibriyl basi yeye ndiye aliyeteremsha Qu'ran kwa mtume muhammad swala na amani ziwe juu yake kwa idhni ya allah, habari ya shetani inatoka wapi?! na aya inayofuatia baada ya hiyo inaonesha wazi makusudio ya aya ya juu, ama shetani hawezi kuteremsha Qu'ran wala haimpasii yeye kufanya hivyo.

"wala {hii Qur'an}hawakuteremka nayo mashetani, wala haiwapasii wao, na wala hawawezi, hakika hao wametengwa {mbali} na kusikia{ukumbusho....."

Qu'ran 26:210-212

Basi maadui wa jibriyl ni mayahudi.

"Basi yeyote ambaye ni adui wa Allah na malaika wake na mitume wake na jibril na miykaail, basi hakika Allah ni ni adui wa makafiri.."

Qu'ran 2:98

Usirudie tena kutafsiri Qu'ran kama unatafsiri lambert.
 
akili Ina ukomo wa kuyajua mambo ya Mungu ama Mungu mwenyewe. Kwa mfano: akili ya mwanadamu haiwezi kujua maisha baada ya maisha haya. Nini kitafuata baada ya mtu kukutwa na mauti, akili haiwezi kujua.
Kwenye Qur'an yote yameelezwa yaani historia yote ya kuanza mwanadamu mpaka mwisho wake umeelezwa, ila kuyaingiza kwenye fikra nzito kwa akili zetu ndio haiwezekani kwasababu mengi ni mambo ya ghayb, yaliyofichikana na yanayotokea kwenye ulimwengu mwingine baada ya kufa.
 
NA MTUME PAUL MWENYEWE ANAJI CONTRADICT,UKISOMA MATENDO YA MITUME 16,32,NA ...........KUNA SEHEMU ANASEMA YEYE NI MYAHUDI WA UKOO WA BENJAMINI KUNA SEHEMU ANASEMA YEYE NI MRUMI NA PIA NILIWAHISOMA KWENYE ARTICLE MOJA WANASEMA THE BOOK OF ACTS HAVE WRITTEN BY SCHOLARS AND IS HIGHLY FICTIOUS
mtume Paulo ni Myahudi wa Tarso wa kabila la Benyamini aliyezaliwa Rumi. Haya mambo yako wazi kwa mtu kuwa na uraia wa nchi mbili ni kawaida kabisa!
 
Kwenye Qur'an yote yameelezwa yaani historia yote ya kuanza mwanadamu mpaka mwisho wake umeelezwa, ila kuyaingiza kwenye fikra nzito kwa akili zetu ndio haiwezekani kwasababu mengi ni mambo ya ghayb, yaliyofichikana na yanayotokea kwenye ulimwengu mwingine baada ya kufa.
yeah, mambo ya ulimwengu wa roho akili ya mwanadamu haiwezi kuyaelewa. kamwe!
 
Ndugu nimepitia andiko lako,ila kwa uelewa mdogo nilionao juu ya biblia ni mkusanyiko wa nyaraka zilizoandikwa na wanadamu,kila waraka ulielekezwa kwa jamii fulani. Nadhani nyaraka hizi kwakuwa waandishi ni binadamu basi zina mapungufu mengi na inawezekana baadhi zimetungwa tu.
Vitabu vyote vya Dini vimeandikwa na Binadamu... hakuna kitabu kimetoka mbinguni
 
Marufuku kwenye Quran zipo kibao tuu hii inatokea tuu pale Muhammad anataka apendelewe kuanzia Kuoa yeye alioa wanawake wengi,mtoto wa mke wako au mtoto uliomchukua kumlea kuwa kama mtoto halali ilikua inakubaliwa ila baada ya kisa cha mwanae wa kambo kuwa na mwanamke mzuri kupelekea Mtume wa Allah kumtamani,Adoption ikapigwa marufuku.

Sasa kwenye swala la Mutah hakuna Aya kwenye Quran iliokuja kukataza badala yake Ilikuja Hadith kitu ambacho kwa uislam Hadith haina nguvu kukataza jambo la Quran ila Quran ndio kauli ya mwisho kuliko Hadith kutokana na hivyo ndomana Shia wanaendelea na Kuchukua vimada kwa mda na kuwalipa hela.
Acha kuzungumzia mambo ya watu wakati huyajui sheria mama kwenye uislamu ni Qu'ran na hadithi sahihi za mtume muhammad swala na amani ziwe juu yake, mtume ndiye anayeeleza maana ya Qu'ran na kuitafsiri:-

"......na tumekuteremshia wewe ukumbusho ili uwabainishie watu yale yaliyoteremshwa kwao, na ili wapate kutafakari.."

Qur'an 16:44

Hivyo mambo ya waislamu tuachie wenyewe nyie pambaneni na mafundisho yenu ya Paulo na wenzie, sisi sheria yetu imebebwa na Qu'ran na hadithi sahihi za mtume swala na amani ziwe juu yake, na elimu ya sayansi ya hadithi ni elimu wanaisoma wanafunzi na wanazijua hadithi sahihi na zilizotungwa kwa malengo ya kuuharibu uislamu, kila kitu kimechungwa na kuhifadhiwa.
 
Vitabu vyote vya Dini vimeandikwa na Binadamu... hakuna kitabu kimetoka mbinguni
Unazungumzia dini gani, nani huyo mwenye kuweza kutunga kitabu kisicho na kosa hata 1 kama Qu'ran katika viumbe yuko wapi? haiwezekani kabisa.
 
Acha kuzungumzia mambo ya watu wakati huyajui sheria mama kwenye uislamu ni Qu'ran na hadithi sahihi za mtume muhammad swala na amani ziwe juu yake, mtume ndiye anayeeleza maana ya Qu'ran na kuitafsiri:-

"......na tumekuteremshia wewe ukumbusho ili uwabainishie watu yale yaliyoteremshwa kwao, na ili wapate kutafakari.."

Qur'an 16:44

Hivyo mambo ya waislamu tuachie wenyewe nyie pambaneni na mafundisho yenu ya Paulo na wenzie, sisi sheria yetu imebebwa na Qu'ran na hadithi sahihi za mtume swala na amani ziwe juu yake, na elimu ya sayansi ya hadithi ni elimu wanaisoma wanafunzi na wanazijua hadithi sahihi na zilizotungwa kwa malengo ya kuuharibu uislamu, kila kitu kimechungwa na kuhifadhiwa.
Paulo kaenda shule,kafundisha sawasaw na Yesu Kristo alivyofundisha Sio kinyume kama mafundisho mengine yaliyofuata karne ya 7
 
Back
Top Bottom