Kuna muda unaweza ukaona umetoa hoja nzito kumbe umeongea zaidi ya pumba za mabua ya mahindi, umeandika nini? hiyo aya aliyekwambia inatafsiriwa hivyo ni nani? kwenye kiarabu kuna vitu vinaitwa dhwamiri hizi zimetumika zaidi kwenye Qur'an, basi hiyo aya inasema hivi:-
"{ قُلۡ مَن كَانَ عَدُوࣰّا لِّجِبۡرِیلَ فَإِنَّهُۥ نَزَّلَهُۥ عَلَىٰ قَلۡبِكَ بِإِذۡنِ ٱللَّهِ مُصَدِّقࣰا لِّمَا بَیۡنَ یَدَیۡهِ وَهُدࣰى وَبُشۡرَىٰ لِلۡمُؤۡمِنِینَ }
[Surah Al-Baqarah: 97]
Aya hii iliyeteremka kwaajili ya mayahudi maana wao ndio husema kuwa jibriyl ni adui yao katika malaika tangu enzi ya musa swala na amani ziwe juu yake, na aya hizi mbili zimeshuka kuwatahariza kuwa kama wao ni maadui wa jibriyl basi yeye ndiye aliyeteremsha Qu'ran kwa mtume muhammad swala na amani ziwe juu yake kwa idhni ya allah, habari ya shetani inatoka wapi?! na aya inayofuatia baada ya hiyo inaonesha wazi makusudio ya aya ya juu, ama shetani hawezi kuteremsha Qu'ran wala haimpasii yeye kufanya hivyo.
"wala {hii Qur'an}hawakuteremka nayo mashetani, wala haiwapasii wao, na wala hawawezi, hakika hao wametengwa {mbali} na kusikia{ukumbusho....."
Qu'ran 26:210-212
Basi maadui wa jibriyl ni mayahudi.
"Basi yeyote ambaye ni adui wa Allah na malaika wake na mitume wake na jibril na miykaail, basi hakika Allah ni ni adui wa makafiri.."
Qu'ran 2:98
Usirudie tena kutafsiri Qu'ran kama unatafsiri lambert.