Sheria Na Ahadi
15 Ndugu zangu, napenda nitoe mfano kutoka katika maisha ya kila siku. Hakuna mtu anayetengua wasia wa mtu au kuuongezea ukishatiwa sahihi. 16 Abrahamu alipewa ahadi yeye pamoja na mzawa wake. Lakini Maandiko hayasemi, “Na wazao wake,” Kwa maana ya wengi, bali yanasema, “Na mzawa wake,” yaani mmoja, ambaye ndiye Kristo. 17 Ninachotaka kusema ni kwamba, sheria, ambayo ilitolewa miaka mia nne na thelathini baadaye, haiwezi kutangua agano lililothibitishwa na Mungu na kulifanya duni. 18 Kwa maana, kama urithi wetu unategemea sheria, basi hauwezi tena kutegemea ahadi ya Mungu. Lakini Mungu kwa neema yake alimpa Abrahamu urithi kwa njia ya ahadi. 19 Kwa nini basi ipo sheria? Sheria iliwekwa kwa ajili ya uhalifu hadi atakapokuja yule wa uzao wa Abrahamu, ambaye ali tajwa katika ahadi hiyo. Sheria ililetwa na malaika kwa mkono wa mjumbe. 20 Lakini mjumbe huwakilisha zaidi ya mtu mmoja; bali
Lengo La Sheria
21 Je, sheria inapingana na ahadi za Mungu? La, sivyo! Kama ingetolewa sheria ambayo ingeweza kuwapa watu uzima, basi haki mbele za Mungu ingepatikana kwa kutimiza sheria. 22 Lakini Maan diko yanasema kwamba ulimwengu wote upo chini ya utawala wa dhambi, kwa sababu hiyo, ile ahadi inatolewa tu kwa njia ya imani katika Yesu Kristo na wanaoipokea ni wale wenye imani.
23 Kabla imani haijakuwepo tulikuwa tumefungwa chini ya sheria, mpaka imani ifunuliwe. 24 Kwa hiyo, sheria ilikuwa kama kiongozi wa kutufikisha kwa Kristo, ili tuhesabiwe haki kwa imani. 25 Lakini sasa kwa kuwa imani imekuja hatusimamiwi tena na sheria. 26 Ninyi nyote mmekuwa wana wa Mungu kwa kumwamini Kristo. 27 Kwa maana nyote mliobatizwa katika Kristo, mmemvaa Kristo. 28 Hakuna tena tofauti kati ya Myahudi na Mgiriki, mtumwa na mtu huru, mwanaume na mwanamke. Wote mmekuwa kitu kimoja kwa kuungana na Kristo Yesu. 29 Ikiwa ninyi ni wa Kristo, basi ni wa uzao wa Ibrahimu na ni warithi wa ahadi aliyopewa na Mungu.
Hapa unaona Paulo alikua.anawafundisha wagalatia ambao walirudi nyuma kutaka kuhesabiwa haki kwa matendo ya mwili ambacho ni kinyume kwa Wakristo wa sasa maana hatupo chini ya sheria