Hongera Kinana kwa kumjibu Tundu Lissu ila kazi bado ipo

Hongera Kinana kwa kumjibu Tundu Lissu ila kazi bado ipo

Kinana hajajibu chochote ni brainwasher, alichokisema hakina mashiko ni kama ametupa wanachama lambalamba siku ipite, personally sijaona hoja
Hata mimi nawashangaa watu ambao wanaona Kinana kajibu hoja.

Wakati wenzake amehoji ratio ya Wapiga kura na Majimbo yeye wanazungumzia idadi ya majimbo/wawakilishi.

Pia, Kile anachojaribu kuwatuhumu CDM kuwa wanachokita wao ndiyo kiwe ndicho hicho hicho wanachokifanya wao CCM.
 
Ila kwenye Katiba na Muungano hapo tutamuonea. Pale hata Malaika hawezi toa majibu yatakayoeleweka.
Mkuu, hiyo mifano ni miigo tu, alitakiwa atoe sababu za kitakwimu zenye tafiti za kisayansi bila kuwa na shaka, ukweli unabaki palepale huwezi ukamuiga jirani bila kujua sababu za msingi za maamuzi yake kama mazingira yenu na uwezo havifanani
 
Mkuu, hiyo mifano ni miigo tu, alitakiwa atoe sababu za kitakwimu zenye uwiano wa kisayansi bila kuwa na shaka, ukweli unabaki palepale huwezi ukamuiga jirani bila kujua sababu za msingi za maamuzi yake kama mazingira yenu na uwezo havifanani
Kama ulimsikiliza hoja yake ni kuwa uwakilishi wa Zanzibar unatokana na Zanzibar kuwa Nchi.

Hapa alipangua hoja ya Tundu Lissu kuhusu idadi ya watu!

Mahali pekee ambapo hata hakupaongelea ni wazanzibar kushika nafasi Tanganyika zisizohusiana na Muungano. Hapa kwa kweli tutamuonea hakuna atakayeweza kutoa maelekezo na yakaeleweka kwenye hili.

Pia issue ya Katiba imetukalia vibaya CCM
 
Kama ulimsikiliza hoja yake ni kuwa uwakilishi wa Zanzibar unatokana na Zanzibar kuwa Nchi.
Mkuu nakuelewa sana lakini tutazame kwenye resouces
Na huku bara je?
Usawa/uwiano katika kugharamia hao wabunge kwa fedha ya Muungano uko wapi
 
Mkuu nakuelewa sana lakini tutazame kwenye resouces
Na huku bara je?
Usawa/uwiano katika kugharamia hao wabunge kwa fedha ya Muungano uko wapi
Ndo mana hata Karume alitaka Nchi 1 na Serikali 1 maana ukisikiliza zinazoitwa kero za Muungano zote suluhisho lake la kweli ni Nchi 1 na Serikali 1.

Ukishaanza kutizama resources sijui basi hapo hakuna Muungano kuna mmoja anayemlalia mwenzie
 
Kuna mambo hayana majibu ya kurizisha lakini hatuwezi kumlaumu kinana kwasababu hana maamuzi nayo. Issue ya muundo wa muungano Nyerere kana kwamba alitengeneza mazingira ya kuivutia Zanzibar ili tu iwe chini ya uangalizi wa tanganyika na kusahau habari ya watanganyika wananufaika vipi.

Tanganyika fahari yetu ni kuona tupo pamoja na Zanzibar habari za kunufaika hatuna habari nayo labda kiulinzi. Tunatakiwa kuwapa motisha wazanzibar Ili wabaki nasi
 
Nape alisema ni Mtanzania Si mzanzibari.

Viongozi wengi wa juu wa CCM hawajui hadi Abdulrahman Kinana awaambie kuwa anaafikia na Tundu Lissu juu ya uZanzibari wa mheshimiwa rais Dk. Samia Suluhu Hassan
 
Viongozi wengi wa juu wa CCM hawajui hadi Abdulrahman Kinana awaambie kuwa anaafikia na Tundu Lissu juu ya uZanzibari wa mheshimiwa rais Dk. Samia Suluhu Hassan
Kinana hata ujibuji wake wa hoja na anavyoelezea mambo ana utofauti mkubwa sana na wapiga kelele wetu wa CCM
 
Abdulrahman Kinana Amvaa Tundu Lissu Suala la Rais Mzanzibari, "Nani Amekataa?".

TOKA MAKTABA:

1714928478528.png
 
Katika CCM ya sasa watu pekee ambao naweza kusema wana maarifa na uwezo wa kuweza kujibu hoja nzito za wapinzani na Watanzania ni Makamu Mwenyekiti wa chama Ndug. Abdulrahman Kinana na Katibu Mkuu Ndug. Emmanuel Nchimbi.

Kitendo cha Kinana leo kutoka na kumjibu Lissu kimeonesha kuwa japo huyu mtu sasa anazeeka ila bado ana uwezo mkubwa sana wa kujibu hoja za Wapinzania na angalau akaeleweka kwa Jamii ya watu wasomi wanaofikiri vizuri.

Pamoja na kuweza kuzijibu hoja za Tundu Lissu japo si kwa kiwango ambacho wengi walitegemea hasa kwenye maswali magumu ya Katiba yetu na masuala ya Muungano naweza kusema huko mbeleni suala la Katiba na Muungano zinaweza kuwa hoja ngumu sana kwa CCM

Maswali ya Lissu kuhusu wazanzibari kushika nafasi Tanzania Bara ambazo hazihusiani na masuala ya Muungano, pamoja na Katiba yetu kuwapa nguvu wanasiasa zaidi ya wataalam na kutoweka mazingira ya kuwawajibisha wanasiasa ni hoja nzito sana ambazo nina uhakika kwa kadri siku zinavyokwenda zitawapa wana CCM wakati mgumu sana katika kuzijibu.

Mimi ni CCM ila napenda kukiri kati ya Mambo ambayo ni lazima yafanyiwe kazi sasa ni:

1. Kukubaliana na Mawazo ya Marehemu Rais Karume kwa kuufanya Muungano wetu kuwa wa Nchi Moja na Serikali Moja

2. Kurekebisha Katiba iliyopo au kuja na Katiba mpya ambayo itaweka iwajibikaji wa Wanasiasa na Viongozi kwa Wananchi kiasi ambacho itamlazimu Kiongozi kuiheshimu na kuilinda katiba ambayo itambana kutofanya jambo lolote kinyume na Katiba.
Sidhani kama watakubali kumpa nguvu mpiga kura kuchagua viongozi.

Muasisi wa wizi wakati wa kura ni shujaa wa afrika na ndio chanzo cha umaskini wetu na unyonge wetu
 
Katika CCM ya sasa watu pekee ambao naweza kusema wana maarifa na uwezo wa kuweza kujibu hoja nzito za wapinzani na Watanzania ni Makamu Mwenyekiti wa chama Ndug. Abdulrahman Kinana na Katibu Mkuu Ndug. Emmanuel Nchimbi.

Kitendo cha Kinana leo kutoka na kumjibu Lissu kimeonesha kuwa japo huyu mtu sasa anazeeka ila bado ana uwezo mkubwa sana wa kujibu hoja za Wapinzania na angalau akaeleweka kwa Jamii ya watu wasomi wanaofikiri vizuri.

Pamoja na kuweza kuzijibu hoja za Tundu Lissu japo si kwa kiwango ambacho wengi walitegemea hasa kwenye maswali magumu ya Katiba yetu na masuala ya Muungano naweza kusema huko mbeleni suala la Katiba na Muungano zinaweza kuwa hoja ngumu sana kwa CCM

Maswali ya Lissu kuhusu wazanzibari kushika nafasi Tanzania Bara ambazo hazihusiani na masuala ya Muungano, pamoja na Katiba yetu kuwapa nguvu wanasiasa zaidi ya wataalam na kutoweka mazingira ya kuwawajibisha wanasiasa ni hoja nzito sana ambazo nina uhakika kwa kadri siku zinavyokwenda zitawapa wana CCM wakati mgumu sana katika kuzijibu.

Mimi ni CCM ila napenda kukiri kati ya Mambo ambayo ni lazima yafanyiwe kazi sasa ni:

1. Kukubaliana na Mawazo ya Marehemu Rais Karume kwa kuufanya Muungano wetu kuwa wa Nchi Moja na Serikali Moja

2. Kurekebisha Katiba iliyopo au kuja na Katiba mpya ambayo itaweka iwajibikaji wa Wanasiasa na Viongozi kwa Wananchi kiasi ambacho itamlazimu Kiongozi kuiheshimu na kuilinda katiba ambayo itambana kutofanya jambo lolote kinyume na Katiba.
Limejibu Nini tapeli na zee la hovyo hilo
 
05 May 2024

Abdulrahman Kinana Amvaa Tundu Lissu Suala la Rais Mzanzibari, "Nani Amekataa?
".

View: https://m.youtube.com/watch?v=zFJ1jRSRBXs
Leo Mei 5,2024, Makamu Mwenyekiti wa CCM anazungumza na waandishi wa habari na wanaCCM katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Dodoma. Anategemewa kuzungumzia masuala mbalimbali ikiwemo kujibu shutuma mbalimbali zilizoibuliwa na upinzani ambazo CCM wameziita ni za kibaguzi dhidi ya Muungano.

Hii statement inahitaji mjadala:

"Ndivyo tulivyokubaliana kuwa mgombea u - Rais akitoka bara, mgombea mwenza atatoka Zanzibar".

Swali kwa CCM na Kinana:

Hivi kina nani walikubaliana haya? Wananchi au viongozi wa CCM hasa Nyerere na Karume..​

All in all, Abdulhaman Kinana na CCM bado hawajajibu maswali ya Tundu Lissu na watanzania tunaoitakia mema Tanganyika kuhusu upogo ulioko kwenye katiba.

Ndugu Abdulhaman Kinana na CCM, msingi wa hoja za Tundu Lissu uko kwenye katiba zote ya JMT (1977) na Zanzibar (1984)..

Lakini cha ajabu, Kinana anikwepa katiba na badala yake anapiga propaganda za Rais Samia kajenga barabara, shule nk

Huku ni kukwepa kukabili hoja na ni kuahirisha matatizo ambayo huko mbeleni yanaweza kuiwasha moto nchi hii..
 
Hivi statement inahitaji mjadala: "Ndivyo tulivyokubaliana kuwa mgombea u - Rais akitoka bara, mgombea mwenza atatoka Zanzibar".

Swali kwa CCM na Kinana
: Hivi kina nani walikubaliana haya? Wananchi au viongozi wa CCM hasa Nyerere na Karume..

All in all, Abdulhaman Kinana bado hajajibu maswali ya Tundu Lissu kuhusu upogo ulioko kwenye katiba.

Ndugu Abdulhaman Kinana na CCM, msingi wa hoja za Tundu Lissu uko kwenye katiba zote ya JMT (1977) na Zanzibar (1984)..

Lakini cha ajabu, Kinana anikwepa katiba na badala yake anapiga propaganda za Rais Samia kajenga barabara, shule nk

Huku ni kukwepa kukabili hoja na ni kuahirisha matatizo ambayo huko mbeleni kutawaka moto..
Kwenye Katiba na Muungano tutamuonea tu Kinana. Lile ni fupa gumu ambalo hakuna anayeweza kutoa majibu akaelewa awe ndani ya CCM au hata atoke mbinguni.

Kati ya vitu ambavyo CCM tunatakiwa kurekebisha haraka ni kuunda muungano wa Serikali 1 na nchi moja na kuweka Katiba Mpya.

Watu wakizidi kuamka kwenye haya huko mbeleni tutagawana mbao
 
kinana hana majibu ya hoja za lisu, kinana anatafuta hoja nyepesi kukwepa hoja halisi za lisu, Rais wa sasa wa JMT ni raia wa Tanzania kwa kuzaliwa ama kuhamia?, zanzibar nayo ni nchi huru maana ina bendera yake, waatu wake, katiba yake na serikali yake....mtu akija tanganyika akiwa anatokea zanzibar huyo mtu anakuwa mkimbizi, so tumemkabidhi nchi mkimbizi au sio? ....kuna mtu mkubwa mmoja alisema tumewakabidhi wakimbizi nchi yetu...tena tumewapa nafasi za juu kabisa za nchi..ndio haya mambo sasa naona
 
Kwenye Katiba na Muungano tutamuonea tu Kinana. Lile ni fupa gumu ambalo hakuna anayeweza kutoa majibu akaelewa awe ndani ya CCM au hata atoke mbinguni.
Hii statement; "....Si Kinana wala CCM anaweza kutoa majibu kuhusu katiba ya JMT hata kama atatoka mbinguni na akaeleweka.." una maanisha nini hasa? Kwamba, tulishajiingiza kwenye shida wenyewe na hivyo ni halali yetu kubaki huko milele?
Kati ya vitu ambavyo CCM tunatakiwa kurekebisha haraka ni kuunda muungano wa Serikali 1 na nchi moja na kuweka Katiba Mpya.
Hii ni ngumu na haikubaliki kamwe kwa Wazanzibari. Hawa wanapenda sana kujitambulisha kwa utaifa wao. Ni ngumu kuwatoa hapo kwa kuifuta Zanzibar na uzanzibari wao. Muungano wa serikali moja kwa mambo yalivyo Sasa, it's almost impossible for more than 95%

Options zilizopo ni mbili tu:

1. Serikali tatu ndani ya muungano (Ya Muungano, Tanganyika na Zanzibar) Hizi mbili za mwisho (Tanganyika na Zanzibar) zihusike na mambo yao ya ndani yasiyo ya muungano. Na ile ya muungano ishughulike na issues za muungano pekee. Ikiwa hivi, obviously tutaelewana. Muungano wa namna hii, CCM mnauogopa sana na sababu za hofu zenu ni za kisiasa na madaraka. Na ofcoz uwepo wa CCM mpaka Sasa ni kwa sababu ya uwepo wa muungano huu mbovu wa kimagumashi..

2. La hatuwezi kuwa na muungano wa serikali tatu, basi tupige kura ya maoni ya kuendelea na muungano wa dizaini hii au tugawane mbao kila nchi ianze kuishi kivyake..

##Hizi mbili ndizo Suluhu za kuliondoa zimwi hili..
 
Mfumo huu wa Muungano ni wazo la Nyerere na wala halikuwa pendekezo la Karume.

Kwa hali ilivyo na tunavyoelekea huko mbele itakuwa shida sana kuutetea huu muungano hasa watanganyika wakiona kuna watu wananufaika zaidi na what is called Muungano kuliko wao.

Hata zinazosemwa kero za Muungano ukiangalia kwa undani suluhisho lake sio Serikali 2 au 3 bali ni Serikali 1

Kuna mambo kama tunaipenda lweli nchi yetu ni lazima tuyafanyie maamuzi sasa.
Huu muungano nahisi una mambo ya matambiko ndani yake, ndio maana unatetewa kwa hoja nyepesi, huku udhaifu wake ukiwa wazi kuliko kiwango Cha utetezi wake.
 
Sera ya muungano ilikuwa hoja ya act wazakendo, sera ya muungano ilikuwa sera ya DP sasa hawa washenzi washaacha sera zao za kupambana na ufisadi na kupigania utalawala wa majimbo sasa wamerukia sera zingine kabisa yaani wanayumba ka ngama ya wakara
Hakuna haki miliki ya hoja, kumbuka elimu bure ilikuwa ajenda ya cdm ccm wakarukia. Ama hujui unaoongea Nini dogo?
 
Kama ulimsikiliza hoja yake ni kuwa uwakilishi wa Zanzibar unatokana na Zanzibar kuwa Nchi.

Hapa alipangua hoja ya Tundu Lissu kuhusu idadi ya watu!

Mahali pekee ambapo hata hakupaongelea ni wazanzibar kushika nafasi Tanganyika zisizohusiana na Muungano. Hapa kwa kweli tutamuonea hakuna atakayeweza kutoa maelekezo na yakaeleweka kwenye hili.

Pia issue ya Katiba imetukalia vibaya CCM

Lakini katiba ya Tanzania haiitambui Zanzibar kama nchi.
 
Kama ulimsikiliza hoja yake ni kuwa uwakilishi wa Zanzibar unatokana na Zanzibar kuwa Nchi.

Hapa alipangua hoja ya Tundu Lissu kuhusu idadi ya watu!

Mahali pekee ambapo hata hakupaongelea ni wazanzibar kushika nafasi Tanganyika zisizohusiana na Muungano. Hapa kwa kweli tutamuonea hakuna atakayeweza kutoa maelekezo na yakaeleweka kwenye hili.

Pia issue ya Katiba imetukalia vibaya CCM
Ukituliza kichwa ,unaanza kuona jinsi Mh Rais anavyoachwa na anaoamini wanaweza kuona mitego iliyopo...inatolewa hoja halisi kwa njia ya mzunguko,masikini viongozi wanaivamia na kuijibu bila tahadhari ,baada ya kuijibu ndipo sisi watu tunapoona jinsi walivyo na mkwamo wa kufikiri..
 
Back
Top Bottom