Mfumo huu wa Muungano ni wazo la Nyerere na wala halikuwa pendekezo la Karume.
Kwa hali ilivyo na tunavyoelekea huko mbele itakuwa shida sana kuutetea huu muungano hasa watanganyika wakiona kuna watu wananufaika zaidi na what is called Muungano kuliko wao.
Hata zinazosemwa kero za Muungano ukiangalia kwa undani suluhisho lake sio Serikali 2 au 3 bali ni Serikali 1
Kuna mambo kama tunaipenda lweli nchi yetu ni lazima tuyafanyie maamuzi sasa.
Mambo madogo sana haya. Watanzania tuko 61 Million na ardhi yetu ina 945,000 Sqaure kilometres za ukubwa.
Zanzibar wako 1.2 Million na ukubwa wa 2,460 Square kilometres.
Ni aibu leo watu 61 Million kuanza kugombea ki-ardhi kidogo namna hiyo wakati huku kumejaa mapori makubwa ya kutisha.
Hizo fursa za kazi unazozitaka ZNZ ziko wapi? Kama elimu yako na uwezo wako hauwezi kukupatia ajira hapa Bara penye uchumi wa GDP ya USD 85 Billion ndiyo ukabamane na GDP ya ZNZ ambayo USD 3.75??
Tunahitaji kubadilisha mtazamo tu. Tatizo letu kubwa ni umaskini. Zanzibar ingekuwa tajiri kama Qatar, mengi ya yanayosemwa wala isingekuwa issue. Kama sikosei, Area Commissioners from Zanzibar au positions nyingine zimepewa Watu wa upande mwingine wa Mwungano toka enzi za Mwalimu.
Na hizi feelings zikipewa nafasi, zinaweza hata kuleta issues kati ya movements za watu mikoani. Kuna watu, suddenly, watadai wakuu wa mikoa, wilaya, watoke katika mkoa huo huo.
Mikoa kama ya Mbeya, Mwanza, Kilimanjaro, Arusha ina mchango mkubwa kiuchumi kuliko mikoa mingine kama Tabora, Singida, Kigoma, Mtwara. What if hao wenye uchumi mkubwa wakaona wanannyonywa au kutawaliwa na watu wa mikoa maskini?