The Khoisan
JF-Expert Member
- Jun 5, 2007
- 16,434
- 14,547
Hata mimi nawashangaa watu ambao wanaona Kinana kajibu hoja.Kinana hajajibu chochote ni brainwasher, alichokisema hakina mashiko ni kama ametupa wanachama lambalamba siku ipite, personally sijaona hoja
Mkuu, hiyo mifano ni miigo tu, alitakiwa atoe sababu za kitakwimu zenye tafiti za kisayansi bila kuwa na shaka, ukweli unabaki palepale huwezi ukamuiga jirani bila kujua sababu za msingi za maamuzi yake kama mazingira yenu na uwezo havifananiIla kwenye Katiba na Muungano hapo tutamuonea. Pale hata Malaika hawezi toa majibu yatakayoeleweka.
Kama ulimsikiliza hoja yake ni kuwa uwakilishi wa Zanzibar unatokana na Zanzibar kuwa Nchi.Mkuu, hiyo mifano ni miigo tu, alitakiwa atoe sababu za kitakwimu zenye uwiano wa kisayansi bila kuwa na shaka, ukweli unabaki palepale huwezi ukamuiga jirani bila kujua sababu za msingi za maamuzi yake kama mazingira yenu na uwezo havifanani
Mkuu nakuelewa sana lakini tutazame kwenye resoucesKama ulimsikiliza hoja yake ni kuwa uwakilishi wa Zanzibar unatokana na Zanzibar kuwa Nchi.
Ndo mana hata Karume alitaka Nchi 1 na Serikali 1 maana ukisikiliza zinazoitwa kero za Muungano zote suluhisho lake la kweli ni Nchi 1 na Serikali 1.Mkuu nakuelewa sana lakini tutazame kwenye resouces
Na huku bara je?
Usawa/uwiano katika kugharamia hao wabunge kwa fedha ya Muungano uko wapi
👍✔️Ndo mana hata Karume alitaka Nchi 1 na Serikali 1 maana ukisikiliza zinazoitwa kero za Muungano zote suluhisho lake la kweli ni Nchi 1 na Serikali 1.
Nape alisema ni Mtanzania Si mzanzibari.
Kinana hata ujibuji wake wa hoja na anavyoelezea mambo ana utofauti mkubwa sana na wapiga kelele wetu wa CCMViongozi wengi wa juu wa CCM hawajui hadi Abdulrahman Kinana awaambie kuwa anaafikia na Tundu Lissu juu ya uZanzibari wa mheshimiwa rais Dk. Samia Suluhu Hassan
Abdulrahman Kinana Amvaa Tundu Lissu Suala la Rais Mzanzibari, "Nani Amekataa?".
Sidhani kama watakubali kumpa nguvu mpiga kura kuchagua viongozi.Katika CCM ya sasa watu pekee ambao naweza kusema wana maarifa na uwezo wa kuweza kujibu hoja nzito za wapinzani na Watanzania ni Makamu Mwenyekiti wa chama Ndug. Abdulrahman Kinana na Katibu Mkuu Ndug. Emmanuel Nchimbi.
Kitendo cha Kinana leo kutoka na kumjibu Lissu kimeonesha kuwa japo huyu mtu sasa anazeeka ila bado ana uwezo mkubwa sana wa kujibu hoja za Wapinzania na angalau akaeleweka kwa Jamii ya watu wasomi wanaofikiri vizuri.
Pamoja na kuweza kuzijibu hoja za Tundu Lissu japo si kwa kiwango ambacho wengi walitegemea hasa kwenye maswali magumu ya Katiba yetu na masuala ya Muungano naweza kusema huko mbeleni suala la Katiba na Muungano zinaweza kuwa hoja ngumu sana kwa CCM
Maswali ya Lissu kuhusu wazanzibari kushika nafasi Tanzania Bara ambazo hazihusiani na masuala ya Muungano, pamoja na Katiba yetu kuwapa nguvu wanasiasa zaidi ya wataalam na kutoweka mazingira ya kuwawajibisha wanasiasa ni hoja nzito sana ambazo nina uhakika kwa kadri siku zinavyokwenda zitawapa wana CCM wakati mgumu sana katika kuzijibu.
Mimi ni CCM ila napenda kukiri kati ya Mambo ambayo ni lazima yafanyiwe kazi sasa ni:
1. Kukubaliana na Mawazo ya Marehemu Rais Karume kwa kuufanya Muungano wetu kuwa wa Nchi Moja na Serikali Moja
2. Kurekebisha Katiba iliyopo au kuja na Katiba mpya ambayo itaweka iwajibikaji wa Wanasiasa na Viongozi kwa Wananchi kiasi ambacho itamlazimu Kiongozi kuiheshimu na kuilinda katiba ambayo itambana kutofanya jambo lolote kinyume na Katiba.
Limejibu Nini tapeli na zee la hovyo hiloKatika CCM ya sasa watu pekee ambao naweza kusema wana maarifa na uwezo wa kuweza kujibu hoja nzito za wapinzani na Watanzania ni Makamu Mwenyekiti wa chama Ndug. Abdulrahman Kinana na Katibu Mkuu Ndug. Emmanuel Nchimbi.
Kitendo cha Kinana leo kutoka na kumjibu Lissu kimeonesha kuwa japo huyu mtu sasa anazeeka ila bado ana uwezo mkubwa sana wa kujibu hoja za Wapinzania na angalau akaeleweka kwa Jamii ya watu wasomi wanaofikiri vizuri.
Pamoja na kuweza kuzijibu hoja za Tundu Lissu japo si kwa kiwango ambacho wengi walitegemea hasa kwenye maswali magumu ya Katiba yetu na masuala ya Muungano naweza kusema huko mbeleni suala la Katiba na Muungano zinaweza kuwa hoja ngumu sana kwa CCM
Maswali ya Lissu kuhusu wazanzibari kushika nafasi Tanzania Bara ambazo hazihusiani na masuala ya Muungano, pamoja na Katiba yetu kuwapa nguvu wanasiasa zaidi ya wataalam na kutoweka mazingira ya kuwawajibisha wanasiasa ni hoja nzito sana ambazo nina uhakika kwa kadri siku zinavyokwenda zitawapa wana CCM wakati mgumu sana katika kuzijibu.
Mimi ni CCM ila napenda kukiri kati ya Mambo ambayo ni lazima yafanyiwe kazi sasa ni:
1. Kukubaliana na Mawazo ya Marehemu Rais Karume kwa kuufanya Muungano wetu kuwa wa Nchi Moja na Serikali Moja
2. Kurekebisha Katiba iliyopo au kuja na Katiba mpya ambayo itaweka iwajibikaji wa Wanasiasa na Viongozi kwa Wananchi kiasi ambacho itamlazimu Kiongozi kuiheshimu na kuilinda katiba ambayo itambana kutofanya jambo lolote kinyume na Katiba.
Hii statement inahitaji mjadala:05 May 2024
Abdulrahman Kinana Amvaa Tundu Lissu Suala la Rais Mzanzibari, "Nani Amekataa?".
View: https://m.youtube.com/watch?v=zFJ1jRSRBXsLeo Mei 5,2024, Makamu Mwenyekiti wa CCM anazungumza na waandishi wa habari na wanaCCM katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Dodoma. Anategemewa kuzungumzia masuala mbalimbali ikiwemo kujibu shutuma mbalimbali zilizoibuliwa na upinzani ambazo CCM wameziita ni za kibaguzi dhidi ya Muungano.
Kwenye Katiba na Muungano tutamuonea tu Kinana. Lile ni fupa gumu ambalo hakuna anayeweza kutoa majibu akaelewa awe ndani ya CCM au hata atoke mbinguni.Hivi statement inahitaji mjadala: "Ndivyo tulivyokubaliana kuwa mgombea u - Rais akitoka bara, mgombea mwenza atatoka Zanzibar".
Swali kwa CCM na Kinana: Hivi kina nani walikubaliana haya? Wananchi au viongozi wa CCM hasa Nyerere na Karume..
All in all, Abdulhaman Kinana bado hajajibu maswali ya Tundu Lissu kuhusu upogo ulioko kwenye katiba.
Ndugu Abdulhaman Kinana na CCM, msingi wa hoja za Tundu Lissu uko kwenye katiba zote ya JMT (1977) na Zanzibar (1984)..
Lakini cha ajabu, Kinana anikwepa katiba na badala yake anapiga propaganda za Rais Samia kajenga barabara, shule nk
Huku ni kukwepa kukabili hoja na ni kuahirisha matatizo ambayo huko mbeleni kutawaka moto..
Hii statement; "....Si Kinana wala CCM anaweza kutoa majibu kuhusu katiba ya JMT hata kama atatoka mbinguni na akaeleweka.." una maanisha nini hasa? Kwamba, tulishajiingiza kwenye shida wenyewe na hivyo ni halali yetu kubaki huko milele?Kwenye Katiba na Muungano tutamuonea tu Kinana. Lile ni fupa gumu ambalo hakuna anayeweza kutoa majibu akaelewa awe ndani ya CCM au hata atoke mbinguni.
Hii ni ngumu na haikubaliki kamwe kwa Wazanzibari. Hawa wanapenda sana kujitambulisha kwa utaifa wao. Ni ngumu kuwatoa hapo kwa kuifuta Zanzibar na uzanzibari wao. Muungano wa serikali moja kwa mambo yalivyo Sasa, it's almost impossible for more than 95%Kati ya vitu ambavyo CCM tunatakiwa kurekebisha haraka ni kuunda muungano wa Serikali 1 na nchi moja na kuweka Katiba Mpya.
Huu muungano nahisi una mambo ya matambiko ndani yake, ndio maana unatetewa kwa hoja nyepesi, huku udhaifu wake ukiwa wazi kuliko kiwango Cha utetezi wake.Mfumo huu wa Muungano ni wazo la Nyerere na wala halikuwa pendekezo la Karume.
Kwa hali ilivyo na tunavyoelekea huko mbele itakuwa shida sana kuutetea huu muungano hasa watanganyika wakiona kuna watu wananufaika zaidi na what is called Muungano kuliko wao.
Hata zinazosemwa kero za Muungano ukiangalia kwa undani suluhisho lake sio Serikali 2 au 3 bali ni Serikali 1
Kuna mambo kama tunaipenda lweli nchi yetu ni lazima tuyafanyie maamuzi sasa.
Hakuna haki miliki ya hoja, kumbuka elimu bure ilikuwa ajenda ya cdm ccm wakarukia. Ama hujui unaoongea Nini dogo?Sera ya muungano ilikuwa hoja ya act wazakendo, sera ya muungano ilikuwa sera ya DP sasa hawa washenzi washaacha sera zao za kupambana na ufisadi na kupigania utalawala wa majimbo sasa wamerukia sera zingine kabisa yaani wanayumba ka ngama ya wakara
Kama ulimsikiliza hoja yake ni kuwa uwakilishi wa Zanzibar unatokana na Zanzibar kuwa Nchi.
Hapa alipangua hoja ya Tundu Lissu kuhusu idadi ya watu!
Mahali pekee ambapo hata hakupaongelea ni wazanzibar kushika nafasi Tanganyika zisizohusiana na Muungano. Hapa kwa kweli tutamuonea hakuna atakayeweza kutoa maelekezo na yakaeleweka kwenye hili.
Pia issue ya Katiba imetukalia vibaya CCM
Ukituliza kichwa ,unaanza kuona jinsi Mh Rais anavyoachwa na anaoamini wanaweza kuona mitego iliyopo...inatolewa hoja halisi kwa njia ya mzunguko,masikini viongozi wanaivamia na kuijibu bila tahadhari ,baada ya kuijibu ndipo sisi watu tunapoona jinsi walivyo na mkwamo wa kufikiri..Kama ulimsikiliza hoja yake ni kuwa uwakilishi wa Zanzibar unatokana na Zanzibar kuwa Nchi.