25 Aprili 2025
JAMIIFORUMS NI JUKWAA KUBWA LA MEDIA, NAAMINI WATU WAMEITAFAKARI HOTUBA PIA TOFAUTI NA MEDIA ZINGINE TUNAWEZA KUIJADILI ILI KUJENGA TAIFA
Leo mheshimiwa rais wa Jamhuri ya Muungano, jioni tarehe 25 Aprili 2025 alitoa hotuba inayo semekana aliongea na taifa.
Je wewe kama mwananchi ulipata wasaa wa kuitazama au kuisikiliza ulikuwa na matarajio yapi hotuba hiyo ya mkuu wa nchi angegusia.
Uzi huu ni maalamu kwa ajili ya kutoa mrejesho, ili wananchi na viongozi wasitofautiane sana matarajio yao.
Na pia mrejesho wenu wananchi, unaweza kutoa dira kwa viongozi kuwa wananchi wana mambo gani wanadhani rais na wateule wake wangetekeleza na sababu zao ni zipi.
View attachment 3315718
Mheshimiwa Rais Samia Hassan alipokuwa anaongea na taifa.
N.B
Mrejesho wa raia kwa viongozi ni jambo jema. Hii ndiyo nafasi adimu ya kuzungumza na viongozi moja kwa moja baada ya hotuba, matamko n.k kutoka kwa viongozi walio ktk ofisi za umma.