Hotuba ya Rais Samia ikipishana na matarajio ya raia, ina maana gani?

Hotuba ya Rais Samia ikipishana na matarajio ya raia, ina maana gani?

Utaniwia radhi mkuu mleta mada. Pamoja na yote uliyohimiza wachangiaji tuyatafakari na kuleta mrejesho kuhusu hotuba hiyo ya kiongozi; mimi maoni yangu yameishia kwenye kuiangalia hiyo picha ya Rais hapo juu.
Kwa mara ya kwanza namtazama kitofauti sana na nilivyo mwona huko siku za nyuma.

Sipendezewi na sura ya huyu kiongozi wetu.
Huu ndio mchango wangu kwa mada hii.
binafsi niwe mkweli, huwa ninashindwa kumwangalia hata kama ni kwenye picha.
 
Selassie na Ghadafi sijawahi kuwasikia.

Kuna li mtaa kuuubwa Dar linaitwa Haille Selasie. 99% of Watanzania we have no freaking clue Selassie alisema nini, alisimamia nini. Mbona tunaenda mbali mno kutafuta ma hero ?

Pombe Magufuli kila alipoongea na Taifa kesho yake uswahilini tulifanya vijiwe na kuulizana, ee banah ee ulimsikia yule Mwamba ??? Siku zote ana jambo impactfull au nation shocking!!!

Give the devil his due. Hata shetani ana sifa zake. Magufuli akiongea dunia inam quote kwenye New York Times! Hahahaaaaa....

Jana Samia kaongea.
Sikujua. Na sina shauku ya kujua kasema nini. Haya, wanasema kaongelea nishani. Military police wamesimama kwenye ma pick up kila mahala tayari kuua, na raia mmoja kafa, kapigwa rungu la kichwa geti la kisutu. Unaongeleaje nishani ??? Unatuchukuliaje yani ??

her time is running out! Mungu wa mbinguni hadhihakiwi!
 
25 Aprili 2025

JAMIIFORUMS NI JUKWAA KUBWA LA MEDIA, NAAMINI WATU WAMEITAFAKARI HOTUBA PIA TOFAUTI NA MEDIA ZINGINE TUNAWEZA KUIJADILI ILI KUJENGA TAIFA

Leo mheshimiwa rais wa Jamhuri ya Muungano, jioni tarehe 25 Aprili 2025 alitoa hotuba inayo semekana aliongea na taifa.

Je wewe kama mwananchi ulipata wasaa wa kuitazama au kuisikiliza ulikuwa na matarajio yapi hotuba hiyo ya mkuu wa nchi angegusia.

Uzi huu ni maalamu kwa ajili ya kutoa mrejesho, ili wananchi na viongozi wasitofautiane sana matarajio yao.

Na pia mrejesho wenu wananchi, unaweza kutoa dira kwa viongozi kuwa wananchi wana mambo gani wanadhani rais na wateule wake wangetekeleza na sababu zao ni zipi.
View attachment 3315718
Mheshimiwa Rais Samia Hassan alipokuwa anaongea na taifa.


N.B
Mrejesho wa raia kwa viongozi ni jambo jema. Hii ndiyo nafasi adimu ya kuzungumza na viongozi moja kwa moja baada ya hotuba, matamko n.k kutoka kwa viongozi walio ktk ofisi za umma.
Ilikuwa hotuba ya hovyo iliyozungumzia mambo juu juu. Inaonyesha Samia ana kiburi cha kimamlaka. Yani anajiona kuwa yeye ndiye chuma na hawezi kujishusha kwa wengine.
 
Hotuba ni hopeless , haina mvuto….. pia Imekosa tija…. Aliemuandikia kamuingiza cha kiume …. Bad timing ….. kwa yanayoendelea …. Wengi wamepoteza heshima na matumaini nae ….. zamani ilikuwa ukisikia hotuba ya Rais … watu walikuwa wanawahi siti za mbele….

Sasa kwenye hiyo hotuba kuna
Kipi kigeni au cha maana.

Samia Apumzike… amechoka na
Yeye anajua hilo

Nchi haina Dira…..anaonya taasisi za umma na binafsi kutokuwa juu ya sheria, really ? Hivi Madam yupo hata serious kweli ….? Usikute sisi ndio tupo serious wakati yeye wala….. she is just playing joke cards
Hana uchungu kabisa na watanganyika yeye yupo bize kuchuma na kupeleka kizimkazi
 
Jambo gani gumu kaliacha zaidi ya Muungano tunaosheherekea Leo, Uchaguzi Mkuu tunaofanya mwaka huu na amani na utulivu wa nchi kwa kipindi chote? Kasahau nini hapo?
Rudiii shulee,watoto waendee shulee watusaidie baadayeee
 
Mh Rais wa Tanzania kwanza nianze kwa kukusalimia Mh Rais Shikamoo
Baada ya salamu Mh Rais naomba nikili binafsi sijakuelewa katika hotuba Yako yote nimekusilikiza na nmeisoma iliyotumwa mitandaoni nakili sijakuelewa

Mh Rais ebu nijuze ni nani anatishia amani ya nchi ya Tanzania
Kati ya Hawa watu?
Anaetaka tume huru ya uchaguzi au hasiyetaka ambaye ni wewe na chama chako?

Mh Rais niamini UTAWALA wa Nyerere, Mwinyi mkapa na kikwete sio sawa na utawala wako, watu wameelimika vyakutoaha mama yangu kweli watanzania tulitaka Mh Rais usionekane paspo kupaka ripustiki kwenye midomo Yako mbele za wageni?

Watu wanataka tume huru ya uchaguzi wewe na wenzako mnabadili Jina kutoka tume ya uchaguzi kuja tume huru ya uchaguzi?

Watu wanasema wasimamizi wa uchaguzi wasiwe wateule wako waombe KAZI waajiliwe au tuwapigie kura wale wenye maadili Bado wewe utaki.

Tunakwambia uchaguzi usimamiwe na mkweo, wewe unasema mkweo anakifua ataweza kusimamia hivi anaweza kusimamia uchaguzi uwe huru na haki Ili mama mkwe wake ashindwe?

Mh Rais serikali ya MUUNGANO ni kiini macho zanzibari Wana Rais, Wana bendera Yao Wana wimbo wa TAIFA WA kwao sie Tanganyika chetu viko wapi?

Mh Rais 4R zako sio zisitumike kama sababu kuvunja amani ya nchi nani anazitumia vibaya hivyo?
Wewe ulie zileta ukizitekeleza vyema je wapi amani itavunjika?

Tatzo lipo kwako ulizitumia kuwalaghai wapinzani Hasa chadema lakini katika kuzitekeleza ukaona itakuwa noma ukapiga chini.

Mh Rais tafta namna uhutubie taifa la Tanzania Mimi binafsi sijakuelewa kabisa.
 
Napita nitafuatilia mrejesho wa wajibu ya maswali na hoja panapo majaaliwa.Najua ni matarajio ya wengi kuwa yapo maswali kuliko majibu kama nilivyo pia.
 
Back
Top Bottom