Hotuba ya Rais Samia ikipishana na matarajio ya raia, ina maana gani?

Hotuba ya Rais Samia ikipishana na matarajio ya raia, ina maana gani?

Hotuba ni hopeless , haina mvuto….. pia Imekosa tija…. Aliemuandikia kamuingiza cha kiume …. Bad timing ….. kwa yanayoendelea …. Wengi wamepoteza heshima na matumaini nae ….. zamani ilikuwa ukisikia hotuba ya Rais … watu walikuwa wanawahi siti za mbele….

Sasa kwenye hiyo hotuba kuna
Kipi kigeni au cha maana.

Samia Apumzike… amechoka na
Yeye anajua hilo

Nchi haina Dira…..anaonya taasisi za umma na binafsi kutokuwa juu ya sheria, really ? Hivi Madam yupo hata serious kweli ….? Usikute sisi ndio tupo serious wakati yeye wala….. she is just playing joke cards

Anadai hakuna sliye juu ya sheria wakati yeye na akina Mriro wanayoyafanya yako juu na kinyume cha sheria
 
25 Aprili 2025

JAMIIFORUMS NI JUKWAA KUBWA LA MEDIA, NAAMINI WATU WAMEITAFAKARI HOTUBA PIA TOFAUTI NA MEDIA ZINGINE TUNAWEZA KUIJADILI ILI KUJENGA TAIFA

Leo mheshimiwa rais wa Jamhuri ya Muungano, jioni tarehe 25 Aprili 2025 alitoa hotuba inayo semekana aliongea na taifa.

Je wewe kama mwananchi ulipata wasaa wa kuitazama au kuisikiliza ulikuwa na matarajio yapi hotuba hiyo ya mkuu wa nchi angegusia.

Uzi huu ni maalamu kwa ajili ya kutoa mrejesho, ili wananchi na viongozi wasitofautiane sana matarajio yao.

Na pia mrejesho wenu wananchi, unaweza kutoa dira kwa viongozi kuwa wananchi wana mambo gani wanadhani rais na wateule wake wangetekeleza na sababu zao ni zipi.
View attachment 3315718
Mheshimiwa Rais Samia Hassan alipokuwa anaongea na taifa.


N.B
Mrejesho wa raia kwa viongozi ni jambo jema. Hii ndiyo nafasi adimu ya kuzungumza na viongozi moja kwa moja baada ya hotuba, matamko n.k kutoka kwa viongozi walio ktk ofisi za umma.
Hotuba hata Lucas Mshambwa na wenzake wanapata mtihani kuipaka mafuta kwa mgongo wa chupa....
 
Kuna vitu nimejifunza toka kwa mama,kwa kipindi mpk amefikia hapa:
Km ni mfuatiliaji mzuri wa siasa,western like US kila wanachotaka kufanya lazima watangaze chochote kile,raisi/senetor lazima akiseme;
Ukienda Russia/China/Asia unaona matendo tu na mara chache sana utasikia wanatamka hukumu/jinsi wanavyotatua mambo ya ndani.
Mama siasa zake ni kama za Asia/Russia na ndio maana hata maadui wa hizo nchi wanapata shida sana kujua wanawaza nini.
Simtetei mtu lakini siasa za mama nikumaliza matatizo ya wanaoehindwa fanya kazi anazowatuma ndani kwa ndani Ww unasikia tu mtu amehamishwa/ondolewa madarakani
 
Hawa watawala sijui wanadanganywa na wasaidizi wao! wanaongea watu wasivyo taraji!, inaonekana wananchi wapo mbali kuliko viongozi. Wanaongea mambo mepesi mno wanaacha mamboya maana,ilimradi wameonekana runingani!
 
Sijapata kabisa kusikiliza hiyo Hotuba yake na mpaka sasa wala bado sijakifahamu hicho alichohutubia.

Isipokuwa napenda tu kusema kwamba kwa Watawala wa nchi za Afrika waliopo madarakani hivi Sasa, hakuna hata mmoja ambaye mwenye sifa au uwezo wa kutoa Hotuba yenye mvuto, Hotuba yenye ushawishi na/au Hotuba yenye hoja zenye akili kama ilivyokuwa huko miaka ya nyuma nyakati za Utawala wa Waasisi wa Mataifa yetu haya ya kiAfrika. Kwanza karibia Watawala wote kabisa waliopo madarakani hivi Sasa kwenye nchi zetu hizi za kiAfrika hawana mvuto wa kisiasa wala mvuto wa kidiplomasia si kwa Wananchi wao wenyewe wala siyo kwa Raia wa Kimataifa hapa duniani.

Zama za waAfrika kuwa na Watawala wa nchi wenye mvuto mkali wa kisiasa zimepita, itachukua miaka mingi Sana hapa Afrika kuwapata tena Watawala wenye Sifa hizo mfano wa Nelson Mandela, Mwl. J. K. Nyerere, Haile Selassie, Muammar Ghadafi, n.k.

Barani Afrika kwa Sasa tuna bahati mbaya, kwani Watawala wetu wengi zaidi hawana mvuto wa kisiasa na wala hawana ushawishi katika jamii zetu na hata kwa diplomasia ya Kimataifa
Mimi nilijua ataongea utumbo ndio maana sikutaka kufuatilia
 
Back
Top Bottom