HORSE POWER
JF-Expert Member
- Feb 22, 2015
- 2,328
- 1,666
Binafsi hata nikisikia anahutubia ni bora nikarudie 'series' ya Jumong maana simuelewi
Mimi nilipoona tu yuko live nikabadilosha chanelli haraka sana na wala sikutaka pressure kabisa sababu viongozi wa nchi hii hawana mpango na raia wake.Sisi tulidhani anatangaza kuachia ngazi tupumue hapo ndipo tulipopishana naye
Very trueMimi nilipoona tu yuko live nikabadilosha chanelli haraka sana na wala sikutaka pressure kabisa sababu viongozi wa nchi hii hawana mpango na raia wake.
Watu wanasinzia kwenye hotupa ujue hapo hamna kitu,Bora lyende!Sijapata kabisa kusikiliza hiyo Hotuba yake na mpaka sasa wala bado sijakifahamu hicho alichohutubia.
Isipokuwa napenda tu kusema kwamba kwa Watawala wa nchi za Afrika waliopo madarakani hivi Sasa, hakuna hata mmoja ambaye mwenye sifa au uwezo wa kutoa Hotuba yenye mvuto, Hotuba yenye ushawishi na/au Hotuba yenye hoja zenye akili kama ilivyokuwa huko miaka ya nyuma nyakati za Utawala wa Waasisi wa Mataifa yetu haya ya kiAfrika. Kwanza karibia Watawala wote kabisa waliopo madarakani hivi Sasa kwenye nchi zetu hizi za kiAfrika hawana mvuto wa kisiasa wala mvuto wa kidiplomasia si kwa Wananchi wao wenyewe wala siyo kwa Raia wa Kimataifa hapa duniani.
Zama za waAfrika kuwa na Watawala wa nchi wenye mvuto mkali wa kisiasa zimepita, itachukua miaka mingi Sana hapa Afrika kuwapata tena Watawala wenye Sifa hizo mfano wa Nelson Mandela, Mwl. J. K. Nyerere, Haile Selassie, Muammar Ghadafi, n.k.
Barani Afrika kwa Sasa tuna bahati mbaya, kwani Watawala wetu wengi zaidi hawana mvuto wa kisiasa na wala hawana ushawishi katika jamii zetu na hata kwa diplomasia ya Kimataifa
Acha kukariri wewe, watu kitambo wameshahamia Mikocheni wewe bado umenasa kwenye zile propaganda za CCM kuisema CHADEMA kuwa ipo ufipa.hotuba ya kumfurahisheni kila mwana ufipa
Anaogopa kushindwa vibaya uchaguzi mkuu👿Nuru imepotea,nadhani usingizi hapati vizuri...siasa bhana🙌
Ruto alisingiziwaunamkumbuka na ruto 🤣
Umesahau issue ya IPTL nadhani na habari za matibabu ya tezi dume?Anaacha mambo magumu yanayohitaji majibu anaongelea ishu za kutoa nishani. So what?
alisingiziwa nini mkuu? --- mimi namaanisha baada ya kuingia madarakani nahisi maandamano ya kwanza yale uso ulikua umedhoofika tofauti na wakati wa kampeni 🤣Ruto alisingiziwa
Ile habari ya ICcalisingiziwa nini mkuu? --- mimi namaanisha baada ya kuingia madarakani nahisi maandamano ya kwanza yale uso ulikua umedhoofika tofauti na wakati wa kampeni 🤣
sina kumbukumbu nayo mkuu --- ila nao chamoto hua wanakionaIle habari ya ICc
Hotuba ni zile zile, ignore baadhi ya mambo usiyaongelee, pretend kama hamna jambo. Endelea na mengineHotuba ya Rais Samia Suluhu Hassan ya 25 Aprili 2025 ilijaribu kuwasilisha ujumbe wa umoja na amani, lakini matukio ya kupigwa na kukamatwa kwa wanachama wa CHADEMA siku moja kabla, tarehe 24 Aprili 2025, wakati wa kesi ya Tundu Lissu, yanaonyesha tofauti kubwa kati ya kauli za Rais na vitendo vya mamlaka za serikali. Vurugu hizi zimeimarisha hisia za wananchi kwamba serikali inaendelea kuwakandamiza upinzani, na hotuba ya Rais haikuweza kushughulikia moja kwa moja mvutano huu wa kisiasa. Matukio haya yanaonyesha changamoto za kudumisha demokrasia na uhuru wa kisiasa nchini Tanzania, hasa kuelekea uchaguzi wa 2025.
25 Aprili 2025
JAMIIFORUMS NI JUKWAA KUBWA LA MEDIA, NAAMINI WATU WAMEITAFAKARI HOTUBA PIA TOFAUTI NA MEDIA ZINGINE TUNAWEZA KUIJADILI ILI KUJENGA TAIFA
Leo mheshimiwa rais wa Jamhuri ya Muungano, jioni tarehe 25 Aprili 2025 alitoa hotuba inayo semekana aliongea na taifa.
Je wewe kama mwananchi ulipata wasaa wa kuitazama au kuisikiliza ulikuwa na matarajio yapi hotuba hiyo ya mkuu wa nchi angegusia.
Uzi huu ni maalamu kwa ajili ya kutoa mrejesho, ili wananchi na viongozi wasitofautiane sana matarajio yao.
Na pia mrejesho wenu wananchi, unaweza kutoa dira kwa viongozi kuwa wananchi wana mambo gani wanadhani rais na wateule wake wangetekeleza na sababu zao ni zipi.
View attachment 3315718
Mheshimiwa Rais Samia Hassan alipokuwa anaongea na taifa.
N.B
Mrejesho wa raia kwa viongozi ni jambo jema. Hii ndiyo nafasi adimu ya kuzungumza na viongozi moja kwa moja baada ya hotuba, matamko n.k kutoka kwa viongozi walio ktk ofisi za umma.