Hotuba ya Rais Samia Suluhu kwenye Baraza la Umoja wa Mataifa (UN) - Septemba 23, 2021

Huyu mama hatorudi madarakani 2025, CCM wachague muungano au huyu mama.
Unajidanganya nafsi yako bure, huyu ndio Amiri jeshi mkuu na pia ndio mwenyekiti wa ccm.

Si vizuri kwa mtu mwenye akili timamu kujidanganya mwenyewe.

Ni ugonjwa au kifo tu ndio kinaweza kumuweka mama pembeni kutokuwa Rais mpaka 2030.
 
Mbona huyo chuma alikula hela za corona kwanini hakuzirudisha zilipotoka?
 
Bora mmewatafsiria kwa kiswahili ili Mataga waweze kuelewa kuwa mama kaenda kuwaombea misaada ya Chanjo ya Covid19.
 
JF, mimi huwa ni mkweli kabisa kabisa ...na maisha yangu yanasimamia kwenye ukweli...

Sitamsikiliza huyu maza kabisa sababu ntakwazika saana ...ntaumia sabababu najua mambo mengi yatakuwa fix fix.
Bora hujamsikiliza
 
Hakuna kitu unajua, kuhusu uchumi we ni taburarasa tu. Bora ukae kimya kulinda heshima yako jukwaani.
Kwani ni nchi gani ambayo haikuathirika uchumi Wake?hao hanaolilia ndio walipigika vibaya, wakati wao walikuwa wamejifungia Sisi huku tulikuwa tunachapa kazi, ndio wameanza kufufua uchumi wao eti anaomba msaada.

Marais wa Africa kuna mtu aliyewaloga Sio bure, unawezaje kuomba msaada wakati una lasmali lukuki,Madini, Mifugo,aridhi yenye rutuba,kila kitu wanacho lakini wanavyolialia kwa Wazungu utafikiri nchi zao ni majangwa, kumbe yanawaza ufisadi mtupu
 
Aliwahutubia akina nani. Unaweza kutuonyesha picha za waliokuwa wanasikiliza hotuba hiyo?
Isijekuwa alikuwa akihutubia mwenyekiti na watu aliokwenda nao kwenye msafara wake!
 
Mbona huyo chuma alikula hela za corona kwanini hakuzirudisha zilipotoka?
Kwani uliona anakwenda kupiga magoti kuziomba,yaani mtu ajipendekeze kuletea ela tena bila kuomba,alafu urudishe!utakuwa rofa,wao walijependekeza kwa chuma nae kawajengea watu Wake barabara
 
Kwani uliona anakwenda kupiga magoti kuziomba,yaani mtu ajipendekeze kuletea ela tena bila kuomba,alafu urudishe!utakuwa rofa,wao walijependekeza kwa chuma nae kawajengea watu Wake barabara
Una uhakika gani kwamba hakuomba?Au ulitaka akutangazie kuwa kaomba?
 
Kwani uliona anakwenda kupiga magoti kuziomba,yaani mtu ajipendekeze kuletea ela tena bila kuomba,alafu urudishe!utakuwa rofa,wao walijependekeza kwa chuma nae kawajengea watu Wake barabara
wewe kweli ni taburarasa.
huyo chuma si ndio aliomba afutiwe madeni kutokana na corona?

Sio yeye aliyekuwa anawapiga fiksi watu miradi inajengwa kwa fedha za ndani wakati kapanga foleni kwenda kukopa kwa hao 'mabeberu'
 
Kwani ni nchi gani ambayo haikuathirika uchumi Wake?hao hanaolilia ndio walipigika vibaya, wakati wao walikuwa wamejifungia Sisi huku tulikuwa tunachapa kazi, ndio wameanza kufufua uchumi wao eti anaomba msaada...
zaidi ya kutumia hisia, huna pointi.

toka kwenye hisia uje kwenye uhalisia.
 
Bora umeongea mkuu maana wazee wa mapambio ni mapovu tu yanawatoka, hana fluency yoyote wala misamiati ambayo inaweza kuaminisha watu kwamba ana master hiyo lugha.......
Katika kusoma tu, kuna makosa madogo madogo ya hapa na pale. Sehemu nyingine, ilikuwa plural lakini akasoma singular. Nina imani aliandikiwa vizuri ili kakosea kusoma.
 
Wabongo mna jazba na mtimanyongo na mama, itabidi mzoee ngoma mpaka 3035 hiyo imeishaaa. Wajanja tushalipia kadi za ccm miaka 10. Tunazama kwenye ccmapp tu sass hivi kupata fursa.
Umepewa chanjo milioni 1 mpaka sasa waliochanjwa hawafiki hata laki 3. Alafu unaenda #UNGA kuiambia dunia unataka chanjo nyingine! Seriously!
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]ata sijui nachekea nini lakini nimecheka tu
 
Katika hotuba yake huko USA amedai mpaka kufikia katikati ya mwaka 2022 watanzania %70 watakuwa wamechanjwa, hao watanzania ni akina nani wakati sasa hivi ndo uviko imepamba moto na watanzania hawataki kuchanja?

Juzi kati tu akiwa hapa kawe alihoji wananchi Kama watachanja wakamjibu waziwazi kuwa hawachanji yeye atatumia mbinu gani kuwashawishi wachanje?

Hau anaongelea kinyume na kuwazuga wazungu ili wampe mkopo mwingine! Kuna chanjo milioni moja zimeletwa na zimetumika %30 tu na watu hawana habari nazo tena je atatumia mbinu gani kuwashawishi wananchi angalau wazimalize? Hau anasubiri mda huo ufike apike takwimu ili apewe mkopo tena.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…