Miezi sita...????Wafanyabiashara wanaohitaji umeme, hasahasa hawa wa uwezo wa kati na chini..hiyo miezu sita hali itakuwaje???
Mama awe makini sana na hao wanaomletea hizo taarifa...wafrika sio watu wa kuwaamini hata kidogo...hawakawii kukudidimiza....
Kwa hiyo kipindi cha mwandazake ukame haukupiga na hizo maintenance zilikua hazifanyiki....???
Kweli mpaka miaka hii bado tunaongelea umeme wa maji kweli na wakati tumejifunz ukame unavyosumbua??
Tanzania ya viwanda utawezekana kweli kwa stahili hii??
Hivi serikali haijaona umuhimu wa kuhamia seriously kwenye vyanzo vingine mpaka tuongelee maji miaka yote??
Hivi kama mpaka karne hii tunashindwa kutatua suala la umeme 100% tutaweza kweli ku-assemble achilia mbali kutengeneza magari, nguo, pikipiki...Tunamipango ya exploration na uwekezaji kwenye teknologia mpya kwa ajili ya vizazi vyetu??
Hivi sisi, tunaweza kitu gani aisee....Nyerere alijitahidi kaanzisha viwanda..karibia vyote vimepotea...Mama awe makini yaani atashtuka hata hayo ma-turbines watu wameng'oa na kupeleka kusikojulikana...
Serikali na viongozi wetu wako bizy sana...Vikao vya kutosha, uteuzi mwingi, semina nje ya nchi, watu wanabadirishana tu, vitengo na vyeo ni vya kutosha lkn hakuna mabadiriko yenye uhakika....Mfano mara huyo Ndugu Maharage katolewa TANESCO, kaenda TTCL, then Posta..hivi tunatarajia mabadiliko yoyote kweli??Na watanzania walio wengi hata hawafuatilii hayo mambo ni kama wamesusa..
Daah..tutafika tumechoka sana...