Hotuba ya Rais Samia yalituliza Taifa na Kukata kiu ya Watanzania juu ya changamoto ya umeme

Hotuba ya Rais Samia yalituliza Taifa na Kukata kiu ya Watanzania juu ya changamoto ya umeme

Mama Abdu angekuwa mzalendo kama wewe angekuteua basi angalau uwe mkuu wa wilaya
Hapana mimi nafanya kazi kwa uzalendo na siyo kwa ajili ya kusaka uteuzi.sisi sote hatuwezi kuwa viongozi ,hivyo tusio viongozi tuna mchango kwa taifa letu.
 
Kwahiyo makali ya mgao wa umeme yanatulizwa kwa hotuba? Amesema nini kipya?
Makali ya umeme yanatulizwa kama alivyofanya Rais samia kwa kueleza kwanza chanzo cha Tatizo, muda wa kukabiliana na tatizo pamoja na Mikakati na mipango ya serikali kumaliza Tatizo. Ambapo Chanzo kimeelezwa,muda wa kukabiliana nayo imeelezwa pamoja na njia za kumaliza changamoto imewekwa wazi kabisa .
 
Alisema itachukua miaka mitano kazi ya kuweka sawa miundombinu ya umeme. Hilo umelisahau?

Sasa hii ya kusema miezi sita hii changamoto itakua imesahaulika ni ndani ya hiyo miaka mitano au Iko nje ya hicho kipindi?

Nawewe unakubali kwamba hizi changamoto za kukosekana umeme miaka yote ni kutokana na kutokua na maintenance kwenye miundo mbinu?

Kwa kumbukumbu zako ni lini kipindi Cha mwisho hiyo miundo mbinu ilifanyiwa maintenance?
 
Uwe na subira ndani ya muda mfupi changamoto hii inakwenda kuisha ,ndio maana hata sasa mgao siyo mkali sana kutokana na kazi inayoendelea kufanywa na serikali yetu katika kuhakikisha kuwa inatumia vyanzo vingine kuzalisha umeme,.Hivyo kufanya shughuli mbalimbali zinazotegemea umeme zisiathirike sana. Rais wetu ina tambua changamoto ya umeme ndio maana leo amelieleza ukweli Taifa na mikakati ya serikali yetu katika kulimaliza Tatizo hili.

Achana na haya mashairi mengi, unakumbuka ni katika kipindi chake tumeambiwa na aliyekua mkurugenzi wa hilo eneo kwamba hata bwawa kubwa linalojengwa likikamilika Bado hapatakua na unafuu tunaoutarajia?
 
Miezi sita...????Wafanyabiashara wanaohitaji umeme, hasahasa hawa wa uwezo wa kati na chini..hiyo miezu sita hali itakuwaje???
Mama awe makini sana na hao wanaomletea hizo taarifa...wafrika sio watu wa kuwaamini hata kidogo...hawakawii kukudidimiza....

Kwa hiyo kipindi cha mwandazake ukame haukupiga na hizo maintenance zilikua hazifanyiki....???

Kweli mpaka miaka hii bado tunaongelea umeme wa maji kweli na wakati tumejifunz ukame unavyosumbua??

Tanzania ya viwanda utawezekana kweli kwa stahili hii??

Hivi serikali haijaona umuhimu wa kuhamia seriously kwenye vyanzo vingine mpaka tuongelee maji miaka yote??

Hivi kama mpaka karne hii tunashindwa kutatua suala la umeme 100% tutaweza kweli ku-assemble achilia mbali kutengeneza magari, nguo, pikipiki...Tunamipango ya exploration na uwekezaji kwenye teknologia mpya kwa ajili ya vizazi vyetu??

Hivi sisi, tunaweza kitu gani aisee....Nyerere alijitahidi kaanzisha viwanda..karibia vyote vimepotea...Mama awe makini yaani atashtuka hata hayo ma-turbines watu wameng'oa na kupeleka kusikojulikana...

Serikali na viongozi wetu wako bizy sana...Vikao vya kutosha, uteuzi mwingi, semina nje ya nchi, watu wanabadirishana tu, vitengo na vyeo ni vya kutosha lkn hakuna mabadiriko yenye uhakika....Mfano mara huyo Ndugu Maharage katolewa TANESCO, kaenda TTCL, then Posta..hivi tunatarajia mabadiliko yoyote kweli??Na watanzania walio wengi hata hawafuatilii hayo mambo ni kama wamesusa..
Daah..tutafika tumechoka sana...
 
Sawa lakin UKWELI NI KUWA MWAKA NYANDA ZA JUU KUSIN HAKUKUWA NA UHABA WA MVUA NA VYANZO VIKUBWA VYA MTO RUAHA YAAN MTERA NA KIDATU VILIPATA MAJI UA KUTOSHA NDO MANA HATA MAZAO MWAKA HUU WAT WA KUSINI WAMEPATA SAAAN HIVYO

MNYONGE MNYONGENI HAK YAKE MPENI MAJI YALIMWAGWA KUSUD KUTENGENEZA MGAO HJU KWA AJIL YA DILI YA UMEME WA SOLAR NA GAS NA DIL ZENGINE WANAK ZIJUA WAO .
 
Back
Top Bottom