Humphrey Polepole: Rostam ni mfadhili mkuu wa wanamtandao, alipora 'Channel Ten', kauziwa kihuni mgodi wa Makaa ya Mawe na Serikali

Humphrey Polepole: Rostam ni mfadhili mkuu wa wanamtandao, alipora 'Channel Ten', kauziwa kihuni mgodi wa Makaa ya Mawe na Serikali

Kina tlaahtlaah na Lukas Mwashambwa na chiembe,Mtoto wa shule nk,Watajuta kwa uchawa wao,Hakibitasimama
Hata enzi za 2010/14 Kuna ID zilikuwa humu kuwasafisha Wanamtandao katika kuwatengenezea njia

Baada ya 2016 zikapotea na kuibuka nyingine

Kwasasa tunazo hizo lakini waliopo wakiondoka, wanakuja na id nyingine tena 🙌
 
Duh, mambo mengine Polepole anadanganya sasa, hapo ndio ninapogundua kuna vitu pia huyu Polepole hana taarifa sahihi.

Mgodi wa makaa ya mawe mahakama ndio iliyoamua baada ya kampuni ya Caspian kuwa wanamdai Tancoal kiasi kikubwa cha hela baada ya Tancoal kupewa huduma kwa muda mrefu na kushindwa kulipa deni, sio Caspian tu, Tancoal walikuwa wanamadeni mengi baada ya kupewa huduma na kushindwa kulipa madeni na makampuni tofautitofauti.

Caspian alikuwa anatoa huduma ya haulage pale na alipeleka mitambo yake kufanya kazi kwa muda mrefu, Tancoal akawa na financial crisis na kushindwa kulipa madeni.
Kesi ikaenda mahakamani deni likaonekana ni kubwa Tancoal hawezi kulipa ikabidi wakubaliane Tancoal amaliziwe hela ili abwage hisa zake.

Tuwe tunatafuta taarifa sahihi ya baadhi ya mambo pamoja na ugomvi wetu na CCM.
Yale yale ya uongo wa Lissu na kifo cha mlinzi wa JPM pale BBC au uongo wa Dr Slaa na bomba la gas lililopita baharini kwenda Dubai.

ndani ya mitaa ya Benghazi Libya.
Mahakama za ya nchi gani iliamua hiyo kesi?
 
Usiseme aliuziwa na Serikali, sema aliuziwa na wahuni wenzie!
Rosti tamu ni mtu wa kupenda kuhonga, fisadi na laghai miaka yote!
 
Kuna watu wanalipwa humu kwaajili ya hiyo kazi

Ndiyo muone ilivyo ngumu kufanyika mabadiriko kwenye hii Nchi
Ndio maana nilimuuliza mahakama ya nchi gani? Rostam ni msanii ndio maana utajiri wake haupo wazi, ila nitajiri kuliko hao tunawasikia kila siku Tanzania
 
Mahakama za ya nchi gani iliamua hiyo kesi?

Haijalishi ni mahakama ipi, maana ilikuwa ni kweli Tancoal anadaiwa na kweli Caspian alikuwa anafanya hizo kazi na alikuwa halipwi na mikataba Iko wazi.
Mhusika Tancoal hakuwa akidaiwa na Caspian tu alidaiwa na makampuni mengi yaliyokuwa yanatoa huduma na alikuwa hana uwezo wa kulipa, sasa hapo unataka rule out ya namna gani.
 
Eti haijalishi, mahakama zetu kama hauzijui sawa ila kama unazijua wazee wakusubiria call kutoka juu hamna cha maana kujadiliana hapa.
 
Ndio maana nilimuuliza mahakama ya nchi gani? Rostam ni msanii ndio maana utajiri wake haupo wazi, ila nitajiri kuliko hao tunawasikia kila siku Tanzania
Ndiyo maana anapambana Usiku na Mchana kuhakikisha Wanamtandao wanaendelea kusalia madarakani tangu 2005
 
Ndiyo maana anapambana Usiku na Mchana kuhakikisha Wanamtandao wanaendelea kusalia madarakani tangu 2005
Naam! Ni msanii nje ya system anakuwa si chochote utajiri wake unategemea sana serikali, kama serikali lege lege ndio anapiga aswaa.

Kama unakumbuka kipindi cha mwisho jpm alimrudisha kimkakati, kwanza alimkamata ndugu yake jangili wa meno ya tembo, lengo Rost alikuwa anashikilia mali za chama kama Chanel ten,magic fm, hisa pale voda na kadhalika
 
Wapo Mkuu, huoni watu wanachafuka na bado wanaenda kupewa madaraka pamoja na uchafu na madudu yao

Siku CCM ikiweza kutoka madarakani ndiyo Siku mabadiriko makubwa yatatokea kwenye hii Nchi

Lakini otherwise sio rahisi kuyaona na kupata hayo mabadiriko

Kwenye genge la wezi wakifanikiwa kuiba hawaachagi kupeanaadaraka, heshima ni kupewa madaraka na wananchi
 
Naam! Ni msanii nje ya system anakuwa si chochote utajiri wake unategemea sana serikali, kama serikali lege lege ndio anapiga aswaa
Ndiyo maana wakati wa JPM alipotea kwenye front page

Ila enzi za JK na sasa Mama, anatamba Kila Kona

Imefikia wakati hadi anasaini mikataba Kwa niaba ya Serikali 🙌

Kweli aliyetoroga kafa
 
Rostam angepiga kimya tu....kutafuta ligi na Polepole ni kujivua nguo tu..makandokando mengi.
Lkn Polepole naye, kama Rostam alitumia connection yake akanunua na akalipa kodi, no problem..sisi si tumelala..
 
Eti haijalishi, mahakama zetu kama hauzijui sawa ila kama unazijua wazee wakusubiria call kutoka juu hamna cha maana kujadiliana hapa.

Kuna vitu viwili, Kuna tukio na Kuna mahakama.

Umeua kweli, mahakama ikakuhukumu kukunyonga, hapo tutasema mahakama imepokea rushwa ili unyongwe? Ilihali umeua.

Sasa Tancoal anadaiwa na hana uwezo wa kulipa na wakakubaliane wajadiliane na mahakama na baada ya majadiliano wahusika wakakubaliana walivyokubaliana na mahakama ikatoa rule out, HAPO UNATAKA TUSEME SHIDA NI MAHAKAMA?...

Ndani ya mitaa ya Benghazi Libya.
 
Back
Top Bottom