Humphrey Polepole: Rostam ni mfadhili mkuu wa wanamtandao, alipora 'Channel Ten', kauziwa kihuni mgodi wa Makaa ya Mawe na Serikali

Humphrey Polepole: Rostam ni mfadhili mkuu wa wanamtandao, alipora 'Channel Ten', kauziwa kihuni mgodi wa Makaa ya Mawe na Serikali

Huyo Ponjoro kwani kama kashindikana kwa njia za kawaida si alogwe afie mbali
 
Inawezekana watanzania kweli tuna shida na CCM na watawala, lakini tuwe makini sana na baadhi ya watu maana naona kuna uongo na manipulations nyingi sana zinazoendelea.

HP, Sugu na Gwajima hawana uaminifu wowote wakuwasemea na kuwapigania watanzania, na haya ndio hufanya harakati zakuitoa CCM kila siku kurudi nyuma, maana tunaowaamini wajinga kila siku.

TL ni mzalendo wa kweli na kweli ana nia ya dhati, shida yake naye hayuko well informed kwenye mambo meeengi na ni mwepesi sana kuwa manipulated..
Kuishinda hii vita anahitajika mhuni anayeyajua mengi ya dark world.

ndani ya mitaa ya Benghazi Libya.
Kwahiyo tukuamini wewe tu?
 
Akili ya kawaida inaniambia Rostam hawezi kuwa anafaidika peke yake, bali kuna wanasiasa wako nyuma yake na ndio anashirikiana nao.
Rostam ana malori semitrailers, pulling, , long base, tipper 400 zinabeba makaa hayo ya mawe kutoka huko kusini masaa 24 gari ziko barabarani route kusini, manyoni, Tabora mjini, Nzega via kahama ,Mpaka Uganda ana mpango wa kuongeza malori mengine abebe makaa ya mawe mpaka ayamalize , nyuma yake Kuna wastaafu wakubwa , hii ndio itakuwa imempa kesi Lissu .
 
Kwahiyo tukuamini wewe tu?

Usiniamini mimi, fuatilia fact.
Binafsi najua fact nyingi sio hear say za watu, nikiona mtu anasema uongo inanipa shida kidogo.

amini katika hili la Tancoal, HP kadanganya na aamini pia HP hayajui mengi hana ukweli wa mengi, nimemsikiliza toka day 1 kwenye hizo episodes zake, nimegundua hajui mengi na hana power.

ndani ya mitaa ya Benghazi Libya.
 
Huyu jamaa angeachana na hizi sarakasi tu, hakuna faida yoyote ataipata, anajihatarishia maisha yake bure tu. Angepambana na maisha yake
Huna akili nyamaza.keep your cowardice to yourself
 
Ni kweli siyo rahisi.Lakini tayari anaowakosoa tayari amewaathiri kisaikolojia kupita kiasi.Pia uoga uliokuwa umetamalaki umepungua sana.
Tangu nione anayopitia Mhe. Lissu kwenye hili Taifa ndiyo nikajua na nina hakika hii Nchi imeshikwa na wachache wenye hela

Na ukiwa msomaji wa vitabu ama nyuzi za kitambo humu utakuwa umejua ni Kwa kiasi gani hao Wana mtandao wamefanikiwa kuwaondoa wakosoaji wao wote ukianzia na Mwaka 99 hadi sasa

Hao watu Wana mizizi mikubwa sana hii Nchi

Na bahati mbaya, wamefanikiwa kutugawa Watanzania ambapo ingekuwa Nchi nyingine, yangekuwa yanafanyika maandamano makubwa ya kupinga yanayo endelea

Badala yake, tumebaki kusema kwani jambo lililofanyika, si amefanyiwa fulani sio Mimi
 
Vyomb vya ulinzi na usalama vijitafakari kama kweli vinaistahili hii nchi, haiwezekani mtu mmoja tena sio indigenous ashikilie uchumi wa nchi kwa kuhodhi biashara zote za maliasili yetu kuanzia gesi, chuma ,makaa ya mawe na dhahabu. How comes vyombo vimeacha hili jambo kuendelea miaka yote hii? Yaani mtu mmoja kashikilia sekta yoye ya energy na wako kimya tu?!! Hawaoni hatari ya kuingiza nchi kwenye resources curse kama ya DRC na Nigeria?
 
Watu wapenda haki mapinduzi ya fikra wakikusikiliza wewe Nchi itaoza Asubuhi mapema kwani hutaki watu wakatae maovu wizi kisa utawabambikia kesi za uhaini kwa njia za kishetani
Nafahamu kiu uliyonayo Mkuu juu ya mabadiriko ya hii Nchi kuelekea ustawi na mustakabali Mkubwa wa kesho ya Taifa letu

Lakini bahati mbaya hao watu wameshafanikiwa kuligawa Taifa

Imefikia kipindi anayeonekana kinara wa kupinga udhalimu anafanyiwa matendo ya kishetani na Tanzania nzima inashuhudia pasipo kufanyika jambo lolote

Hebu angalia tukio la Lissu

Kisha angalia tukio la Mzee Kibao

Nenda pale Mbeya angalia tukio la Mdude

Haya matukio, ingekuwa Nchi zingine yalitosha kuwawajibisha waliopo madarakani

Kwakuwa wamefanikiwa kutugawa, hatuoni likitugusa kwakuwa aliyefanyiwa yale sio Mtanzania mwenzetu
 
Kwahiyo akae kimya?alaf kabisa mtoto wa kiume unaandika umejikatia tamaa..kweli we have a long way to go...
Simaanishi akae kimya, hoja yangu ni nilitamani Watanzania wote wangekuwa na umoja wa kukemea yanayoendelea

Kwakuwa hao Wanamtandao wamefanikiwa kutugawa Watanzania, sioni vita hii akivishinda huyo HPolepole akiwa peke yake hivi

Nilitolea mfano, angalia madhira anayopitia Lissu lakini hapo hapo Watanzania wametulia tu ili hali wangekuwa na umoja wangeandamana hadi ku-push agenda ya mabadiriko wayatakayo

Angalia visa vilivyowapata akina Mzee Kibao na Mdude

Lakini hakuna reaction ya Watanzania kwenye yale matukio

Angalia kisa cha Padri Kitima, lakini hata makanisa yameshindwa kuwaunga Mkono wenzao

Point yangu ni kwamba, hata HPolepole aandike na kusema nini hakuna kitu kitaenda kubadirika kama Watanzania wenyewe wataendelea kukubali kugawanywa Kwa namna hii

Kama hadi ndani ya CDM yenyewe ilikuwa na wanufaika wa Wanamtandao, unadhani hili kundi ni la mchezo

Magu mwenyewe pamoja na kuwa na vikosi vyote vya jeshi lakini amelazwa Chini na hili kundi

Anyways, ngoja tusubiri hiyo press yake ya Leo kama itaweza kuwaamsha Watanzania kwenye huu Usingizi wa Pono waliolala
 
Polepole muongo, rostam alianza kununua magazeti ya jenerali ulimwengu 'rai' akaja malizia channel ten,kisha CCM wakainunua channel ten, ulimwengu alianzisha raia mwema
Ulimwengu walimpora tu magazeti yake baada ya partner wake Salva Rweyimamu ku-join na wahuni ambao Jenerali alishatofautiana nao baada kuwa anaibua kashfa kadha wa kadha kuhusu wahuni (wanamtandao). However, you're right, Channel ten ilikuwa ya Francesco Tramontano under African Media Group, haikuwa ya ccm.
 
Hakuna yeyote alielipwa ni upumbavu tu watanzania.. kutetea wahuni wakihisi nao watanufauka sijui watanufauka kinamna gani..
Siku Watanzania watakachoka labda wataweza kuungana na kuwa kitu kimoja kwenye mambo ya kitaifa

Lakini Kwa mgawanyo huu tulionao, sioni kama tutapiga hatua manake hao watu wameweza kujizatiti Kwa muda mrefu kwenye hii Nchi

Mbaya zaidi ndiyo wameanza harakati za kuendelea kutawala hata baada ya wao kuondoka Kwa Uzee miaka 20 ama 15 ijayo 🙌
 
Umeniku
Rostam alinunua "Habari Corparation" kukufisha media hii kuichallenge serikati ya kikwete kuibua ufisadi,baada ya hapo waandishi nguli km Joseph Mihangwa,Johnson Mbwambo na Ulimwengu mwenyewe wakagoma kuandika habari kwa maelekezo ya Rostam... hii ndio sababu ya kuanzia Raia Mwema..
Umenikumbusha mbali
 
Tusipo.msikiliza na kumwelewa Polepole. Tumeisha kabisa. Na aliyeko gerezani ndio atanyongwa kabisa. Nchi Haina mwenyewe. Ni kujipakulia tu na kuwaua wote wanaokosoa. Hatutapata mtu.mwingine wa aina ya Polepole.
 
Kwa hiyo kwa sababu hawezi kushinda vita inatakiwa akae kimya sio daah..
Angalia sauti ya hayo anayoongea Polepole zinawafikia kundi gani? Ni hawa wenye access ya YouTube/TikTok n.k.

Lissu yeye alikuwa anaenda Kijiji Kwa Kijiji, ambapo nina amini sauti ya ngurumo zake zilikuwa zinawafikia hadi Mama zetu kule Kijijini

Lakini amefanyiwa yale aliyofanyiwa na hakuna kitu tumefanya walau kama Nchi kumpigania

Unajua chanzo ni nini Mkubwa? Tumekubali kugawanywa kama Taifa

Na kete kubwa wanayoitumia miaka yote hao watawala ni kusema Tuilinde Amani, Kuna watu wametumwa na mabeberu kuja kutuharibia Amani

Basi Watanzania wanaingia na hofu na kukubali kuingia Kwenye huo mtego

The rest, hao wachache wenye kupaza sauti wanaishia kuteseka na wengine kuuawa kama ilivyotokea Mdude na Padri Kitima
 
Hii vita inapiganwa na MUNGU kwa niaba ya WaTanganyika! Usiogope!
Na iwe hivyo Mkuu

Wengine tumeshakula chumvi, tungetamani kabla hatujaondoka kwenye hii Dunia tuwe tumeshuhudia ustawi wa watoto na Wajukuu zetu kupitia mabadiriko tunayotamani kuyaona
 
Hakuna aliyesafishika
Wapo Mkuu, huoni watu wanachafuka na bado wanaenda kupewa madaraka pamoja na uchafu na madudu yao

Siku CCM ikiweza kutoka madarakani ndiyo Siku mabadiriko makubwa yatatokea kwenye hii Nchi

Lakini otherwise sio rahisi kuyaona na kupata hayo mabadiriko
 
Back
Top Bottom