Humphrey Polepole: Sihami CCM labda Wanitupe nje!, Nimeitwa TCRA nijieleze. Hoja haipigwi rungu bali inajibiwa

Humphrey Polepole: Sihami CCM labda Wanitupe nje!, Nimeitwa TCRA nijieleze. Hoja haipigwi rungu bali inajibiwa

Hivi na wewe unaamini anachokifanya huyu Jamaa. Hivi uliamini kuhusu Membe na ACT, Hivi uliamini kuhusu Nyalandu. Kinachotengenezwa hapo ni kuonekane kuna mgogoro kati yake na chama halafu baadae atoke mumpokee huko kama shujaa. 2025 sio mbali.
Sasa nani akipokee kingedere hicho!
 
Hi guys. Hope mnado poa.

Kuna page imeandika kuwa bwana Polepole atajitoa chamani wakishirikina na taasisi 2.

Hii ni nyepesi nyepesi.

At Calvary.

====

Taarifa kwa Vyombo vya Habari.
Jumamosi tarehe 11, Disemba 2021 saa 5:00 Asubuhi nitazungumza na Wanahabari pamoja na Mambo mengine nitazungumzia Shule ya Uongozi | The Leadership School. Mahali - Ofisi za Kituo cha Msaada wa Kisheria na Haki za Binadamu (LHRC).
-Ujamaa ni Imani-
View attachment 2039936View attachment 2039938

=====

UPDATES;

======

"Kama viongozi wasiposali na kumtemea Mungu nchi yetu haiwezi kuendelea, tumtangulize Mungu mbele. Kuanzia diwani, mpaka mawaziri na kule juu tuwe watu wa maombi, kukumbushana ni muhimu, naona kama tunatakiwa tuishi maisha ya Kimungu hivi." - Humphrey Polepole

"Viongozi wanatakiwa wawe waadilifu na wanyenyekevu." - Humphrey Polepole.

"Nilisema kuhusu magonjwa, mfano ebola, kesi moja tu imewahi kupenya na ikafuatiliwa na sasa tuko salama. Yakaja haya magonjwa mengine maarufu hivi karibuni lakini sio kitu. Nikasema muwe makini hawa wahuni wa kimataifa ni wajanja." - Humphrey Polepole.

"Nilizungumza kuhusu songombingo la wamachinga, Mhe. Rais Samia Suluhu alitoa maelekezo mazuri sana lakini wapo waliotekeleza vizuri wengine wamefanya vibaya mno, wameboronga, ukimkosoa DC au RC kuhusu hili wanasema umemkosoa Rais, nani kakwambia?" - Humphrey Polepole.

"Rais Samia Suluhu alitoa maelekezo mazuri sana kuhusu wamachinga, wapangeni vizuri, msiwazonge, msiwapige, msiwanyanyase.... mimi ni mwana-CCM bana, fitina kwangu ni mwiko. Nikasema mlivyotenda kwa machinga baadhi yenu mmekosea na nikatoa mifano." - Humphrey Polepole.

"Kwenye mgongano wa kimasilahi kuna aina tatu, masilahi ya Taifa, kundi au mtu mmoja mmoja, wanaanza na masilani ya mtu mmoja, kisha kundi na baadaye Taifa, nikasema wanaopanga hivi ni wahuni." - Humphrey Polepole.

"Wahuni wanapenda masilahi binafsi kwanza, kazi yetu ni kuwadhibiti bila huruma wala kucheka nao. Yanatokea majitu tena viongozi na kusema mimi ni muhuni nimepenya, unaweza kutafakari namna gani kiongozi huyu yuko serious, huwezi kuwa kiongozi ukachekelea kuwa mhuni." -Polepole.

"Kule bungeni tunakutana mara chache, mfano kuna kipindi cha mwezi Machi hadi Julai, ina maana mimi niongee mara nne tu kwa mwaka kuhusu wahuni, unadhani inatosha, nitatumia fursa zozote za kusema ili kuwasema wahuni," - @hpolepole, Mbunge wa kuteuliwa.

"Kwa sasa nimeshaanza kufuatilia mambo kadhaa, watu wakizingua pahala ninatoka ninasema hapa umezingua nitaruka na wewe, nakulipua, si wanachelewa kuchukua hatua? - Humphrey Polepole.

"Sijasema Serikali haifanyi kazi, Serikali inafanya kazi nzuri sana lakini ni jukumu letu na kukumbushana. Unadhani kwa nini malaria haiishi na tumesoma mpaka madarasa tukayamaliza? Halafu tunasema tu lete net, hivyo viwanda wanatengeneza wapi?, vya msaada. - Humphrey Polepole.

"Nilieleza kuhusu uchambuzi wa matatizo, malaria haiishi Tanzania kwa sababu hatuchambui tatizo, unadhani ufumbuzi ni chandarua kwani ukitoka usiku kwenda haja ndogo mbu si wanaunga na wewe? tunafanya maamuzi ambayo hayajajengwa katika kutatua tatizo, hilo nalo tatizo." -Polepole

"Kuna kiwanda kipo hapa nchini kinatengeneza viuatilifu vya kuua mazalia ya mbu, nyie wanahabari waulizeni wamewahi kunnuua pale? Mtu analala kwenye chandarua mguu upo nje, mbu wanamng'ata, nauliza sisi tumekwenda shule tukasoma, hii ndio suluhisho kweli?" - Humphrey Polepole.

"Nilizungumza kuhusu deni la taifa, kuna watu wengine ni wabunge wakaibuka wanasema ooh deni limekuuwa kubwa, zito linamuelea mama. Nikatoka nikasema ukweli wasipotoshe, ni uongo. Si viongozi wote tupo kwa nini mwenzetu anapotosha na hatutoki kusema? kimya. -Humprhey Polepole.

"Sijui kwa nini viongozi wanaogopa kusema, sijui wanaogopa, kwa sababu deni linalosemwa viongozi wote walikuwepo, niweke sawa watu wasielewe tofauti. Kwa nini wenzetu msitoke mkasema, au mpaka watu wachanganyikiwe, penye ukweli lazima tuseme ukweli? - Humphrey Polepole.

"Juzi Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo ndiye amekuwa mtu wa kwanza kutoka na kusema deni la Taifa ni himilivu, na yeye amejiongeza tu baada ya kuona kimya." - Humphrey Polepole.

"Sijazungumzia mtu, mbunge, mamlaka ya nchi wala mjomba wake mtu lakini baadhi ya viongozi wamechukia, kwa nini unaongea? Hivi imefika pahala tunaulizana kwa nini umeongea, Mungu amenipa mdomo unataka nifanye nini? Kuna kula na kuongea. - Humphrey Polepole.

"Nilipofanya Shule ya Uongozi nikapigiwa simu na watu wanaambiwa acha kwanza, nikauliza kwa nini? hakuna majibu. Nimefanya kazi na Mzee Mkapa, Kikwete, Magufuli na Mama Samia, hawa viongozi wangu wote hawajawahi kuniambia 'kaa kimya', nawashangaa wanaotaka ninyamaze." - Polepole.

"Mwalimu Nyerere alisema 'hoja ahipigwi rungu, inajibiwa kwa hoja bora zaidi', mimi ni mwana-CCM ninawaambia hapa kuna tatizo linarekebishika hivi, unasema kaa kimya, hilo ni jibu la hoja nilililoitoa." - Humphrey Polepole.

"Niliitwa kwenye chama kwa tuhuma, nilizijibu zote moja baada ya nyingine, siwezi kusema, chama kitakuja kuzungumza." - Humphrey Polepole.

"Nimeitwa TCRA, wanasema nimetoa maudhui ya kupotosha umma yanayoweza kuchochea Watanzania kugomea na kudhoofisha kampeni ya Kitaifa kujikinga na Corona. Hivi mimi nimeshawahi kuwaambia tudhoofishe kampeni ya kujikinga na corona? hawa wanataka kunichomeka hapa" -Humphrey Polepole

"Sijawahi kusema kwa nini sichanji, sasa tusisukumane nikafafanua kwa nini sikutaka kuchanja. Sasa nitakwenda TCRA kupeleka utetezi wangu nikaseme ukweli maana tunatafutana kwenye korido la corona." - Humphrey Polepole.

"Hii hoja ya wamachinga nasema kweli mmeonea watu, halafu mtu anasema kaa kimya, kumbe jukumu la mbunge ni nini? Sauti ya watu ni ipi? Hii kaa kimya nimehangaika nayo sana, nimefanya tu kiubishi." - Humphrey Polepole.

"TCRA wanasema wamenipa leseni kwa ajili ya maudhui ya kipindi cha Papo kwa Hapo, wanahoji kwa nini ninafanya Shule ya Uongozi... hivi mimi nimekulipa milioni ile halafu unanipangia cha kuzungumza? naweza kuposti familia yangu au mbwa wangu, utaniuliza?" - Humphrey Polepole.

"Kuhusu corona kuna ubishi wa kidunia, kila mtu ana upande wake, na mimi niweke wazi nipo kwenye ubishi huo. Mpaka Yesu atarudi tunaendelea na ubishi," Humphrey Polepole.

"Suala la machinga wanasema nimesema uongo, tena kwenye hilo nitasema na mengine ambayo sikutaka kusema, nina ushahidi, nimepeleka watafiti wilaya zote za Dar es Salaam, mtu amehamishwa na kupelekwa kwenye karo la choo, hivi Mhe. Rais aliwatuma hivyo?" - Humphrey Polepole.

"Kuna watu wanasema Polpole anajitoa CCM anakwenda kuanzisha chama chake, nataka niwaambie niliingia CCm kwa hiari mwaka 2000 nikapiga kura kwa mara ya kwanza, sitatoka CCM kwa hiari. Kama ninatoka CCM washike wanitupe nje, bado tupo sana hapa." - Polepole.


Mbunge wa Kuteuliwa (CCM),Humphrey Polepole amesema amepokea Mashtaka ya TCRA yanayosema kupitia Kipindi chake cha Shule ya Uongozi, amerusha Maudhui yanayopotosha Umma na yanayoweza kuchochea Watanzania kuweza kugomea Kampeni ya Kitaifa ya #COVID19

Akizungumza leo amesema, "Hivi mimi nimewahi kuwaambia ninyi tudhoofishe Kampeni ya Corona? Wapi niliwaambia kwa maana hiyo?"

Amesema kwasababu amepewa nafasi ya kujibu, atapelekea Utetezi wake aliodai unajitosheleza

#JamiiForums #UVIKO3

We kiroboto kaa KWA kutulia nyie mliua watu, militia watu vilema, mlifunga watu, mlipora uchaguzi leo unataka kutuambia nini we kiroboto
 
CHAGGA DEVELOPMENT MANIFESTO

Mnachekesha sana,asubuhi mliamka na thread za kuuaminisha umma humu mitandaoni kwamba Polepole anakwenda kutangaza kujivua uanachama.

Baada ya kuumbuka na uongo wenu, sasa mnatunga uongo mwingine mwiingi.

Polepole hana njaa na amekwisha weka wazi kwamba 2025 hataki ubunge

Yule sio kilaza.elimu yake sio kama ya Dj au Sugu na wengine wengi waliochutama kwa sasa huko vijiweni
We jinga kwelikweli karne hii unamtambia nani juu ya elimu,elimu tanzania?kuna watu wana elimu kubwa kuliko huyo kiroboto wako na wapowapo tu kitaa,ashukuru tu huo upepo wa chama chakavu mafi ww
 
Sasa ni zamu ya polepole [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Fitna mbaya sana, hili genge la wahuni litakuja pasuka vipande vipande yani kila mtu atakaposikia masikio yake yatawasha.
 
"TCRA wanasema wamenipa leseni kwa ajili ya maudhui ya kipindi cha Papo kwa Hapo, wanahoji kwa nini ninafanya Shule ya Uongozi... hivi mimi nimekulipa milioni ile halafu unanipangia cha kuzungumza? naweza kuposti familia yangu au mbwa wangu, utaniuliza?" - Humphrey Polepole.

.…............
Chidi Benzi aliwahi kuwaasa viongozi kuwa waboreshe magereza maana hawajui kesho watakuwa wapi.
 
Polepole anawashwa sana,,,, watampoteza taratibu.

Au labda ni mkakati ili waje walete chama kingine
 
Huyo mbwa koko wakati wao alijiona kama dunia yote ni mali yao lakini toka alipofiwa na bwana ake amevurugwa.
 
Mbona enzi zake akiwa na nguvu wenzake wakizungumza wanatekwa au kuuliwa kabisa? Kwa hiyo na yeye atekwe siyo au auliwe kabisa?!!!
Vijana wa ccm tukiwaambia tujenge chi kwanza chama baadaye hamtaki, mnadanganywa eti chama kwanza nchi baadaye...ipo siku ya kila mmoja wenu itafika tu, mnakitukuza chama na kuidharau NCHI!!!!!
Nimekuwa specific kwa ZZK, mara ngapi kazungumza hadharani na kukosoa uongozi wa awamu ya 5 na hakuwahi kutekwa au kuuwawa?

Na tukibaki kwenye muktadha wa Humphrey kukosoa mambo yasiyo sawa, kosa lake liko wapi?

Julius Nyerere alimkosoa mzee Ruksa mara kwa mara baada ya kustaafu. Nape akiwa katibu wa Itikadi na Unenezi amekuwa akisisitiza kuwa CCM kwa culture yao, kujikosoa ndio msingi na nguvu yao ndani ya CCM.

Awamu ya nne kulikuwa na kukosoana sana kati ya Spika Sitta dhidi ya watendaji wa serikali na chama. Na ikafikia wakati mmoja Spika Sitta akawa hapikiki chungu kimoja na Katibu Mkuu CCM- Mzee Makamba.

Humphrey bado hajafikia hata robo ya mtifuano wa hoja kati ya akina Sitta na ile kambi ya wapigaji enzi hizo, mpaka ikifikia Rostam kuachana na Ubunge na kujizuru kwa mfumo kama huu huu wa kukosoana. Labda umesahau hili na tukumbushane.
 
Mheshiwa Polepole ni sauti muhimu sana ya umma. Anawakilisha wengi. Nyie TCRA hamna kazi, kwanza watu kawa hawa wenye mawazo mbadala ya kushauri, kurekebisha, kukumbusha inabidi muwalinde.

Demokrasia ni nini? kuwasikiliza wengi, mawazo yao, maoni yao, kero zao, wanateseka na nini?

Uraia ni nini? A citizen is a participatory member of a political community.
Raia ana haki anatakiwa atoe maoni kwa staha ya kujenga nchi yake. ni jukumu lake, jukumu la raia wote wa nchi yoyote duniani.

Serikali ni nini? Watu wachache wamepewa dhamana, nafasi kuwaongoza Wananchi wote.
Inamaanisha kuwasikiliza, kutatua kero, shida zao, kuweka mazingira sahihi ya biashara, kodi, kilimo, exports, miundombinu yote ( Afya, shule, hospitali, barabara) ustawi wa nchi.

TCRA mnataka kila mtu akubali huu uhuni, maji, umeme, ajira hakuna, mfumuko wa bei, vifurushi, wote inabidi tucheke huku tunakufa taratibu. Mnakosea, hamjui majukumu yenu.
Ana mtaji wa watu, akianzisha chama wasanii wote maarufu na wasio maarufu kumfuata, Yanga yote kumfuata, Wasukuma wote 16% ya watu wote wa nchi kumfuata, vyama vidogovidogo kumfuata, kitabaki nini hapo?
 
Atajibiwa na CCM wenzie, Sisi tupo humu kumpaka Kama yeye alivyotusaliti na kuhamia huko kwenye karamu kisha kuanza kuturingishia viete....Kwa ufupi tunafurahia shida zake.
Posho na mshahara wa ubunge na kiinua mgongo cha baada ya miaka 5 kweli huyu mtu ana shida? Au sijaelewa ulitaka kusema shida aina gani. Ongeza na pesa walizopiga kwenye awamu ya tano!
 
Hukohuko ccm ndio aliondoka Lyatonga, akaondoka Maalim Seif, akaondoka Lowasa, Sumaye, akaondoka membe.....

Na kazi ikaendelea
EeeenHeeee!
Hivi hao waliondoka, au walichukua 'franchise' ya CCM na kuisambazanchi nzima.

Huoni wanaokataa kuwa kitawi cha CCM wanavyohangaishwa?
 
Posho na mshahara wa ubunge na kiinua mgongo cha baada ya miaka 5 kweli huyu mtu ana shida? Au sijaelewa ulitaka kusema shida aina gani. Ongeza na pesa walizopiga kwenye awamu ya tano!
Wee unaujua utamu wa cheo wewe? Kila unapopita watu wanakupapatikia, ubunge gani mbunge Hana hata Jimbo? Jimbo lake ni press conference kweli?😂😂😂
Halafu pesa pekee haitoshi Kwa mtu aliyekuwa na madaraka makubwa ya kuwatetemesha Hadi mawaziri.
 
Ujumbe nzuri siku zote huwa Nipo pamoja na watu wenye msimamo sichanjwa

Hawa TCRA wanatatizo gani kutaka kulazimisha kampeni za Chanjo.
 
Mheshiwa Polepole ni sauti muhimu sana ya umma. Anawakilisha wengi. Nyie TCRA hamna kazi, kwanza watu kawa hawa wenye mawazo mbadala ya kushauri, kurekebisha, kukumbusha inabidi muwalinde.

Demokrasia ni nini? kuwasikiliza wengi, mawazo yao, maoni yao, kero zao, wanateseka na nini?

Uraia ni nini? A citizen is a participatory member of a political community.
Raia ana haki anatakiwa atoe maoni kwa staha ya kujenga nchi yake. ni jukumu lake, jukumu la raia wote wa nchi yoyote duniani.

Serikali ni nini? Watu wachache wamepewa dhamana, nafasi kuwaongoza Wananchi wote.
Inamaanisha kuwasikiliza, kutatua kero, shida zao, kuweka mazingira sahihi ya biashara, kodi, kilimo, exports, miundombinu yote ( Afya, shule, hospitali, barabara) ustawi wa nchi.

TCRA mnataka kila mtu akubali huu uhuni, maji, umeme, ajira hakuna, mfumuko wa bei, vifurushi, wote inabidi tucheke huku tunakufa taratibu. Mnakosea, hamjui majukumu yenu.
Ila suala la Covid ni suala la majabali ya dunia, anatakiwa akokotoe hesabu zake vizuri vinginevyo watamshughulikia wenyewe kwa mbinu zao wazijuazo ikiwemo kupigwa marufuku kwenda nchi za majabali given kwamba hata yeye hajachanja.

Yeye saizi yake ni watu wa ndani ya nchi, kule nje siyo saizi yake. Watu wametoa ela zao zikatujengea shule na vituo vya afya nchi nzima ili wafanye biashara ya chanjo, barakoa na kits alafu utie mchanga kitumbua chao?? weweee..!! Jipange....

Tozo za miamala kwa ajili ya kujengea shule, vituo vya afya na maji zilikuwa zimetufarakanisha na serikali, wao wakatoa fungu kufanya kazi hizo alafu uwe na msimamo tofauti na wao....
 
Mbona akina ZZK wamekuwa na youtube talks, kuna akina Maria wana space talks, kuna akina Jenerali wanazindua vitabu na kujiachia kuzungumza.

Kwanini Polepole kuzungumza na media LHRC inaonekana nongwa? Nadhani maadamu hajavunja sheria na msingi wa uongozi ni kukosoana kwa misingi ya kujenga hoja pasi kutwezana, bila shaka Humphrey ana ujumbe wa kutufikirisha.
Mkuu 'Freddie Matoja', sina hoja kinzani juu ya hao akina Zitto na wengine kuruhusiwa kufanya wanayofanya; ila nielewavyo mimi, Popole ni tofauti sana na hao wengine.
Kumbuka CCM wanavyojinadi kuwa na njia zao za kumaliza mambo ndani ya chama chao bila ya kuyapeleka nje ya chama. Popole bila shaka wanataka akazungumzie ndani ya chama ili waweze kummaliza kimya kimya huko huko.
 
Back
Top Bottom