Huu haukuwa muda muafaka wa Rais Samia kutembelea Marekani: Amejiweka kwenye Shinikizo la kulazimishwa kuilaani Urusi

Nchi haijengwi kwa kutegemea misaada!! Ambayo kuema ukweli si misaada Bali ni mitego!! Mwisho wa siku tunapoteza badala ya kupata!
Kwa Sasa Marekani hawezi kukupa kitu bila kumfurahisha kwa kuilaani Urusi!!
Nakubaliana na wewe. Miaka 5 iliyopita, Serikali ilifanya mambo mengi ya maendeleo, kwa fedha za ndani au mikopo, na si ombaomba ya sasa na Awamu zingine
 
Samia anadanganya tu, how on earth anaenda matekani sasa, there is almost vita ya 3 ya dunia. Thanzania is facing very high inflation, yeye aenda matekani kula bata. This was really a very poor choice, kwenda shopping!
Na Vita ya Tatu ni ya Uchumi
 
Kama unapata riziki zako inatosha.mengine waachie wenyewe

Ila inauma Sana!! Nina hasira na wasaidizi wa Rais, kwa nini waruhusu safari kipindi hiki Cha mashinikizo ya wazi? Kuna asiyeijua Marekani inachotaka kwa Sasa!! Unaamua kwenda kukutana na Simba mwenye njaa unatarajia nini?
 
barua ya ikulu haikutaarifu kuhusu officer yeyote wa kimarekani kumpokea zaidi ya kuhamasisha wana diaspora wajitokeze kwa wingi.

so in short unaweza sema mama kajialika.

Au anaenda kuwatembelea watanzania walioko Marekani? Hayo ni matumizi sahihi ya Kodi yetu? Ngoja tuone! Huyu ni Rais wetu, aibu yake ni aibu yetu, fedheha yake ni fedheha yetu! Walioratibu safari hiyo wawajibike!
 
Wasaidizi wa Rais Samia Suluhu Hassan wametenda kosa kubwa sana kwa kutokumshauri Rais kuwa huu haukuwa muda muafaka wa yeye kutembelea Marekani.

Marekani Ina hasira na Nchi nyingi duniani kwa kutokuiunga mkono katika harakati zake za kuitenga Urusi katika jamii ya kimataifa. Tanzania tumeamua kuwa neutral/kutokuwa na upande katika mzozo wa Urusi na Ukraine.

Kwa Marekani ukiamua kutokuwa na upande unahesabika kuwa uko upande wa Urusi, na inafanya Kila jitihada kuyatisha mataifa yenye msimamo huo Ili yailaani Urusi! Kwa hiyo ukiandaa mazingira ya kukutana na Marekani kwa Sasa lazima ikushinikize kuilaani Urusi.

Sidhani Kama mama atakuwa na ubavu wa kuhimili shinikizo la Marekani katika jambo hili. Anaweza kujikuta amesema jambo ambalo hakutegemea akiwa chini ya shinikizo. Sidhani kama ataweza kuhimili Kama India na Afrika ya kusini zilivyoweza kuhimili.

Afrika hatuwezi kulaani Nchi ya Urusi iliyokuwa mstari wa mbele Sana kwenye harakati za upatikanaji wa uhuru kusini mwa afrika-(Zimbambwe, Msumbiji, Botswana, Angola, Namibia na Afrika ya kusini).

Wakati huo wapigania uhuru akiwemo Mandera walikuwa wanaitwa magaidi na Marekani!! Chonde chonde Samia Mungu akutie nguvu uwatolee nje mabeberu huko Marekani!
Wenzetu wako Busy kuiuza Gesi yetu ili wawe na uhakika wa kula Pensheni vizuri uzeeni.

Sidhani kama January amekosekana kwenye hiyo ziara.
 
Wasaidizi wa Rais Samia Suluhu Hassan wametenda kosa kubwa sana kwa kutokumshauri Rais kuwa huu haukuwa muda muafaka wa yeye kutembelea Marekani.

Marekani Ina hasira na Nchi nyingi duniani kwa kutokuiunga mkono katika harakati zake za kuitenga Urusi katika jamii ya kimataifa. Tanzania tumeamua kuwa neutral/kutokuwa na upande katika mzozo wa Urusi na Ukraine.

Kwa Marekani ukiamua kutokuwa na upande unahesabika kuwa uko upande wa Urusi, na inafanya Kila jitihada kuyatisha mataifa yenye msimamo huo Ili yailaani Urusi! Kwa hiyo ukiandaa mazingira ya kukutana na Marekani kwa Sasa lazima ikushinikize kuilaani Urusi.

Sidhani Kama mama atakuwa na ubavu wa kuhimili shinikizo la Marekani katika jambo hili. Anaweza kujikuta amesema jambo ambalo hakutegemea akiwa chini ya shinikizo. Sidhani kama ataweza kuhimili Kama India na Afrika ya kusini zilivyoweza kuhimili.

Afrika hatuwezi kulaani Nchi ya Urusi iliyokuwa mstari wa mbele Sana kwenye harakati za upatikanaji wa uhuru kusini mwa afrika-(Zimbambwe, Msumbiji, Botswana, Angola, Namibia na Afrika ya kusini).

Wakati huo wapigania uhuru akiwemo Mandera walikuwa wanaitwa magaidi na Marekani!! Chonde chonde Samia Mungu akutie nguvu uwatolee nje mabeberu huko Marekani!
TANZANIA ina fuata mkondo wa Kutofungamana na Nchi yeyote
 
Samia anadanganya tu, how on earth anaenda matekani sasa, there is almost vita ya 3 ya dunia. Thanzania is facing very high inflation, yeye aenda matekani kula bata. This was really a very poor choice, kwenda shopping!
Marekani inakata 40% ya misaada yake kwa wale wote ambao hawakupiga kura dhidi ya urusi pale UN..huenda tunaenda kubembeleza
 
Karibia nchi zote za africa zinaongozwa na viwiliwili engine wanazo wazungu,wanaoitwa mabeberu na viwiliwili wakizima injini viwiliwili vinakata pumnzi,ndio maana safari za kwenda kwa wazungu haziishi.
 
Fikra za utegemezi hazitatuondolea kero za maendeleo. Swali la msingi tangu tumepata uhuru tumekuwa tukitegemea na kupewa misaada, je, imetuondolea umaskini?
Sipo kusapoti utegemez!! Napinga pale mtu anakuja na kualaum viongoz kwenda nje na kuomba msaada, kwasaab huu ni utegemez umewekewa mizizi tang enzi za mwalimu. Kama Taifa kwa watawala hawana dira ya Taifa kutuondoa taratibu kweny huu utegemez, so huez laumu wa sasa kwann aende nje kuomba msaada! Hata kipind cha Mwendazake staili ile ya kupiga vita wazungu haikupaswa. Ilitakiwa aweke misingi kimya kimya ya kuja kuondoa utegemez lkn haitakua haraka na rahisi tu, utawala tang enzi ulipaswa uweke misingi ya muda mref ya kujikwamua na utegemez.
 
Ushauri kwa mama: Akiona shinikizo limezidi, aamue kulaani Nchi zote zilizowahi kushambilia nchi nyingine. Aanze kuilaani Marekani kwa kuushambulia Iraq kwa kisingizio Cha silaha za maangamizi ambazo haikuwa nazo, kwa kuishambulia Libya, kwa kuishambulia Syria, na Kisha ndipo ailaani Urusi kwa kuishambulia Ukraine!

Wewe ni mwehu, unatoa ushauri huku tayari una upande.!
 
Mkutano wa wiki iliyopita wa EAC Tanzania iliwakilishwa na nani na why? Mpaka Rais wa Congo DRC alikuwepo mwanachama mchanga wa EAC.
 
Sipo kusapoti utegemez!! Napinga pale mtu anakuja na kualaum viongoz kwenda nje na kuomba msaada, kwasaab huu ni utegemez umewekewa mizizi tang enzi za mwalimu. Kama Taifa kwa watawala hawana dira ya Taifa kutuondoa taratibu kweny huu utegemez, so huez laumu wa sasa kwann aende nje kuomba msaada! Hata kipind cha Mwendazake staili ile ya kupiga vita wazungu haikupaswa. Ilitakiwa aweke misingi kimya kimya ya kuja kuondoa utegemez lkn haitakua haraka na rahisi tu, utawala tang enzi ulipaswa uweke misingi ya muda mref ya kujikwamua na utegemez.
Hii nchi imeanza kusaidiwa leo!? bongolala imesaidiwa miaka nenda rudi na nchi za ulaya ikiwemo nchi za scandnavia, ujerumani na uingereza, hapo hujaongelea marekani......ingekuwa ni nchi ya kuendelea isingekuwa hapa leo......ni kama watoa misaada walishajikatia tamaa, maana ni sawa na kuweka maji kwenye tenga.
 
Back
Top Bottom