View attachment 3189332
Kamanda Wenje mbona unazidi kumuanika na kumuharibia kabisa kamanda Mbowe,
Umesema CHADEMA hatuna pesa ni kweli hatuna lakini kwanini hatuna pesa?
Jibu wahisani hawamwamini tena Mbowe.
Naomba unijubu maswali haya,
1. Je, mikutano mikuu yote ya misingi zaidi ya 64,274 nchi nzima ni Mbowe katoa pesa zake?
2. Je, mikutano mikuu yote ya matawi zaidi 16,602 ni Mbowe ametoa pesa zake?
3. Je, mikutano mikuu yote ya kata zaidi ya 3,956 ni Mbowe katoa Pesa zake?
4. Je, mikutano mikuu ya majimbo yote 264 katoa pesa Mbowe?
5. Je, mikutano mikuu ya Mikoa yote 31 ni Mbowe katoa Pesa zake?
6. Je, mikutano mikuu yote 10 ya Kanda za Chama ni Mbowe katoa Pesa zake?
7.
Sasa Wenje, kama hawa wanachama waliogharamia mikutano mikuu yao yote tangu misingi mpaka Kanda wanashindwaje kujigharamia kwenye mkutano Mkuu wao huu maalum mmoja tu wa Taifa?
Mwisho, Mkutano Mkuu wa mwaka 2019 Mbowe aliichangia kiasi gani mbona hujasema??!!
Mbowe kwanini hakuchangia 2019 achangie 2024?!!
Hii TZS250M ni rushwa toka CCM
Hakuna namna Mbowe ataendelea kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA lazima apishe akili mpya za kutafuta pesa sio kuchangisha wajumbe wa Kamati Kuu kwani hilo sio jukumu la mjumbe wa Kamati Kuu.