IGP Simon Sirro: Magaidi wapatao 300 kutoka Msumbiji walivamia Kijiji cha Kitaya mkoani Mtwara

Aina haja ya mahakamani hao viumbe,wakikamatwa ni kuchukuliwa maelezo kisha wachinjwe.
 
Hao watu wakizidisha mashambulizi Tanzania itaingia Msumbiji ipende isipende.
 
Hakuna gaidi aliekamatwa hapo mmekamata raia wema tu mnawatesa.
 
Sijawai sikia magaidi 300 yamevuka mpaka wa USA or Israel
Magaidi 300 ni wengi sana

Hata 50 tu ni wengi sana. Hapo kuna ufa mkubwa sana kwenye usalama wetu. Yaani usalama Tanzania ni mbovu sna
 
Hapa bado kuna wale wanaoshindwa kufiria nje ya box,wao kila kitu ni siasa watakuja kuponda utazani wanaishi nje ya Tanzania au labda magaidi wakishambulia watakuwa wanawaachia kisa wao ni wa chama fulani.

Kazi nzuri imefanywa na askari wetu.
hiyo kufiria nje ya box ndio nini mkuu
 
Hata 50 tu ni wengi sana. Hapo kuna ufa mkubwa sana kwenye usalama wetu. Yaani usalama Tanzania ni mbovu sna
Ndo maana mi siamini kama kweli walikuwa 300 kama kweli icho kijiji kisingebaki na mtu mzima
 
Ndo maana mi siamini kama kweli walikuwa 300 kama kweli icho kijiji kisingebaki na mtu mzima
wakati mwingine pia serikali inaweza kuficha takwimu ili kutoa aibu,fikilia ikisema magaidi walikuwa 40 alafu hicho kijiji ukute kina mgambo na sungusungu 30,polisi wilaya 200+ hiyo si ni aibu ? kwamba watu 30 wamefanya ugaidi zaidi ya nusu saa na pia kuteka kifaru
 
Watu 80 wenye silaha wanaweza kuingia bongo na kutoka kirahisi hivyo? Kama ni rahisi hivyo tungekuwa tunashambuliwa kila siku.
kwa mujibu wa taarifa magaidi walipita njia za bahari/maji na walipoondoka walichukua simu zote kijijini
 
bila shaka ni wananchi kwa maana hao magaidi inadaiwa waliingia kijijini na kuanza kuchoma nyumba bila kujificha hivo basi lazima wananchi waliwahesabu
Haha ebu kuwa serious brother
Sasa hao wananchi waliwahesabu vipi huku wanashambuliwa?
 
Wanaogopa aibu kama ya Westgate kenya
 
Sijawai sikia magaidi 300 yamevuka mpaka wa USA or Israel
Magaidi 300 ni wengi sana
Wanaweza wakawa wengi lkn impact yake ikawa ndogo,USA walio wa shambulia sept 11 hawavuki 10 lkn impact yake ilikuwa kubwa dunia ilitikisika,walingia USA wakasomea urubani wakapata chansi ya kuwa marubani wakateka ndege na kulipua majengo yake,ina maana mda huo USA alikuwa wapi? manake alikuwa na mda mwingi wa kukusanya taarifa kuliko huku kwetu wameshtukiza wakashambulia wakaondoka.

Kwa Israel kweli magaidi hawakuwai kuvuka,ila Hizbolah wamesharusha rockets zao mara nyingi na kufanikiwa kupiga baadhi ya maeneo ya Israel,ina maana mda huo Israel alikuwa wapi.?

Hezbollah fires rockets into Israel from Lebanon
 
Haha ebu kuwa serious brother
Sasa hao wananchi waliwahesabu vipi huku wanashambuliwa?

mkuu,nipo serious hao jamaa inavoandikwa huko mitandaoni ni kwamba hawakuziba uso kama ulivoona zile clip.emu fikilia kwa mfano kijiji kizima mnatolewa nje nyumba zinachomwa moto alafu wananchi hawajazibwa uso wala magaidi hawajajificha,je hamuwezi kuwahesabu ? wakichukuliwa wananchi wote kila mmoja si atasema kwao walienda wangapi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…