IGP Sirro soma alama za nyakati, jiuzulu
Kuna mambo yanafanyika isivyo, I wish ningekuwa na nafasi nifanye write up ya kutosha yamkini iweze kuleta maboresho ya kukidhi mahitaji ya wakati ya waTZ.
 
Kuna mambo yanafanyika isivyo , I wish ningekuwa na nafasi nifanye write up yakutosha yamkini iweze kuleta maboresho yakukidhi mahitaji ya wakati ya waTZ.
Hayo wanayofanya unadhani ni kwa bahati mbaya au hawajui namna ya kuboresha?? Unakumbuka kikichotokea october 2020 and forth?
 
Hili liko wazi.
Ila kwa kuwa polisi wako upande wa chama chetu pendwa Cha CCM,wacha kazi iendelee.
Mungu atakuja kulipa kwa wakati.
 
Kwa hiyo wenye dhamana ya kulinda wananchi na mali zao wanaua ? [emoji24]
Inasikitisha Sana.

Lakini ukweli ndiyo huo, waliopewa dhamana ya kulinda Raia na mali zao, wanakuwa wao ndiyo wako mstari wa mbele, kudhulumu uhai wa Raia hao na kupora mali zao!

Hakika ni muda muafaka, IGP Sirro, atake asitake, ang'oke kwenye nafasi hiyo na ampishe mwingine atakayefanya Kazi kwa weledi
 
Kwanza ni kukithiri kwa kashfa nyingi zinalorihusu jeshi la polisi juu ya ukiukwaji wa haki za binadamu kwa kupiga na kutesa watuhumiwa kinyume kabisa na ibara ya 13 (6)(b)(e). Malalamiko yamekuwa mengi kiasi cha kulichafua taifa letu kuwa lina jeshi la wapiga raia na watesa raia wanaotuhumiwa kwa makosa mbalimbali.

Kuibuka kwa matukio ya mauaji ambayo yamelikumba taifa letu kiasi cha kuwafanya watanzania wapate hofu kubwa. Kufuruliza kwa mauaji haya yanatia hofu kuwa sasa maisha yao yapo hatarini na wauaji wamejiamini kuwa hakuna chombo kinachoweza kuwatia mikononi mwa sheria.

Kujihusisha kwa maafisa wa polisi na siasa waziwazi kiasi cha baadhi ya maafisa kukiri wazi wazi kuwa wanailinda Ccm ibaki madarakani kwa mtutu wa bunduki. Mfano ni afande Kiondo ambaye amefunguka hadharani kabisa.

Rushwa kuwa sehemu ya maisha ya jeshi la polisi huku wasio na pesa wanapotenda makosa ndio hufikishwa mahakamani ambapo wenye pesa hawagusi mahakamani kabisa.

Kwa mukutadha huu sirro alitakiwa awe amefutwa kazi.
Labda ndio Majukumu yake Mapya Nchi ina Mambo hii

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
Nashauri Rais achague meja general kutoka JW ndio awe IGP,

itaondoa kulindana na itaongeza ufanisi kwenye jeshi la polisi
 
Kwanza ni kukithiri kwa kashfa nyingi zinalorihusu Jeshi la polisi juu ya ukiukwaji wa haki za binadamu kwa kupiga na kutesa watuhumiwa kinyume kabisa na ibara ya 13 (6)(b)(e). Malalamiko yamekuwa mengi kiasi cha kulichafua taifa letu kuwa lina jeshi la wapiga raia na watesa raia wanaotuhumiwa kwa makosa mbalimbali.

Kuibuka kwa matukio ya mauaji ambayo yamelikumba taifa letu kiasi cha kuwafanya watanzania wapate hofu kubwa. Kufululiza kwa mauaji haya yanatia hofu kuwa sasa maisha yao yapo hatarini na wauaji wamejiamini kuwa hakuna chombo kinachoweza kuwatia mikononi mwa sheria.

Kujihusisha kwa maafisa wa polisi na siasa waziwazi kiasi cha baadhi ya maafisa kukiri wazi wazi kuwa wanailinda Ccm ibaki madarakani kwa mtutu wa bunduki. Mfano ni afande Kiondo ambaye amefunguka hadharani kabisa.

Rushwa kuwa sehemu ya maisha ya jeshi la polisi huku wasio na pesa wanapotenda makosa ndio hufikishwa mahakamani ambapo wenye pesa hawagusi mahakamani kabisa.

Kwa mukutadha huu Sirro alitakiwa awe amefutwa kazi.
Apo kwenye kujihusisha na siasa ndio pa ovyo kabisa.
 
Back
Top Bottom