IGP Sirro soma alama za nyakati, jiuzulu
Ni maajabu ya Dunia!

Kwa kada mwaminifu wa chama tawala, kupost kama mpinzani wa Chadema!
Ni ajabu na kweli!

Leo hii kada maarufu wa chama tawala cha Sisiem, kupost utadhani ni mpinzani wa Chadema!
Tatizo lenu ndio hilo
 
Sirro hakutakiww kuwa Ofisin kwa muda mrefu sana...ni ajabu polisi wanaua Raia na yeye bado yuko Anaendeshwa na gari za umma..
 
Mama wa michongo katika unafiki wake ...halafu nikikuta baadhi ya sehemu unakoti neno la Mungu huwa nafunga kinyeo ili usipate aibu ...mfyuuu

Unafki unaufanya wewe mwenye ID mpya kila kuchwao ili utukanie watu.... wewe endelea kutumia hicho kinyeo chako vibaya ukidhani kwamba umejificha sana.
Mimi niache nikoti neno la Mungu sababu hunijui kama unavyodhani unanijua. Tusiingiliane kwenye majukumu binafsi

Chukua na hiyo
Luka 8:17-19
"Kila jambo lililofichwa litawekwa wazi na kila siri itajulikana na kila mtu ataiona. Hivyo yatafakarini kwa umakini yale mnayosikia. Watu wenye uelewa kiasi watapokea zaidi. Lakini wale wasio na uelewa watapoteza hata ule wanaodhani kuwa wanao.”
 
Nivile tu kama Taifa hatuna utamaduni wakuwajibika kwa manufaa ya uma kwa kuachia ngazi,matatizo yanalolikumba Taifa kwa sasa ni ya kimfumo, mfumo nimbovu ambao umepelekea watu kuvunja katiba hadharani,haya unayoyaona sio kwa taasisi ya mapolice tu!.
Kwanza ni kukithiri kwa kashfa nyingi zinalorihusu Jeshi la polisi juu ya ukiukwaji wa haki za binadamu kwa kupiga na kutesa watuhumiwa kinyume kabisa na ibara ya 13 (6)(b)(e). Malalamiko yamekuwa mengi kiasi cha kulichafua taifa letu kuwa lina jeshi la wapiga raia na watesa raia wanaotuhumiwa kwa makosa mbalimbali.

Kuibuka kwa matukio ya mauaji ambayo yamelikumba taifa letu kiasi cha kuwafanya watanzania wapate hofu kubwa. Kufululiza kwa mauaji haya yanatia hofu kuwa sasa maisha yao yapo hatarini na wauaji wamejiamini kuwa hakuna chombo kinachoweza kuwatia mikononi mwa sheria.

Kujihusisha kwa maafisa wa polisi na siasa waziwazi kiasi cha baadhi ya maafisa kukiri wazi wazi kuwa wanailinda Ccm ibaki madarakani kwa mtutu wa bunduki. Mfano ni afande Kiondo ambaye amefunguka hadharani kabisa.

Rushwa kuwa sehemu ya maisha ya jeshi la polisi huku wasio na pesa wanapotenda makosa ndio hufikishwa mahakamani ambapo wenye pesa hawagusi mahakamani kabisa.

Kwa mukutadha huu Sirro alitakiwa awe amefutwa kazi.
 
Acha ibaki hivyo hivyo... Labda wananchi watajitambua zaidi.
 
Haitasaidia kitu.

Wabadili tu mfumo wa jeshi.
 
Amfute kazi mtu aliyemuwezesha kushinda uchaguzi kwa njia haramu?

CCM na Tanpol ni kitu kimoja kila mtu anamtegemea mwenzie kuendelea kuwepo.

Umeshajiuliza bila kuwepo kwa polisi uhai wa CCM ungekuwepo?

Jionee hapo.
 
Kwanza ni kukithiri kwa kashfa nyingi zinalorihusu Jeshi la polisi juu ya ukiukwaji wa haki za binadamu kwa kupiga na kutesa watuhumiwa kinyume kabisa na ibara ya 13 (6)(b)(e). Malalamiko yamekuwa mengi kiasi cha kulichafua taifa letu kuwa lina jeshi la wapiga raia na watesa raia wanaotuhumiwa kwa makosa mbalimbali.

Kuibuka kwa matukio ya mauaji ambayo yamelikumba taifa letu kiasi cha kuwafanya watanzania wapate hofu kubwa. Kufululiza kwa mauaji haya yanatia hofu kuwa sasa maisha yao yapo hatarini na wauaji wamejiamini kuwa hakuna chombo kinachoweza kuwatia mikononi mwa sheria.

Kujihusisha kwa maafisa wa polisi na siasa waziwazi kiasi cha baadhi ya maafisa kukiri wazi wazi kuwa wanailinda Ccm ibaki madarakani kwa mtutu wa bunduki. Mfano ni afande Kiondo ambaye amefunguka hadharani kabisa.

Rushwa kuwa sehemu ya maisha ya jeshi la polisi huku wasio na pesa wanapotenda makosa ndio hufikishwa mahakamani ambapo wenye pesa hawagusi mahakamani kabisa.

Kwa mukutadha huu Sirro alitakiwa awe amefutwa kazi.
Kufuta kazi,kutumbua na kuhamisha viongozi hakujaweza kumaliza tatizo la utawala wa CCM.Magu alitumbua majipu mwisho wake sote tunafahamu.
Tatizo letu Watanzania ni kuacha kuwa ving'ang'anizi.
Tusipong'ang'ana kupata Katiba mpya hali yetu itakuwa mbaya siku hata siku.
 
Inasikitisha Sana.

Lakini ukweli ndiyo huo, waliopewa dhamana ya kulinda Raia na mali zao, wanakuwa wao ndiyo wako mstari wa mbele, kudhulumu uhai wa Raia hao na kupora mali zao!

Hakika ni muda muafaka, IGP Sirro, atake asitake, ang'oke kwenye nafasi hiyo na ampishe mwingine atakayefanya Kazi kwa weledi
Atatokea idara ya Traffic POLICE,hiyo idara angalau kwa makusanyo madogo ya Tsh.2000 kwa kila gari wamedhibiti ajali za barabarani.
 
Back
Top Bottom