Ikulu: Rais Magufuli awaapisha viongozi walioteuliwa. Mathias Kabunduguru, Godfrey Mweli na Ali Sakila

Ikulu: Rais Magufuli awaapisha viongozi walioteuliwa. Mathias Kabunduguru, Godfrey Mweli na Ali Sakila

Kuombea mtu afe, hata gaidi, ni jambo baya.

Ni jambo ambalo kwa kanuni ndogo tu za utu siwezi kulitetea.

Ila, tujiulize. Inakuwaje mpaka rais aliyeanza urais kwa kupendwa na watu wengi sana akaja kuchukiwa mpaka kuombewa afe na watu wengi sana kwa njia ambayo si kawaida katika utamaduni wa Watanzania?

Tumekosea wapi au rais kakosea wapi?
Eti watu wengi sana!! Sure?...[emoji848][emoji848][emoji848]
 
Duh! Ila kuna kitu mkuu inabidi ajifunze hapa!

Kuzushiwa kifo na watu walivyokuwa wakishangilia unadhani tuna Taifa moja tena?

Wengi waliokuwa wakifurahia kwamba amekufa, walitoa sababu za wale mashabiki wake kufurahia mateso ya Lissu na walofurahia kupotezwa na inasemekana kuuwawa kwa Ben Saanane!

Hamkani mambo siyo shwari tusidanganyane!
Kioo cha MTU ni watu
 
Umefanya summary nzuri, ni majuha tu na hamna namna ya kuwaita majina mengine. Nadhani hata upumbavu ni staha sana kwao kuwaita.
Mzima mzima kutukana ni ujuha wa kiwango cha phd.
 
Rais wetu anaongea lakini hana furaha kabisa kama siku zote...

Amekwazika sana...


Cc: mahondaw
 
Hana cha kujifunzaZitto na kigogo2014 ndo wanapaswa kujifunza ktu
Halafu hawana heshima kabisa hawajui Rais ni no moja wengine tunafuatia anauwezo wa kusema kulala ianzie saa kumi alasiri na ikawa hivyo naona panahitajika somo la uzalendo na utu tatizo mananabii wa siku hizi wamebaki kuhubiri fungu la kumi na kuolewa wamesahau kuhubiri Tunda la Roho ambalo lina mashina yake Amani, Upendo,Uvumilivu,Utu wema Fadhili na mengine yanayofanana nayo, MUNGU Ibariki Tanzania
 
Eti watu wengi sana!! Sure?...[emoji848][emoji848][emoji848]
Mkuu, kwani unabisha?

Umefuatilia mijadala ya uvumi wa kifo cha Magufuli na watu walivyokuwa wanajadili kama "good riddance" ?

Ishawahi kutokea hivi kwa rais mwingine yeyote?
 
Mange Kimambi naye aliaibika Kwa style za kichawichawi hivi hivi!

Siku hizi kakunjia mkia makalioni
 
Huwa nakuona wa maana lkn akili zako zipo hovyo kbs.nakufatiliaga hila kwenye mahabaya siasa huna logic.bule kbs
Kuombea mtu afe, hata gaidi, ni jambo baya.

Ni jambo ambalo kwa kanuni ndogo tu za utu siwezi kulitetea.

Ila, tujiulize. Inakuwaje mpaka rais aliyeanza urais kwa kupendwa na watu wengi sana akaja kuchukiwa mpaka kuombewa afe na watu wengi sana kwa njia ambayo si kawaida katika utamaduni wa Watanzania?

Tumekosea wapi au rais kakosea wapi?
 
Kwa siku kadhaa sasa kuna watu [majuha] kupitia hii mitandao ya kueneza na kujazana ujinga na ujuha walikuwa wameshupaza shingo na kupaza sauti zao kutoa na kueneza uongo, uzushi, na pumba zao kuwa Rais ni mgonjwa, mara amekufa, sijui kapelekwa wapi huko kwenda kutibiwa, na kadhalika.

Wengine wakaja na upumbavu wao kuwa sijui kafanyiwa mambo ya kichawi huko Ruangwa. Wakaja na video inayoonyesha moshi kwenye sehemu aliyokuwa amesimama Rais wakati anahutubia. Wengine wakasema kwenye video hiyo wameona mwanga ambao hawana uhakika ni wa nini! Hata kama ni mwanga wa jua, eti hawakujua ni wa nini.

Just stupid beyond belief.

Nadhani sasa huo upumbavu wao umemalizwa na Rais mwenyewe. Nampongeza kwa yeye kuendelea kubaki njia kuu [taking the high road] na kufanya kazi zake.

Hao majuha wanaomwombea mabaya sasa sijui watakuja na tukio gani jingine!?!! Tusubiri tuone...

Ila nimestaajabu sana. Hivi hata kama mtu hukubaliani naye kisiasa na kiitikadi ndo umwombee mabaya ya kiwango cha kifo??

Kweli kabisa?? Yaani mtu unajitoa fahamu kabisa na kumwombea kiongozi wa nchi kifo??

Kifo hakina mwenyewe. Madhila maishani hayana mwenyewe.

Nyie mlokuwa mmeshupaa kuombea na kufurahia mmenufaikaje sasa?

Magufuli akifa leo hii wewe kama liuso lako lilikuwa na chunusi kama tunda la fenesi, hizo chunusi zitatoweka?

Bure kabisa.

Hii mitandao ya kijamii imetengeneza tabaka la majuha na mapunguwani kwa kiwango kikubwa sana hadi inatisha.

Ooh eti Kigogo kasema...[sasa hivi naona wametoka kwa ‘Da Mange kasema’ na wamehamia kwa Kigogo 🤣].

Wengine wanasema kuwa eti sijui Magufuli ajitafakari, ajifunze, n.k.

Ha! Ajifunze nini? Ajitafakari nini?

Kwendeni zenu huko.

Jitazameni nyie wenyewe kwanza kabla hamjaanza kuwahubiria wengine.

Mliokuwa mnashabikia madhila dhidi yake ndo mna la kujifunza na kujitafakari......

Wenu Ngabu aka Outlaw Immortal [emoji1548][emoji1617]


Sitaki kuamini kweli kweli Serkal yetu imeshindwa kumpata huyu Nyang'au Mzushi Kigogo?
 
Mwenye hekima huwa ana kikomo.

Mjinga/juha/ na mpumbavu hana kikomo.
Unanishangaza Nyani, watu ambao kwako ni majuha na wapumbavu unadhani wanaweza kweli kukuelewa? Waache tu waseme, wana uhuru kama wewe ulivyo na uhuru wa kuwaita majuha na wapumbavu hata kama siyo kweli.
Huwezi kulazimisha watu wampende mtu au wamchukie mtu. Huo ni uamuzi wao, uwe wa kijuha au wa kipumbavu.
Tatizo letu sisi binadamu ni kutaka kusikia vile tunavyopenda kusikia. Kutaka watu wafanye yale yanayotupendeza tu basi. Mwenyezi Mungu hakuumba dunia ya namna hiyo.
Hata JPM kwa mara ya kwanza leo nimemsikia akisema kwenye uongozi unatakiwa kuwa mvumilivu, utasemwa vibaya, utatukanwa na kusingiziwa. Kwa hiyo hata hayo yaliyosemwa na hao unaowaita majuha na wapumbavu rais anajua yapo na yataendele kusemwa na zaidi ya hayo.
Punguza hasira Nyani, kuna siku utawelewa hao majuha na wapumbavu au wao wakuelewe wewe japo nadhamu utakuwa muujiza.
 
Mkuu, kwani unabisha?

Umefuatikia mijadala ya uvumi wa kifo cha Magufuli na watu walivyokuwa wanajadiki kama "good riddance" ?

Ishawahi kutokea hivi kwa rais mwingine yeyote?
Kwasababu anapendwa,they care about him.kama unafuatilia mitandao mingine ukiachana na jf,umeona shangwe baada ya mzee meko kuwa hewani akiapisha?,kuna kikundi cha watu wachache ndio wanaenezaa propaganda,magufuli amewashika vizuri mafisadi,lazima wamchukie,2020 sio mbali,atabeba kura 90%.
 
Mange Kimambi naye aliaibika Kwa style za kichawichawi hivi hivi!

Siku hizi kakunjia mkia makalioni
idara ya usalama wa Taifa wa sasa sio ya kuchezea kigogo ni pambasi iliyofutiwa breed za mwanamke aliye MP
 
Huwa nakuona wa maana lkn akili zako zipo hovyo kbs.nakufatiliaga hila kwenye mahabaya siasa huna logic.bule kbs
Wewe usiyejua kuandika "bure" unaandika "buke" ndiye wa kuhukumu kama mimi ni wa maana au si wa maana?

Sijawahi kukuomba unione wa maana na wala sijawahi kutafuta yeyote anione wa maana.

Kwa hiyo ondoa shaka, nione ovyo unavyotaka.

Ila niachie uhuru wangu wa kuandika ninavyotaka.

Tena unavyozidi kuniona wa maana ndivyo unazidi kunipunguzia uhuru wangu wa kujieleza.

Kwa sababu kila nitakaloandika nitakuwa nafikiria "watu wananiona wa maana sana, nijichunge nisiandike ninavyotaka, niandike wanavyotaka watu wanaoniona wa maana".

Kwa hivyo, natoa tangazo kwako na wote mnaoniona wa maana sana.

Nawaomba msinione wa maana sana, kwa namna ya kuninyima uhuru wangu wa kujieleza.

Siku nikijisikia kumtukana mtu niweze kumtukana bila hofu ya kufikiri "watu wananiona wa maana sana".

Sihitaji mtu anayeandika "bule" badala ya "bure" awe jaji wa kunijaji mimi kama mimi ni wa maana au si wa maana.

Kama hujui herufi za Kiswahili tu, utajuaje kuhukumu kama mimi ni wa maana au si wa maana?

Unaandika kuhusu logic wakati hata herufi za Kiswahili zinakushinda?
 
Waliomzushia kifo wanajisikiaje?
Tz tuna siasa za hovyo sana
 
Back
Top Bottom