Imeniuma Sana kuona ng'ombe anakatwa kichwa, sitakula nyama maisha yangu yote

Imeniuma Sana kuona ng'ombe anakatwa kichwa, sitakula nyama maisha yangu yote

miaka fulani jamaa mmoja alipata kazi kwenye kampuni fulani ya kizungu kwa bahati ikatokea kipindi cha Noel na wazungu wakawa wanafikiria ni kwa jinsi gani wanaweza kuchinja bata mzinga.
jamaa akawajibu simple naweza basi jamaa akenda kwao akakamata kama tulivyozoea kuchicha kuku akawachinjia lakini kilichotokea sasa.
wakamwambia Kazi kwao basi kwa kuwa walimwona ni mtu katili sana.
😅😅😅😅sio chai hii mkuu
 
Ukatili haumfanyi mtu kwa 'mwanaume zaidi' au 'jasiri', zaidi zaidi ni kipimo cha ujinga na kukosa ustaarabu / ushenzi.

Nimechinja sana kuku nikiwa kijana, yaani nyumbani ndiyo ilikuwa kazi yangu hiyo. Lakini kuna siku nikiwa na kisu mkononi, nimemkany'aga kuku miguu na mabawa, kulikuwa na kuku wengine wawili watatu wamesimama pembeni wanaanglia kwa mshangao nilichotaka kufanya, nilijikuta tu namwachia yule kuku.

Nilitafakari sana ubinafsi wetu binadamu. Kuku wale tuliowafuga walikuwa wamenizoea sana, yaani pengine walikuwa wananiona kama mungu flani hivi kwao, alafu mwisho wa siku naishia kuwachinja kikatili kabisa.

Kurudi ndani nikaulizwa kuku yuko wapi, nikawaaambia kaniponyoka kakimbia, tuangalie utaratibu mwingine. Watu walinuna kwelikweli lakini maza akasema basi leo haikupangwa kuwa siku ya kuku, na tule mboga za majani.

Toka siku hiyo sijawahi tena kuchinja kuku.
 
Nje ya Mada kidogo.

Zamani kabla sijaoa nilikuwa na kademu kwao Machame - Moshi. Siku nikaenda kwao sikukuu nikashuhudia Kanachinja Mbuzi.

Nikaondoa wazo la kuoa kule.
 
Kuna uhusiano gani Kati ya ubora wa nyama na damu mkuu
Mkuu kwa ufupi ni kwamba damu ikiganda kwenye nyama inafanya nyama iwe km ya kibudu.Kuchuruzika kwa damu hufanya nyama kuwa tamu.Kitaalamu kuna Kitu kinaitwa "Carcass Marbling",means tenderness and juiciness of the meat.Samahani nimeshindwa kuiweka ktk Kiswahili,lkn Ina maana ya Nyama kuwa ktk hali ya ubora kwa kulika na utamu.Lkn km damu haijachuruzika hiyo "Carcass Marbling", haiwezi kuwepo.
 
Alaf unakuta huyu nae ni mtoto wa kiume kwa staili hii kwanini asivae hereni na kusuka na kuona Ni kitu Cha kawaida tu hata kuolewa pia ataona ni jambo dogo
Kisa kumuonea huruma mtongozaji
[emoji134][emoji134][emoji134][emoji134][emoji134]
 
😅😅😅😅sio chai hii mkuu
Sio chai Kuna kisa kimoja alinielezea mzee wangu wakati wanasoma Edinburgh Scotland walipograduate wakapanga kwenda kusheherekea graduation yao kiafrika wakabeba pombe zao na kondoo Kama watatu na walikuwa mataifa combined wakenya watanzania waafrika magharibi nk wakaenda porini na wakawaalika marafiki zao baadhi wa kizungu walipofika kule porini wakaanza kuwachinja wale mbuzi kwa visu .
Wale wazungu kuona ule ukatili walishindwa kuvumilia wakaanza kulia kule maporini wakina baba (mzee wangu) wakashangaa Kuna Nini wale wazungu wengine wakapiga simu polisi ndani ya muda mfupi helkopta ya polisi ikaja wakakamatwa kilichowaokoa wenzetu ulaya Wana Aina nyingi za polisi kwahiyo waliowatetea ni polisi wanaodili na Foreigners tu ndio wakasema hapana Hawa watu waachiwe maana hata huko kwao hufanya hivi hawajafikia ustaarabu na maendeleo Kama ya huku kwetu ndio wakaachiwa lakini wale wazungu waliowaalika waliwachukia kabisa .
 
Ndugu Wana Jamiiforums sikujua Kama ng'ombe anachinjwa kikatili vile.
Alilia Sana
Akatoa haja zote
Mwisho alilia machozi
Macho yakageuka rangi huku machozi yakambubujika kwa uchungu.

Imeniuma Sana naahidi kuwa vegan.

Superbug
Karibu mkuu tupo vegan wenzio huku
 
Dah heko mkuu kwa humanity
Ukatili haumfanyi mtu kwa 'mwanaume zaidi' au 'jasiri', zaidi zaidi ni kipimo cha ujinga na kukosa ustaarabu / ushenzi.

Nimechinja sana kuku nikiwa kijana, yaani nyumbani ndiyo ilikuwa kazi yangu hiyo. Lakini kuna siku nikiwa na kisu mkononi, nimemkany'aga kuku miguu na mabawa, kulikuwa na kuku wengine wawili watatu wamesimama pembeni wanaanglia kwa mshangao nilichotaka kufanya, nilijikuta tu namwachia yule kuku.

Nilitafakari sana ubinafsi wetu binadamu. Kuku wale tuliowafuga walikuwa wamenizoea sana, yaani pengine walikuwa wananiona kama mungu flani hivi kwao, alafu mwisho wa siku naishia kuwachinja kikatili kabisa.

Kurudi ndani nikaulizwa kuku yuko wapi, nikawaaambia kaniponyoka kakimbia, tuangalie utaratibu mwingine. Watu walinuna kwelikweli lakini maza akasema basi leo haikupangwa kuwa siku ya kuku, na tule mboga za majani.

Toka siku hiyo sijawahi tena kuchinja kuku.
 
Ndugu Wana Jamiiforums sikujua Kama ng'ombe anachinjwa kikatili vile.
Alilia Sana
Akatoa haja zote
Mwisho alilia machozi
Macho yakageuka rangi huku machozi yakambubujika kwa uchungu.

Imeniuma Sana naahidi kuwa vegan.

Superbug
Ulivyo elezea umenitia simanzi kwa kweli, na hapa nimepika ndizi nyama, sijui itakuaje.
 
Ndugu Wana Jamiiforums sikujua Kama ng'ombe anachinjwa kikatili vile.
Alilia Sana
Akatoa haja zote
Mwisho alilia machozi
Macho yakageuka rangi huku machozi yakambubujika kwa uchungu.

Imeniuma Sana naahidi kuwa vegan.

Superbug
Umewahi kula mayai huku kuku anakuangalia? Utaacha kula.
 
Back
Top Bottom