Inawezekana ni Kiburi na Jeuri or Real Busy? Wasaidizi wake hawajamwambia ukweli wa ubatili wa Katiba na Sheria ya Uchaguzi?,Tufanye nini kupata Haki?

Hii Hii ni baada ya we kushindwa kufanikiwa kupata fursa kupitia CCM siyo? Kwa hiyo sheria imepitishwa mwaka jana kbla ht haijatumika tuanze kufanya marekebisho? Miongoni mwa fani inayotakiwa kufutwa ni pamoja na sheria, ni fani ya kutengeneza migogoro na ujuaje mbuzi. Nchi haiwezi kuendelea kwa upuuzi km huo
 
CCM imejaa watu wasio na weledi
 
Wanaogopa kuondolewa madarakani. Hivi uchaguzi ukifanyika kwa uhuru na haki unadhani CCM itapiya? Hivi kwa akili timamu wangemchagua Samia apeperushe bendera wakati hata Chamani hawamyaki? Ila sauti ya wengi ni Sauti ya Mungu. One day yes!
 
ni kujidanganya tu kwamba eti kubadili sheria za uchaguzi na katiba ya nchi ndiyo haki,

na kupuuzia nahitaji msingi ya kilasiku ya mwananchi mathalani maji, elimu, afya, kilimo n.k
Uliwahi kusoma Rasimu ya Katiba ya Warioba iliyosheheni maoni na matakwa ya wenye nchi ambao ni umma wa Watanzania kuhusu wanavyotaka juu ya Katiba, Tume ya uchaguzi, nk?
 
Kwa wapumbavu kama hawa kupewa jukwaa la kutoa upumbavu wao sababu wanashiba bila kutoka jasho unafikiri tutafika bila kucharazana bakora kama Kenya?
 
Tatizo ni unafiki wa washauri. Upande mmoja wanasema Mama puuza ni hao hao wanalaumu kwa upande mwingine. Mmoja kati ya wanafiki wakubwa ni Mzee Kikwete ! Badala ya kufikiria nchi ni yeye tu na tumbo lake
Kweli naunga mkono hoja, wazee wanatakiwa wawe ni hazina lakini Tanzania ya CCM wazee wake ni wa hovyo kupindukia. Kwa umri wa akina Wassira, Kikwete, Msekwa Makamba hawana courage na uzalendo kama Nyerere wa kukemea kwenye mapungufu.

Wanafikiria matumbo na hatma ya vizazi vyao, tungepata wazee kama akina Warioba wenye uthubutu wa kukemea tungevuka salama.
 
Kwa wapumbavu kama hawa kupewa jukwaa la kutoa upumbavu wao sababu wanashiba bila kutoka jasho unafikiri tutafika bila kucharazana bakora kama Kenya?
Relax bas gentleman mbona huna hata hoja mayowe na makasiriko ya nini sasa,

tuliza ball na uwasilishe maoni mapya na fikra zako mbadala na bora zaidi ya zangu mbele ya wadau wa JF na itapendeza zaidi,

acha kimbelembele jukwaani bila hoja sawa gentleman?
usirudie tena hii kitu 🐒
 
Kama vile kuwaengua wapinzani kwa takriban 64,000 halafu wanashinda ushindi wa kishindo. Wananchi wa Tanzania wataendelea kuwaamini hofu ya nini kuwaengua kwenye uchaguzi wakati mnaaminika?

CCM imetengeneza wazee wa hovyo
 
Kama vile kuwaengua wapinzani kwa takriban 64,000 halafu wanashinda ushindi wa kishindo. Wananchi wa Tanzania wataendelea kuwaamini hofu ya nini kuwaengua kwenye uchaguzi wakati mnaaminika?

CCM imetengeneza wazee wa hovyo
Gentleman,
wale wote wasiokudhi sifa, vigezo na masharti ya kisheria na kikatiba kugombea uongozi wa nafasi mballimbali nchini, ni muhimu sana wakaenguliwa mara moja, ili kuepuka kunajisi katiba yetu tukufu ya Tanzania.

Ni Lazima wale tu waliotimiza vigezo stahiki vya kikatiba ndio wapewe fursa na nafasi ya kugombea uongozi.
haki inaambatana na wajibu.

Atakaeshinda uchaguzi, apewe nafasi na fursa ya kuwatumikia wananchi, bila mbambamba yoyote 🐒
 
Ifike hatua watanzania kwa pamoja akiwemo Paskali tuache unafiki na kusimama kwa pamoja na kudai haki zetu. Ni ngumu wakati wa kudai haki kwenye mabandiko yenu mnadeclare interest kwamba nyie ni CCM halafu mnalalamikia ukiukwaji huu wa sheria na katiba mkijitambulisha na taasisi inayokiuka hizo haki.

Na ndio maana umetafuta wa kumlaumu na wasaidizi wake siyo nyie mnaokujaga na mabadiliko ya kupongeza ushindi unaotokana na sheria hizo hizo.

Pascal acha unafiki huwezi kusukuma gari ukiwa ndani ya hilo gari, if you have guts shuka kwenye gari la wahuni njoo tulisukume au kaa kimya.
 
Na kwenye hilo ni CCM tu wanaokidhi?
 
Uliwahi kusoma Rasimu ya Katiba ya Warioba iliyosheheni maoni na matakwa ya wenye nchi ambao ni umma wa Watanzania kuhusu wanavyotaka juu ya Katiba, Tume ya uchaguzi, nk?
Gentleman,
ile ambayo wapinzani nchini kwa mwavuli wa ukawa waliikataa katu katu pale bungeni dodoma 2014, right?,🐒
 
Na kwenye hilo ni CCM tu wanaokidhi?
Gentleman,
vyama mballimbali vya siasa nchini vilivyo kidhi sifa stahiki, vigezo na masharti ya kisheria na kikatiba vilipata fursa ya kusimamisha wagombea uongozi maeneo mballimbali nchini.

Ni muhimu waliokosa fursa wakati ule wakajipange vizuri kwa chaguzi zijazo 🐒
 
Hii ntaisoma baadae maana inahitaji utulivu
 
Another foolish rhetoric, masikini jamii forums inatufanya tuingie tukikosa la kufanya
 
Who are u mpaka utukataze kutaja majina? Nini maana ya uhuru wa kuongea? Saa100 ni chura kiziwi mwenyewe amejiita hvyo
 
kama kuna dhambi inaliangamiza Taifa letu kwa sasa hivi ni uchawa na unafiki,wanajua mihimili yote,viongozi wa dini wako complomized na mhimili Mmoja so wanchowaza ni kugawana vyeo baada ya october,nani atamfunga paka kengere.
wanacnhi ndio hawa wanadhani kuna chama au mtu atawapambania badala yao.
 
1. Yale mapendekezo ya Kamati ya Professor Simpho Mukandala yako wapi? Yamefanyiwa kazi? Mbona alikuwa na nia ya kuyafanyia kazi? Kwanini tunatumia pesa za walipa kodi kwenye kamati ambazo hatupo tayari kutekeleza maoni yake?
2. Mtu mmoja peke yake hawezi kuleta mageuzi. Inawezekana amesoma mood ya wasaidizi wake ndani ya Kamati Kuu ya Chama, National Security Council, National Executive Council ya Chama na Cabinet. Akaona hapa mabadiliko hayatakiwi, akaamua kutulia. Bila consent kwenye hivyo vyombo na yeye hataweza kutekeleza chochote. Lazima na muhimu awe na backup ya hivyo vyombo.
 
Another foolish rhetoric, masikini jamii forums inatufanya tuingie tukikosa la kufanya
ni muhimu kuepuka kutapeliwa fikra, uhuru na haki zenu za kikatiba na vibaka wa siasa nchini.

kumbuka uchaguzi mkuu wa kihistoria Tanzania ni oct. mwaka huu 2025
 
Maji, elimu, afya kote huko mmefeli, wananchi tumewachoka hatuwataki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…