Inawezekana ni Kiburi na Jeuri or Real Busy? Wasaidizi wake hawajamwambia ukweli wa ubatili wa Katiba na Sheria ya Uchaguzi?,Tufanye nini kupata Haki?

Bahati mbaya Sina chama ni mtu huru kama ni kuunga mkono ningemuunga Mgombea huru kuliko Hawa wanaotokana na vyama kama Wewe!,Ambaye umekumbatia ufia chama hata kwa kuumizwa kwa kile kinachoitwa(Collective responsibility)!,Noma sana kuwa huru nao Uhuru utakuweka huru kweli kweli.
 
Naona unajaribu kuwa relevant, ila ukweli maandishi haya hayana maana tena, wengi wameshasema na ww unafanya marudio tu, ili huko mbeleni uweke link kwenye mabandiko yako kuwa uliwahi kuonya. Nenda mahakamani boss, ukazuie maana huwa unasema una imani na mahakama, na nchi hii inaongozwa na utawala wa sheria. Kinyume na hapo machafuko ama mapinduzi ya kijeshi ndio njia pekee za kupata katiba mpya ya kweli.
 
Naunga mkono hoja.
Kwa maana machafuko au vita ya wenyewe kwa wenyewe itaangamiza jamii yetu na amani tuliyojivunia miaka nenda rudi itakuwa historia.
Naipenda sana nchi yangu Tanzania.
Nchi aliyonipa mwenyezi Mungu.
Mungu Ibarki Tanzania.
 
Umenifurahisha sana uliposema wale matutusa na warembo wa vitu maalum. All in all nadhani kwa hatua tuliyofikia, ni nguvu ya umma pekee ndiyo itawarudisha wanasiasa mezani.

Mtihani uliopo ni ukosefu wa mtu sahihi wa kuiongoza hiyo nguvu ya umma kudai haki zao za msingi! Wengi wetu ni waoga. Na policcm wakishatupiga tu mkwara, tunaifyata mikia yetu.
 
Kwa muda mrefu sana sikuwa na soma post zako, Leo Nimesoma na nakubali kuwa Kuna madini
 
Naunga mkono hoja.
Kwa maana machafuko au vita ya wenyewe kwa wenyewe itaangamiza jamii yetu na amani tuliyojivunia miaka nenda rudi itakuwa historia.
Naipenda sana nchi yangu Tanzania.
Nchi aliyonipa mwenyezi Mungu.
Mungu Ibarki Tanzania.
Ushauri hujatoka mkuu,mbali na kuipenda nchi Yako!
 
mimi ni kiongozi, muhadhiri na mtaalamu wa siasa za vyama vya siasa gentleman na si vinginevyo
 
Pascal Mayalla Historia itakukumbuka kwa Kupigania Haki ya Watanzania Wote.
Jambo hili pamoja na mengine umeyasemea sana.
Hii kwako ni Legasi
 
Big up bro!
 
Good article. Tukiwa hivi naamini madhubuti tutaikomboa nchi yetu. Sisi hatukutakiwa kuwa hivi tulivyo. Tanzania imejaaliwa rasilimali mno
 
Pascal Mayalla kumjibu huyu mtu Kwa like ni kama kijishusha thamani! Hizi Ndio takataka ambazo haziwezi kuamua mustakabali wa taifa letu! Anaandika mambo kinasharia, kuwa watanzania waliowengi out if statistical reference! Ni ujinga sana uliopitiliza watu Hawa Ndio walimdangamnya Jiwe akafananishwa na Mungu akafa!
Please Kama umesema tuwe na jf ya miaka Ile hizi ghasia usizijibu
 
Nimekwambia tulia , hayo ya kusema ati walipo viongozi wakuu wa nchi nawe upo, kwanjza kama viongozi sio nchi , watakuepo na wataondoka ili waendelee heshimika lazima timiza maagano ya nchi na wananchi si vinginevyo , kama sivyo wataondoka kwa fedhea kubwa.

2. Jua mwaka huu hakuna uchaguzi so jitahidi weka ufisadi wako vizuri japo hautakuwa wa mda , maana siku unafukiwa utaondoka na yale ya kati ya miguuni yako tu bila kujali ke au me na mwaka mmoja ukifukuliwa utakua kama mti.

3. Mnaojitwika mzigo mkubwa kuwa chawa ,Bwana anasema mwakesha bure

4. Huwezi kuwa na akiri kubwa kama wewe na bado upo ccm kama sio mchawi , mzandiki , chawa , so Mungu anaongea nawe toka huko hutaki utaenda kufa mdomo wazi.

Thanks
 
unatoa ushauri na huna hoja gentleman dah?

sasa si ujiandikie mabandiko yako na ukae nayo chumbani kwako, kumbwelambwela kwa mihemko na makasiriko ni ushirikina huo gentleman

hakuna haja ya maringo gentleman,
kufa kila mtua atakufa tu hata akiwa mjinga au mjanja,

na,
infact mwili wako na wangu vitaliwa mchangani na hiyo haina mjadala mrefu sana kwasababu ni kadiri ya majira na wakati wa Mungu dhidi ya kila mwanadamu.

Muhimu zaidi ni kwamba,
iwe mvua, liwe jua, hakuna aya, hakuna nukta wala koma kwenye sheria au katiba ya nchi itabadilishwa kuelekea uchaguzi muhimu sana wa kihistoria, utafanyika october mwaka huu2025, bila kelele wala mdomo wa kibaka au tapeli yoyote wa kisiasa humu nchini.
 
Umeandika kitu kizuri sana, nakuunga mkono Kaka P. Jibu liko kwenye Aya yako ya 5. Shida iko kwetu Wananchi kwanza hatuna umoja, kupigania kitu ambacho wote tunataka. Tuko kimatabaka, wanaojipendekeza wanaona mambo yalivyo yanatosha.

Kuna wenye akili wasiojinyenyekeza wao wanataka cake iwe ya nchi nzima, hawa ndiyo wakisema ng'wee kesho katekwa. Sisi wananchi tungekuwa na Umoja Katiba mpya tungeipata, tungepata Tume huru ya Uchaguzi.

Wakati watu tunapigia kelele tume huru ya Uchaguzi, iko mijitu ikisifia na kusujudu vitu vya hovyo, ilimradi wapate teuzi. Hapa tuna shida kubwa na kundi la watu waroho, walafi wa madaraka. Wanatuchelewesha kuwa na Tanzania tuitakayo.

Sisi sote tukiungana hakuna Serikali duniani inashinda mbele ya umoja wa wananchi wote, watafata vile tunavyotaka na si wao watakavyo. Bahati mbaya tuna mijitu ya ajabu sijui ilikuaje ikawa mitanzania inaumiza sana.
 
Gentleman,
uwe na imani haba au thabiti kwa Mungu na kwa serikali,

uchaguzi mkuu wa Tanzania utafanyika kwa mujibu wa katiba kama ulivyo pangwa bila wasi wasi wala chokochoko kutoka kwa chama cha siasa au kundi la watu Fulani wenye mlengo yao binafsi.

Tujitokeze kupiga kura bila kukosa ndugu zangu 🐒
 
Kwa mfano wa mabandiko yako haya,kamwe huwezi pata ubunge kupitia chama kile.
 
Shauri yako ,utajiju nimetimiza agizo la Mungu wangu juu yako ,so kama wafikili ni utapeli kama wa ccm ,OK kama Mungu wangu ataamua ugonvi kati yangu na wewe kwa hili sawa

Sikia la mwisho ,Mungu ŵangu anasema machawa wote wataenda kufa midomo wazi , bila kujali level ya uchawa , wewe kama mchangiaji hapa jf , umekua ukionekana kama chawa ila akili ipo , so nimekwambia kwa moyo mweupe ,utaki sawa unataka sawa , thanks
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…