Ingekuwa vipi ulimwengu kama kusingekuwa na dini, dunia bila dhambi kipimo cha uovu nini?

Umeenda vizuri, ila naomba nikuongezee kipengele kidogo.

Dini siyo lazima ihusishe mungu ama shetani.
 
Mkuu ni vipi unathibitisha kwamba sheria za dini zimetungwa na mwanadamu?
Kwa sababu huyo Mungu anayedaiwa ndiye mtungaji wa hizo sheria za dini hajawahi kuwepo, hayupo na hata uwezekano wa kuwepo kwake Haupo.

Ni binadamu wametunga sheria zao na kuunda dhana uchwara ya kufikirika na kuiita Mungu kudai ndio ametunga ilhali ni haohao binadamu.

Ndio maana kila dini inakuwa na sheria zake halafu hapohapo kila dini inataka kukuaminisha sheria za dini yao ndizo sheria pekee za huyo Mungu.

Mkristo atakwambia Mungu amemwambia aoe mke mmoja, Mwislamu atakwambia Mungu wake alimwambia anaweza kuoa mke zaidi ya mmoja. Hapa tayari kuna Contradiction.

Automatically haiwezekani awepo Mungu mmoja anayetoa sheria moja yenye Contradiction.

Hivyo unaona kwamba hizi sheria zinazodaiwa niza huyo Mungu ni sheria za wahuni tu binadamu walio plan mawazo yao tu yaonekane sheria.
 
Sawa, unadhani ingekuwa vipi maisha ya mwanadamu bila sheria na makatazo?
 
Tunajua sheria za nchi zinatungwa na nani, niambie sheria za dini zilitungwa na kina nani kwa wakati gani.
 
Tunajua sheria za nchi zinatungwa na nani, niambie sheria za dini zilitungwa na kina nani kwa wakati gani.
Kasome Historia ya kanisa na Mitaguso yake.

Mikutano mbalimbali ya kikanisa imefanyika karne na karne kutunga sheria na kufanya modification zake.

Kasome Historia kwanza.
 
Sawa, unadhani ingekuwa vipi maisha ya mwanadamu bila sheria na makatazo?
Japo kwa namna Moja au nyingine dini inaweza kuwa chanzo Cha maadili, lakini sio lazima mtu awe na dini Ili awe na maadili.
Kutegemea nguvu ya kiroho kama chanzo Cha maadili, ni kama vile kusema maadili sio kitu Cha asili, jambo ambalo sio kweli.
Wanyama wengi kama vile nyani na panya hawana dini, lakini wanayo maadili ya kuzuia vitu kama wizi na mauaji.
 
Mkuu lakini Buddhist si wanayo masanamu na wameyaweka ndani? Wanaomba na kutoa shukurani. Je ile sio Miungu yao?
Hapana.

Again, Buddhists do not believe in any kind of deity or god, yule ni Buddha/Mwalimu, Siddhartha Gautama, Founder wa Buddhism,
is considered an extraordinary being, but not a god. The word Buddha means “enlightened.
Followers of Buddhism don’t acknowledge a supreme god or deity. They instead focus on achieving enlightenment, a state of inner peace and wisdom.
"When we bow, we express outwardly what we feel inwardly, our gratitude to the Buddha for what his teachings have given us."
Pitia link hii hapa chini ambapo nimechukua rejea za baadhi ya majibu niliyoweka hapo juu.


Hapo utapata kujua mengi kuhusiana na dini ya Buddha.
 
Kasome Historia ya dini zote.

Ndipo utajua ni wahuni wachache waliji organize kuunda mfumo wa ulaji na kuiita dini.
Sawa, japo nafahamu historia lakini nitarejea na kupitia kwa ufupi kuona kama ni kweli ni sheria za watu na makundi yao.
 
Sawa, kwaiyo unaona ni sawa watu kuishi bila sheria na taratibu?
 
Maelezo yamenyooka mkuu, sasa nimeelewa sio kila dini lazima iwe na Mungu.
 
Sheria na taratibu ni muhimu ziwepo, ila sio lazima zitoke kwenye vitabu vya dini kaka.
Sawa kaka, mimi kwa upande wangu nazingatia na naheshimu sheria za pande zote, pia sio mbaya kubaki na upande mmoja, ni changuo la mtu.
 
Kungekuwa hakuna marginalization wala watu kupigika na shida (hence finding hope) wala dini zisingekuwepo...

In short the mass needs their Opium....
 
Mleta mada Mvivu kutafuta vitu...Dini hapa Tanzania Imeingia karne ya 19 Jiulize izo karne nyingine watu waliishije?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…