Interview ya Tundu Lissu yasitishwa Wasafi FM. Mwenyewe ang'ang'ania ofisi za Wasafi. Wakubaliana kuifanya wakati mwingine

Interview ya Tundu Lissu yasitishwa Wasafi FM. Mwenyewe ang'ang'ania ofisi za Wasafi. Wakubaliana kuifanya wakati mwingine

Wasafi, nao Wana mumunya mumunya tu.

Hatahivyo, tabia ya kukurupuka na kwenda kuvamia kituo cha redio, eti kwasababu hakuridhika na taarifa ya kufutwa au kubadilishiwa Mahojiano yake-Kina uashiria wa Udikteta. Ubabe Ubabe.

Sidhani kama Diamond ana wajibu. Labda kama makubaliano hayakuwekewa kipengele cha "Kusitisha mahojiano bila ya sababu yeyote ile"

....anywho
Unajua Tundu Antipas Lisu ni mgombea Urais kupitia Chama kikuu cha Upinzani hivyo ni mtu nyeti

Kwa maana hiyo Ratiba zake haziwezi kuvurugwa na Watu Wadogo Wadogo kama akina Zembwela 😄
 
Habari zilizonifikia hivi punde ni kwamba interview ya Mh. Tundu Lissu pale Wasafi FM imefutwa.

Awali ilielezwa kwamba Tundu Lissu angefanya mahojiano katika kituo cha Wasafi. Taarifa zisizowekwa wazi ni kwamba mahojiano hayo yamefutwa kufuatia maelekezo ya CCM

Updates

Tundu Lissu sasa yupo Wasafi FM kupata sababu za msingi za kufutwa kwa mahojiano. Licha ya kupewa taarifa kwa njia ya simu, Lissu hakuridhika na badala yake amekuja mwenyewe Wasafi. Uongozi wa Wasafi umeomba radhi bila kueleza sababu za msingi
Wasafi wameepuka Nuksi 🐒
 
Unajua Tundu Antipas Lisu ni mgombea Urais kupitia Chama kikuu cha Upinzani hivyo ni mtu nyeti

Kwa maana hiyo Ratiba zake haziwezi kuvurugwa na Watu Wadogo Wadogo kama akina Zembwela 😄
Ahhh. 😂Kwani pale ni maelezo. Apunguze Udikteta

Akamalizie kombe lake la Uji, aje afanye mahojiano humu basi. T.L aje tu J.F amalize nyongo.
 
Tundu Lissu sasa yupo Wasafi FM kupata sababu za msingi za kufutwa kwa mahojiano. Licha ya kupewa taarifa kwa njia ya simu, Lissu hakuridhika na badala yake amekuja mwenyewe Wasafi. Uongozi wa Wasafi umeomba radhi bila kueleza sababu za msingi[emoji419][emoji375]

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwani anashare pale wasafi hadi aelezwe sababu?
 
Makamu Mwenyekiti wa Chadema Tundu Lissu bado yupo kwenye ofisi za WASAFI FM , akisubiri atajiwe jina la Mtu aliyezuia Mahojiano yake kwenye kioindi cha GOODMORNIG .

Screenshot_2024-02-07-09-45-19-1.png

Lissu alialikwa kwenye kipindi hicho lei aaubuhi , lakini ghafla maagizo kutoka juu yakawatwanga mkwara Wasafi FM kutothubutu kumpa MIC Tundu Lissu
 
Hata sijui mnashangaa kitu gani hapo, kwangu hata kama mahojiano yangefanyika, naona hizo ni siasa tamu za muda mfupi tu

Diamond = CCM.

Kitenge = CCM.

Hayo mambo ni kuyazoea na kuachana nayo, tazameni njia nyingine zenye maana zaidi na uzito, zenye kuleta mabadiliko kiuhalisia, sio kwa maneno.

Hata Lissu sioni maana kwake kwenda huko kupata maelezo, hao jamaa wanatumiwa na CCM, ndio wanaowapa leseni, lakini pia, mambo mengine ni maamuzi yao kwani kituo ni chao.

Kama wameamua kuhairisha au kufuta, muhimu wamuombe radhi Lissu kwa usumbufu, biashara iishe, lakini sio kila siku tuendelee kushangaa hadaa zile zile za miaka yote, ni ujinga.

Lissu nae kama anaona amepotezewa muda, aende mahakamani kudai fidia, lakini sio kugomea kwenye ofisi za watu, ataonekana msumbufu mwishowe aje kuondolewa hapo na polisi, now what is that..!!
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Habari zilizonifikia hivi punde ni kwamba interview ya Mh. Tundu Lissu pale Wasafi FM imefutwa.

Awali ilielezwa kwamba Tundu Lissu angefanya mahojiano katika kituo cha Wasafi. Taarifa zisizowekwa wazi ni kwamba mahojiano hayo yamefutwa kufuatia maelekezo ya CCM

Updates

Tundu Lissu sasa yupo Wasafi FM kupata sababu za msingi za kufutwa kwa mahojiano. Licha ya kupewa taarifa kwa njia ya simu, Lissu hakuridhika na badala yake amekuja mwenyewe Wasafi. Uongozi wa Wasafi umeomba radhi bila kueleza sababu za msingi
Huyu mtu anasemaga uongo na kueneza falsafa isiyofaa ya uliberali tanzania. Eti kila kitu ruksa na kushindana. Wanaruhusu ushoga umalaya eti ni uhuru wa mtu. Asante wasafi kufuta mahojiano na hii kibaraka wa sera za sisi kunyonywa na wageni.
 
Back
Top Bottom