Ipi sahihi sana kati ya Kumsomesha mtoto msingi english medium ya ada 3m per year vs kumsomesha kayumba na kumnunulia kiwanja cha 3m kila mwaka?

Ipi sahihi sana kati ya Kumsomesha mtoto msingi english medium ya ada 3m per year vs kumsomesha kayumba na kumnunulia kiwanja cha 3m kila mwaka?

Mkuu hoja yako ni ya kimasikini sn.
Elimu yetu ya sasa sio ile tuliyosoma miaka ya 80-90.
Peleka mtoto English medium umjenge mtoto msingi mzr wa maisha.
Ukifikiria sn pesa ,,,hata pesa ya kula unaweza ukapiga hesabu ukaona unakula pesa nyingi sn kwa mwaka,,
ukashindwa kula mara 3 kwa siku.. ili pesa zingine usave ununuwe asserts.
Watoto wanaosoma English medium wanaojielewa mapema sn kuliko hawa wa serikali..
Ems inamjengeaje misingi mizuri ya maisha mtoto hali ya kuwa elimu na mtalala unao tolewa kule ni ule ule inayo tolewa kayumba ila Kwa lugha tofauti au ww kwako mtoto kujua kiingereza ndo msingi wa maisha?
,Elimu bora ni ile inayo patikana Internation school basi ,hizi Ems ni kayumba zilizo changamka.
Alafu kingine msingi mizuri wa maisha mtoto huwa hautoi shuleni bali huwa anautoa Kwa wazazi wake.
 
Wewe umemaliza Kila kitu
 
Mtaala wa elimu ya Tz Kwa ujumla ni takataka Kwa hiyo haijalishi unamsomesha mtoto wako kwenye shuleni gani kama hiyo shuleni unaongozwa na mtaala wa Tz basi mtoto wako ni anajaza takataka kichwani.
Sasa ww utachagua umjaze mtoto wako takataka Kwa bie nafuu au Kwa bei kubwa.
 
Kunadogo langu limepiga kuanzia chekechea ad form zaidi ya milion 20 zimekatika,afu limepata division 2 yaani hata wa Kayumba wamempiga

Kama mzee angekua ananunua ndama wa laki 3 saiv angekua na ng'ombe 70 miaka zaidi ya kumi yangekuwa makubwa anauza hata kwa m3 au 1.5 angepiga zaidi ya milion 100 ungefaa kua mtaji wa mtoto angemdakia hata kusta asimamie

Dogo limemaliza shule limekuja kufuga rasta tu na kuvaa majeje limekaa home tu

Lengo la kupeleka private aje kua daktari,ila sasa mambo yamekua tofauti

Watoto wengi waliosoma shule za kishua wanakuwa na umayai mayai sana. Hawapendi majukumu. Maana washazoea kufanyiwa kazi. Ndio maana japan watoto wadogo wanajifanyia usafi wenyewe shuleni. Hii wanafunza majukumu mapema

SnapInsta.to_746003091_18098250173141184_4874430027258733629_n.jpg
 
habari wadau, naombeni majibu njia gani nzuri ambayo mtoto itamsaidia sana mbeleni.

kati ya hizo option mbili, maana baba yake kipato changu kidogo hakiruhusu kufannya vyote kwa pamoja. hivyo kipi sahihi cha kufanya ambacho kitamsaidia mtoto na hata akiwa mtu mzima hatanilaumu baba yake ?

maana nimeona changamoto za ajira na graduates kukosa mitaji zimenitisha

View attachment 3677289
Kati ya suala ambalo linajadiliwa sana mitandaoni kuhusu Elimu ni wapi kunapatikana Elimu Bora?
Kwa bahati mbaya sana, wote wanaoongelea kuhusu Elimu Bora hata hawajui maana ya Elimu Bora. Kwao Elimu Bora ni matokeo mazuri ya MITIHANI.
Duniani nchi inayoongoza kwa ubora wa Elimu ni Ufini (Finland) ingawa kwao hawatumii MITIHANI kama huku kwetu.
Lengo kuu la Elimu (kama ilivyofafanuliwa katika azimio la Musoma) ni kumwandaa na kumsaidia mtu ili aweze kupambana na mazingira yake. (Rudia kusoma hilo lengo la Elimu)
Sasa, ni wapi ambapo ukimpeleka mwanao atapata Elimu itakayomsaidia kupambana na mazingira yake kwa hapa bongo?
Kuna suala pia la kwamba Elimu Bora ni Ile ya kuongea Kiingereza (English medium). Wandugu Kiingereza ni lugha sawa na kiswahili, Kisukuma, kimakonde, kizaramo, Kiha nk. Lugha yeyote duniani, Ina sifa 3, inazaliwa, inakua, inaishi lakini pia inaweza kufa.
Hebu tushuhudie hapa, wote waliosoma Kiingereza na wakawa mahiri mashuleni huko, baada ya kumaliza Elimu zao, na Leo wapi wanaishi hapa nchini, Kiingereza chao kinawasaidia katika lipi?
Ukweli ni kwamba, ama wamekisahau kabisa au kimeporomoka sana kiasi kwamba, ukiwaweka pamoja na wale waliosoma kayumba hakuna tofauti.
Kama huu ndiyo ukweli, je, kulikuwa na haja Gani ya kugharamika kwa mamilioni kwa ajili ya Kiingereza kitakachokufa? Lakini wakati huo huo, wako waliopita Kayumba na Kiingereza broken wakapata connection zinazowalazimu kutumia Kiingereza muda wote, wameimprove ni wanakigonga kuwazidi mbali waliosoma English medium.
Kwa hiyo maisha ni mind set TU, Elimu ni kichocheo na nyenzo mojawapo kati ya nyingi, Wala siyo maisha yenyewe.
 
Haya ni mawazo yako mkuu. Binafsi kipindi nipo form 1 nilisoma shule ada ni milioni 2. Then nikashindwa kuendelea Kwasababu mzee alipata changamoto ya kifedha mara bàada ya mama kuumwa sana. Form 2 nkaamia kidumu na ufagio, nikapata division 1 ya 7 form 4 division 1 ya 12. Na nilisoma kidumu na ufagio. Na Kuna watu walioendelea kusoma pale kwenye shule ya private wakapata 3 na 4. Endelea kukariri maisha hvyhvy.
Kinachofanya mwanafunzi afaulu sio shule tu, hata IQ yake na bidii ya kusoma.

Usidhani private schools watu wanatafuta kufaulu tu, hata exposure. Age mates wangu waliofanikiwa ni wale waliosoma shule za private. Niliosoma nao Kayumba ni bodaboda, walinzi, jobless na kazi za kijungujiko kibao. Sasa haimaanishi kwa vile bahati nzuri IQ yangu ilikuwa vizuri basi nikaze fuvu eti wanangu watasoma shule za kwenda na kuni. What if wanangu hawatakuwa na uwezo kama wangu?

Alafu mtu kama baba yake analipa 2M per month unadhani hivyo viwanja na shamba hamnunulii?
Njoo kwetu sasa, mzee hakunilipia ada na wala hata kijiko sijawahi ambulia. Sijawahi waona hao mnaowasema wanakwepa ada wananunua viwanja, nawaona wanaolipa ada na viwanja na mashamba wananunua.

Kuna family friend alikuwa na akili maandazi kama za mzee wangu. Yeye watoto wake wawili wa mwanzo nimesoma nao, ni vilaza kupindukia walifeli Form 2. Akashtuka akapeleka kuanzia 3rd born hadi last born private, ni wanne. Wote hao wanafanya vizuri na 3rd born chuo tiyari, 4th yuko chuo Muhimbili, 5th yuko wapi sijui. Baba mmoja, mama mmoja. Wale wawili wa mwanzo mzee wao ana mashamba ya miti wanauza wananunua bodaboda wanalewea kisha wanarudi tena kuvizia. First born kamfukuza hataki kumuona tena.

Sijawahi ona hasara ya kulipa ada kubwa. Mbona hamuoni hasara ya pombe, kulewa, kuhonga, umalaya?
Sidhani kama mtu anaweza nishawishi nisitumie gharama kuandaa mazingira mazuri ya watoto wangu. Cheap propaganda na poverty mentality haziwezi nizuia investment ya maana kwa watoto wangu.

Kuna watu nimesoma nao Advance na chuo unamuona kabisa huyu angesoma shule yangu huyu angeishia Form 4. Ila akitoka hapo ana exposure, anajiamini and by the way interviews nyingi sana bongo hazitaki vyeti unless sehemu muhimu kama BOT, EGA, etc. Hao hao ndio wameenda UN organizations au kujiajiri. Kiudumu na mifagio sasa wewe mtu mzee wako alikuwa anaona 2M per year ni hasara, 10M ya mtaji ukikosa ajira ukawa na idea atatoa wapi?

Hapa mnabishana baina ya kuwa responsible na kuwa zaa serikali italea. Kuwa maskini kusifanye watu wakatafuta visingizio, unaweza kubali reality hata kama inaumiza.

Yaani kitu kinafanywa na wafanyabishara wakubwa, wanasiasa wote hata walioishia la sita, wachungaji wakubwa, sheikhs wakubwa, wakulima wakubwa, wachimba madini, kina Diamond ambao hawajasoma, hata madalali kama Dotto Magari ambaye hajui kuandika na anatukana wasomi. Wote hao wanapeleka watoto private schools ila JF unakutana na makapuku wanatafuta visingizio eti ni kuzika hela. Kwamba hao wengine wote ni wapumbavu, sisi humu ndio wajanja sana si ndio?
 
Ukiona mtu anapiga hesabu za hivi ujue hana elimu na pesa ... Elimu ni msingi mzuri wa mtoto , hata uwekeze utajiri mkubwa kiasi gani kama mtoto hana elimu atauza vyote kwa siku moja tu kwishaaaaa. SOMESHA MTOTO

Elimu ya pesa ama Financial literacy haifundishwi private school tu.

Hata mtoto wa kayumba pia unaweza ukamfundisha elimu ya pesa. Maana elimu anaipata hata nyumbani pia

Elimu sio darasani tu. Shuleni. Hata hapa jamiiforums tunapeana elimu pia ya mambo mbali mbali kwa kusoma post za watu

SnapInsta.to_813212426_18631768891003940_4614022344152631327_n.jpg
 
Mbezi juu
Kwa Ilala kuna
Olympio
Diamond
Bunge
Zanaki
Kisutu

Kinondoni kuna
Mwenge
Michael Urio
Oysterbay
Makumbusho
Makongo
Ali Hassan Mwinyi

Zipo nyingi kwa hapa Dar. Kuanzia ada, chakula na usafiri, kwa ujumla kwa mwaka imezidi sana ni 1.2 ila mara nyingi inagotea laki 8,9 hadi 1m.
 
Kinachofanya mwanafunzi afaulu sio shule tu, hata IQ yake na bidii ya kusoma.

Usidhani private schools watu wanatafuta kufaulu tu, hata exposure. Age mates wangu waliofanikiwa ni wale waliosoma shule za private. Niliosoma nao Kayumba ni bodaboda, walinzi, jobless na kazi za kijungujiko kibao. Sasa haimaanishi kwa vile bahati nzuri IQ yangu ilikuwa vizuri basi nikaze fuvu eti wanangu watasoma shule za kwenda na kuni. What if wanangu hawatakuwa na uwezo kama wangu?

Alafu mtu kama baba yake analipa 2M per month unadhani hivyo viwanja na shamba hamnunulii?
Njoo kwetu sasa, mzee hakunilipia ada na wala hata kijiko sijawahi ambulia. Sijawahi waona hao mnaowasema wanakwepa ada wananunua viwanja, nawaona wanaolipa ada na viwanja na mashamba wananunua.

Kuna family friend alikuwa na akili maandazi kama za mzee wangu. Yeye watoto wake wawili wa mwanzo nimesoma nao, ni vilaza kupindukia walifeli Form 2. Akashtuka akapeleka kuanzia 3rd born hadi last born private, ni wanne. Wote hao wanafanya vizuri na 3rd born chuo tiyari, 4th yuko chuo Muhimbili, 5th yuko wapi sijui. Baba mmoja, mama mmoja. Wale wawili wa mwanzo mzee wao ana mashamba ya miti wanauza wananunua bodaboda wanalewea kisha wanarudi tena kuvizia. First born kamfukuza hataki kumuona tena.

Sijawahi ona hasara ya kulipa ada kubwa. Mbona hamuoni hasara ya pombe, kulewa, kuhonga, umalaya?
Sidhani kama mtu anaweza nishawishi nisitumie gharama kuandaa mazingira mazuri ya watoto wangu. Cheap propaganda na poverty mentality haziwezi nizuia investment ya maana kwa watoto wangu.

Kuna watu nimesoma nao Advance na chuo unamuona kabisa huyu angesoma shule yangu huyu angeishia Form 4. Ila akitoka hapo ana exposure, anajiamini and by the way interviews nyingi sana bongo hazitaki vyeti unless sehemu muhimu kama BOT, EGA, etc. Hao hao ndio wameenda UN organizations au kujiajiri. Kiudumu na mifagio sasa wewe mtu mzee wako alikuwa anaona 2M per year ni hasara, 10M ya mtaji ukikosa ajira ukawa na idea atatoa wapi?

Hapa mnabishana baina ya kuwa responsible na kuwa zaa serikali italea. Kuwa maskini kusifanye watu wakatafuta visingizio, unaweza kubali reality hata kama inaumiza.

Yaani kitu kinafanywa na wafanyabishara wakubwa, wanasiasa wote hata walioishia la sita, wachungaji wakubwa, sheikhs wakubwa, wakulima wakubwa, wachimba madini, kina Diamond ambao hawajasoma, hata madalali kama Dotto Magari ambaye hajui kuandika na anatukana wasomi. Wote hao wanapeleka watoto private schools ila JF unakutana na makapuku wanatafuta visingizio eti ni kuzika hela. Kwamba hao wengine wote ni wapumbavu, sisi humu ndio wajanja sana si ndio?
Ebu naomba uniambe ni vitu gani cha ziada kinacho fundishwa EMS alafu kayumba hakifundishwi.
Kwa hiyo kwako ww wote walio somea EMS wote wana maisha mazuri,na walio somea kayumba wote ni boda boda na wavuta bangi?
La msingi peleka mtoto shuleni inayo endana na kipato chako.
 
Kwahiyo kuchoma hela nyingi kwenye elimu ya bongo ni ujinga, labda kama utaenda chuo nje.
Familia zilizojipata watoto wao hawaendi UDSM wala UDOM.
Kuna wanaopeleka watoto India na Thailand huku wengine wenye uwezo zaidi na exposure watoto wao Uk na America.
Kwa hiyo Familia inaweza kuwa na Hela nyingi lakini hakuna mwenye Exposure. refeer watu wa Katoro.
 
Ebu naomba uniambe ni vitu gani cha ziada kinacho fundishwa EMS alafu kayumba hakifundishwi.
Kwa hiyo kwako ww wote walio somea EMS wote wana maisha mazuri,na walio somea kayumba wote ni boda boda na wavuta bangi?
La msingi peleka mtoto shuleni inayo endana na kipato chako.
Ni sawa na kudai anayelala kwenye nyumba nzuri na anayelala nyumba ya matope wote si cha msingi wanasinzia. Au anayeendesha let's say Harrier Anaconda 2022 kama private car na anayeendesha Passo old model wote si wana magari.

Kupelekea shule inayoendana na kipato chako haimaanishi ukikosa hicho kipato ukampeleka atakaposoma bure walimu ama wafundishe ama wauze kachori , basi udai bora nitamnunulia kiwanja. Huwezi shinda njaa ili ujenge. Utakufa uache hizo tofali.
 
Kwa Ilala kuna
Olympio
Diamond
Bunge
Zanaki
Kisutu

Kinondoni kuna
Mwenge
Michael Urio
Oysterbay
Makumbusho
Makongo
Ali Hassan Mwinyi

Zipo nyingi kwa hapa Dar. Kuanzia ada, chakula na usafiri, kwa ujumla kwa mwaka imezidi sana ni 1.2 ila mara nyingi inagotea laki 8,9 hadi 1m.
Ohh hapo sawa bei nafuu zimelingana na private za miaka yetu! Ngoja nifuatilie nimpeleke mtoto huku!
 
Ems inamjengeaje misingi mizuri ya maisha mtoto hali ya kuwa elimu na mtalala unao tolewa kule ni ule ule inayo tolewa kayumba ila Kwa lugha tofauti au ww kwako mtoto kujua kiingereza ndo msingi wa maisha?
,Elimu bora ni ile inayo patikana Internation school basi ,hizi Ems ni kayumba zilizo changamka.
Alafu kingine msingi mizuri wa maisha mtoto huwa hautoi shuleni bali huwa anautoa Kwa wazazi wake.
Wacha kujifariji mkuu,,elimu ya kayumba haiwezi kuwa sawa na English medium school,
Kuanzia ufundishaji hata mazingira ya shule.
Somesha mtoto shule wacha visingizio..
 
Back
Top Bottom