Ipi sahihi sana kati ya Kumsomesha mtoto msingi english medium ya ada 3m per year vs kumsomesha kayumba na kumnunulia kiwanja cha 3m kila mwaka?

Ipi sahihi sana kati ya Kumsomesha mtoto msingi english medium ya ada 3m per year vs kumsomesha kayumba na kumnunulia kiwanja cha 3m kila mwaka?

Wacha kujifariji mkuu,,elimu ya kayumba haiwezi kuwa sawa na English medium school,
Kuanzia ufundishaji hata mazingira ya shule.
Somesha mtoto shule wacha visingizio..
Lakini wakienda chuo wanaenda vyuo pamoja na wanasoma lecture hall Moja na lectures ni mmoja, facilitator ni mmoja na GPA sawa na Bado mtoto wa EMS atakuwa hajui haso akiingua kwenye maisha halisi
 
Ni sawa na kudai anayelala kwenye nyumba nzuri na anayelala nyumba ya matope wote si cha msingi wanasinzia. Au anayeendesha let's say Harrier Anaconda 2022 kama private car na anayeendesha Passo old model wote si wana magari.

Kupelekea shule inayoendana na kipato chako haimaanishi ukikosa hicho kipato ukampeleka atakaposoma bure walimu ama wafundishe ama wauze kachori , basi udai bora nitamnunulia kiwanja. Huwezi shinda njaa ili ujenge. Utakufa uache hizo tofali.
Mkuu ndo maana nimesema Kila mtu asomeshe mtoto kwenye shule inayo endana na uwezo wake wa kipato kama ilivyo kwenye kujenga nyumba,Kama gari na kadharika,na sio ujikaange Kwa mikopo Kwa kujidanganya kuwa huko EMS Kuna cha ziada zaidi ya kayumba.
Mtaala wa elimu ya Tz kiujumla hauna msaada wowote Kwa mtoto nje ya kuajiliwa ambazo na penyewe hizo ajira ni sawa na tone Moja la maji kwenye bahari.

Mfano mm sister za 3 wamesomea kayumba na walikuwa na akili za kawaida tu lakini Kwa Sasa wote wameajiliwa ,wawili ni manesi na mmoja ameajiliwa kwenye benki ya NMB.
Lakini baba mdogo ana watoto wake wawili mpacha mmoja wa kike na mwingine ni wakiume walikuwa vipanga na wote walisoma EMS na alikuwa ana lipa milioni 2 Kwa mwaka wamemaliza chuo lakini wapo nyumbani tu na hawajapata ajira ,wa kiume Sasa anapiga boda ,na wa kike anatembeza na kuuza jiusi ya kutengeneza,inamaana hawa watoto wasipo bahatika kupata ajira au wasipo jipambania Kwa kutumia akili za kuzaliwa maisha yao yatakuwa ya kubangaiza hivyo hivyo na baba mdogo aliwasomesha hao watoto Kwa shida sana.
 
Lakini walienda chuo wanaenda vyuo pamoja na wanasoma lecture hall Moja na lectures ni mmoja, facilitator ni mmoja na GPA sawa na Bado mtoto wa EMS atakuwa hajui haso akiingua kwenye maisha halisi
Ni kwl mkuu,,ila upeo wa mtoto aliyesoma kayumba ni tofauti na English medium..
Chukuwa mwanafunzi wa kayumba aliyemaliza std 7 umpambanishe na English medium STD 7 utaona tofauti..
 
Kumpeleka Mtoto shule yenye Ada kubwa au Shule ya Garama ni kupoteza tu hela, cz
mtoto atasoma atafika hadi Chuo then atamaliza Vizuri chuo, baada ya kumaliza chuo anakuwa
mzigo wako tena anashinda tu nyumbani hana cha kufanya Ajira hamna unaanza kuangaika
upya, Wakati Umetumia gharama nyingi hadi kumfikisha Chuo
Mzazi bora umsomeshe mtoto shule ya kawaida hela ya kumpeleka shule Yenye Ada kubwa
Umuwekee Mtaji kwenye account bank hili akija kumaliza chuo awe na kitu cha kufanya
Sio unatumia gharama kubwa kumsomesha then anakuja kuwa Jobless anaanza kukutegemea
kuanzia kula hadi kuvaa
Kwa sasa bora hiyo hela ya ada Uwekeze kwenye vitu vya maendeleo hata akija kumaliza ana
sehemu ya kujishikiza
Elimu ya bongo ishakuwa hovyo tu unatumia gharama kubwa then hamna faida yeyote, ndo
maana unakuta shule darasa zima wana div one ila wakimaliza chuo ni majobless kazi hakuna

Usisomeshe mtoto shule za gharama kwa matarajio kwamba
atapata ajira, utaishia kuumia tu

Maana Kumekuwa na tabia ya baadhi ya wazazi wakisomesha watoto wao shule za gharama za private
toka chekechea, msingi, o level na advance mpaka chuo kwa mategemeo kwamba watakuwa na
ajira zenye malipo ya juu, watoto wakimaliza chuo hawana ajira ama wanapata ajira zenye mishahara midogooo zinakuwa za chini,

kwao wazazi yanageuka kuwa maumivu:
 
Wacha kujifariji mkuu,,elimu ya kayumba haiwezi kuwa sawa na English medium school,
Kuanzia ufundishaji hata mazingira ya shule.
Somesha mtoto shule wacha visingizio..
Lakini baada ya kumaliza hayo masomo huko Em si ataenda UDOM akutane na walio somea kayumba,akisha maliza chuo yeye na walio somea kayumba watakutana Tamsemi wakipigana vikumbo kuhonga pesa na ngono ili wapate viajira uchwara vya mishaara ya laki 5.

Hapa kinacho angaliwa sio kusoma bali ni matokeo ya hiyo elimu ina msaada gani nje ya ajira.
Sijasema watu wasipeleke watoto Em maana hauwezi kumlazimisa mtu mwenye uwezo wa kununua V8 akanunue paso eti Kwa sababu yote ni magari.
Hivyo kila mtu anatakiwa kumsomesha mtoto kwenye shuleni inayo endana na kipato chake ,hakuna haja ya kujikaanga Kwa madeni na kuuza aset eti ukirazimisha kumsomesha mtoto Em huo ni ujua wa kiwango cha juu kama ela mpeleke Em,kama kipato chako cha kufunga huna haja ya kulazimisha maji kupanda mlima.
 
Hakuna kitu kizuri kama basic,,mtoto unapomuwekea msingi mzr wa elimu huko mbele kunakuwa kwepesi sn..
Mtoto wa English medium hata akienda form 1 shule za serikali bado anakuwa tofauti sn na wengine sababu tayari ana basic toka chini..
Kwanza atakuwa anaelewa anachofundishwa na sio kukariri.
-lugha atakuwa anajuwa vzr nk.
Kusoemesha mtoto kayumba ni sawa na kujenga nyumba ya ghorofa ila msingi wake umeweka udongo.

Usiifikirie sn pesa mkuu,,elimu ni msingi wa maisha ila sio elimu hyo ya kayumba..
Watu wanasomesha kayumba sababu hakuna jinsi ila sio elimu nzr Kwa mtoto..
Elimu gani wazazi mnachangia pesa ya mwalimu wa science? mathematics nk.
 
uandishi wako umebeba hisia na mawazo ya masikini

umeipa ukubwa sana hiyo 3M, kwa wanaosomesha hiyo 3M kwao ni ndogo kama ilivyo laki 3 yako.

kwahiyo, unavyowaza kwanini asinunue viwanja vya 3M ni sawa na maskini aliyechini yako anayewaza kwanini hiyo laki 3 na mahindi unayomsomeshea mtoto wako kayumba usinunulie mashamba vijijini huko kila mwaka.

Anyway, ninachotaka kusema ni kwamba level yako ya kiuchumi ndo inakusukuma kuona hivyo, ila ukifika level ya kushika milioni 5 na kuendelea kwa mwezi hakika utarudi kufuta huu uzi wako.
 
Dogo unaona Level ya kushika milioni 5 ni hela nyingi sana?

Wenzio hizo ni hela za kukaa kwenye simu za mkononi tu. Hata bank haziqualify kukaa.

IMG-20260925-WA0000.jpg

Tukikuonesha salio za bank huchelewi kutuita mafisadi
 
Kwa mtazamo wangu utofauti mkuu ni lugha ya kufundishia na usafi wa mazingira ya shule
Kwa mtazamo binafsi ada ya mtoto haitakaiwi kuzidi 8% ya kipato chako kwa mwaka (kama ni mtu unaejitafuta.

Mfano kwa mwaka unaingiza 12 Million basi ada pamoja na gharama zote za mtoto hazitakiwi kuzidi 1 million kwa mwaka.. Je unaweza kupata shule ya gharama hizo yenye sifa uzipendazo!?
 
Aina na Kiwango cha elimu unachompatia mtoto wako kiendane na malengo na uwezo wako.Kusomesha mtutu shule za English medium haimaanishi kwamba anapata elimu BORA.Kama uwezo upo Basi mpeleke mtutu asome mitaala ya kimataifa,akihitimu Mpeleke Nje ya nchi katika vyuo vya kimataifa akaifahamu na kuitwala dunia.

Iwapo sasa mtoto wako na wewe mwenyewe bado hamjafika level hiyo mpeleke tu shule ya kidumu.Hakuna kitu kibaya kama mtoto kuwa na Kiingereza kizuri halafu hana Maisha ya kueleweka wala connection za kueleweka.

NB:Mtoto kama ana bidii hata akisoma Kayumba anatoboa kabisa.Kuhusu kununua Ardhi nunue kadiri uwezavyo tena maeneo mkubwa kisha otesha miti ya kutosha kabisa.Hakuna kiwanda kinachozalisha ardhi mpaka hapo Elon Musk atakapoweza kutupeleka Mwezini na anga za mbali tukashike viwanja.
 
Jitahidi utafute medium school ya bei rahisi. Lugha ya malkia ni muhimu. Watanzania tunashindwa kushindana kimataifa kwa sababu ya kutokujua lugha ya malkia.
Mimi ni miongoni mwa watanzania wachache tunaoweza kuongea kiingereza dakika 3 mfululizo bila kuchapia.
 
Kwa mtazamo binafsi ada ya mtoto haitakaiwi kuzidi 0.8% ya kipato chako kwa mwaka (kama ni mtu unaejitafuta.

Mfano kwa mwaka unaingiza 12 Million basi ada pamoja na gharama zote za mtoto hazitakiwi kuzidi 1 million kwa mwaka.. Je unaweza kupata shule ya gharama hizo yenye sifa uzipendazo!?

0.8% ya milioni 12 ni 96,000 tu. Haifiki hata laki moja.

Hivyo maana yake mtu mwenye kipato cha milioni 12 kwa mwaka anapaswa atumie chini ya laki moja kwenye kusomesha mtoto
 
Back
Top Bottom