Ng'wanamalundi
JF-Expert Member
- Feb 4, 2008
- 1,203
- 1,422
Wivu gani? Kama ni wivu wangewakataza kwenda huko. Wanachofanya ni kuwaambia kama umeamua kwenda huko, basi nenda moja kwa moja. Usije huku kupokea Sakramenti. Wivu unakujaje hapa?RC wana wivu. Jamaa alijaza nyomi ya hatari.
Labda ni small house ya paroko lazima ashtaki.Daah so sad kanisa limeanza kujishtukia. Ila wale waumini viherehere kila jambo wanaenda kushtaki kwa paroko sijui huwa wanawaza nini
Hawazuiwa kwenda kumuabudu Mungu, wameambiwa hawatapewa ekaristi takatifu hadi waungame.Unaanzaje kumzuia mtu kumuabudu MUNGU?
He mbona tunaenda kwa waganga na walozi Kisha tunarudi kanisani hatufukuzwi?
Kanisa ni kwa wale tuliowaovu sio wasafi, hata YESU alikuja kwa ajili ya waovu
Umeshasikia mtu kazuiwa kumwabudu MUNGU kisa alifumaniwa?
Kwani wasiponizika inasaidia nini wakati tayari sipo duniani?kwanza kuzikwa hakuna umuhimu wowote kuhusu kule uendapo kinachoangaliwa matendo yako ulipokuwa hai,wakristo tuamke.Na RC HUWA hawatanii utasikia na ukifa hatukuziki hata kama mkisafirisha hatuwapi barua ya utambulisho huko muendako.
Hata hizi zetu za kuabudu mizimu nazo zina shida sana.Hizi Imani za kuletewa zina shida aisee
Ndio hapo sasa,mbona hatujaona matamkoNa wanaokwenda kwa waganga inakuaje
Eti kuwaponya wagonjwa ni mafundisho potofu?! Inashangaza sana aiseeNimeshangaa juu ya tamko lao kuhusu uponyaji wa magojwa, nanukuu:
"Tunakemea na kubeza mafundisho potofu ya uwongo (bandia) kama vile ...kuwaponya wagonjwa, ..."
Yesu mwenyewe alisema:
Yohana 14:12
Amin, amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya, kwa kuwa mimi naenda kwa Baba.
Maana ake kama vile Yesu alivyoponya magonjwa, na wafuasi wake wanaponya magonjwa, nk. Sijajua wanatumia maandiko gani kwa hili!!!
Mwamposa pia Ni mganga wa kienyeji anayevaa SutiUnaanzaje kumzuia mtu kumuabudu MUNGU?
He mbona tunaenda kwa waganga na walozi Kisha tunarudi kanisani hatufukuzwi?
Kanisa ni kwa wale tuliowaovu sio wasafi, hata YESU alikuja kwa ajili ya waovu
Umeshasikia mtu kazuiwa kumwabudu MUNGU kisa alifumaniwa?
Kuna dogo alinyang'anywa Bajaji na bosi wake. Amekaa wiki mbili hana KAZI. Siku Mwamposa ametua Iringa dogo akaenda kuombewa. Ametoka tu kuombewa akapigiwa simu na bosi njoo uchukue Bajaji. Dogo alinisimulia huku anatoa machozi ya furaha. MTU kama HUYO ukimwambia Mwamposa tapeli atakuelewa?Mwamposa alisimamisha mkoa wote pale iringa,hakukua na shughuli yoyote iliyoendelea kwa siku 3
Kazi zinapatikana kwa kupeleka CV, Sio kuombewaKkkkk Mbona Mwamposa HUWA anaombea watu wapate KAZI? Fatili Channel take ya Arise and Shine TV.
INATEGEMEA NA IMANI YAKO.Kazi zinapatikana kwa kupeleka CV, Sio kuombewa
UMEONGEA UKWELI WA MUNGU.Huo ni ushetani sasa
Asante mkuu,RC ndivyo tulivyo.Halafu kwenye ule mkanyagano uliowahi kusababisha vifo vya waumini; kwa harufu ya sasa inaonekana kama zilikuwa ni hujuma zilizofanywa makusudi ili kuichonganisha Serikali ya kipindi hicho na taasisi za dini. Ilitarajiwa kuwa hayati JPM angechukua hatua kali dhidi ya tukio hilo, halafu sasa waliokuwa kazini wangeitumia fursa hiyo ili kuchochea moto upande mwingine ule wa pili.
Mwamposa amekuwa akifanya haya matamasha siku zote na mara zote waumini wake wamekuwa wakiyafanya na kuondoka salama, iweje kwenye tamasha hilo tu watu wakanyagane hadi kufikia kiwango cha waumini hao kupoteza maisha na kwa wingi kiasi hicho? Kwa tukio hili mtumishi huyu inabidi aliangalie kwa jicho la pili
Kwa hili la RC, ni kawaida kabisa hamna cha ajabu kwa sababu RC wenyewe wako very strict na ni watu wa principles tu siku zote. Madhahabu ya Bwana kwenye Kanisa la RC inaheshimika nadhani kuzidi makanisa yote ya Kikiristo; kwa maana kuwa halipo kanisa la kikiristo linaloheshimu madhabahu ya Bwana, kama Kanisa la RC. Nilizaliwa na wazazai wa RC, nikabatizwa RC, nikapata kipaimara RC. Nawajua RC in and out!
Ni sawa ila kwani huyo mwamposa na masangoma wana tofauti gan?Mwamposa pia Ni mganga wa kienyeji anayevaa Suti
Unaamini alipata bajaj kwasababu ya mwamposa?Kuna dogo alinyang'anywa Bajaji na bosi wake. Amekaa wiki mbili hana KAZI. Siku Mwamposa ametua Iringa dogo akaenda kuombewa. Ametoka tu kuombewa akapigiwa simu na bosi njoo uchukue Bajaji. Dogo alinisimulia huku anatoa machozi ya furaha. MTU kama HUYO ukimwambia Mwamposa tapeli atakuelewa?
Kwa sababu MUNGU alijibu maombi yake kulingana na imani yake.Unaamini alipata bajaj kwasababu ya mwamposa?