Israel na Marekani zaishambulia Iran. Serikali ya Israel yatangaza hali ya hatari

Huelewi chochote juhusu mchina nakumbia China hawezi kufanya hicho kitu na hajawahi msadia msaidizi wake hata mmoja.
Nikukumbushe aliyosema China na akafanya.
-2018 China ilitangaza kusimamisha uundaji wa iphone na ikafanya.
-China ilitangaza kuwanyima USA rare earth metals na ikafanya.
-China ilitangaza kuongeza ushuru mara 2 kwa USA na ikafanya.

Mida mingine usiwe UNAROPOKWA KAMA MLEVI.
Aliyeongea ni WAZIRI WA MAMBO YA NJE,yule haropoki bali kamati inakaa na kupitisha maamuzi ndio yeye analitamka.

-Hadi sasa Iran inatumia satellite za China kushambulia kambi za USA na Israel.
-China imetoa radar na ADS na makombora kwa Iran,je huo sio msaada!?

Muda mwingine embu tumia akili yako hata kidogo.
 
Iran ina utajiri wa mafuta na gas...
Ila Iran anachofanya sasa ni kuikanya Israel isije kuleta tena mazoea.
There will be no Iran as we know baada ya mgogoro huu na Israel Hegemony ndio itakuwepo middle East.

This war is Israel master class.

Mataifa ya Kiarabu hayakuwahi kujiandaa na vita.

Israel na Marekani walikuwa wanaitaka hii vita sana.

Jiulize kwa nini wanashambulia taasisi za serikali kwanza
 
Serikali ya Iran isha anguka ?
 
Gaza imewashinda vita ya miaka mitatu, wataiweza Iran?
Hezbollah ya Lebanon imewashinda wataiweza Iran?
Houthi ya Yemen imewashinda wataiweza Iran?
 
We jamaa unapenda kuongea hisia kuliko uhalisia.
Be realistic and clinical atleast once.

Israel unayoisemea viongozi wakubwa wote wamekimbilia Ujerumani.
Iran uongozi wake bado upo intact.
Ingekua kushambulia taasisi za serikali ndio kuidhoofisha basi wangeshadhoofu kabla.

Nchi za kiarabu ulizozitaja ZOTE raia wanaonekana kufurahia anachofanya Iran. Na zikizembea tawala zao zitaangushwa mfano mzuri BAHRAIN. Raia wako road sasa hivi wanaleta fujo kwa utawala.
 
Huyo jamaa ukimsoma maelezo yake unaweza ukacheka.
Yani yupo kihisia zaidi na wala sio kiuhalisia.
Hii vita imejaa ushabiki maandazi,humu ndani nisha uliza kosa la Iran ni lipi ? Hakuna team Israel na US walio leta hoja zenye mashiko zaidi ya ushabiki wa udini nk watasema Iran inatoa msaada Kwa Makundi pale Middle East,sasa unajiuliza yule gaidi ambaye sasa ni rais wa Syria msaada wa kumuangusha Asad ,ulitoka Iran ?
 
Kuna ripoti zinasema Iran imeshambulia kambi ya USA nchini Uturuki.
Ndio maana Pentagon na wanachama wa Trump nasikia wanajiuliza huko nani yupo nyuma ya hayo mashambulizi?
Halafu nionavyo unaweza kuta hata hao waarabu wamemchoka Israel, maana mgogoro wa Gaza wengi wao walikasirishwa sana ikiwemo Qatar.. jamaa waliua watoto haijapata kuonekana.

Na inaonekana gulf state wamegawanyika, kuna ambao wanabariki chini chini Iran itwange kambi za US huku wakijitia wanachukizwa, kuna ambao hawataki..

Maana wameshamaliza mfumo wa integrated air defense, sasa Israel inabaki uchi, hakuna early warning, na hao waarabu wanataka Israel ichapike.
 
Vita vilivyopita walitarget Israel Tu yakaisha, sasa hivi Nchi zote za Gulf, Hadi Cyprus wamefika, Watu wamepiga hotel yoyote Ile inayohifadhi CIA na Mossad, mpaka data Centre za Amazon zimeliwa. Hapo Bahrain pia ni Shia Ila kumetandikwa vibaya mno, na hawapigi bomu moja Tu wakaacha, moshi ukipungua Tu kidogo wanatandika jengine, hio kambi ya Bahrain kwa siku inapigwa mara kibao.
 
Ina maana muajemi yeye hataki kuona moshi unapungua hayo maeneo...
 
Iran sasa ndo mtaalam wa ku mass produce hayo madude, makombora yake bei rahisi mno, mwenyewe ashakwambia ana Stock za miaka 2 akiendelea na Dozi kama hii kila siku.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…