Naona unajitahidi kutafuta faraja. Kwahio wewe unafikiri USA hawajui capacity ya Iran kiasi wamchokoze bila enough weapons? Yaani wachambuzi wa Tz mnajua kuliko walioanzisha vita.
Lakini mkuu kuna ukweli, PAC-3 interceptor moja ina cost mpaka $5 Million.
Inawezekana either wameona PAC 3 interceptor zinaelekea kuisha , ama wameona wabakize zilizobakia kwa ajili ya emergency.
Maana PAC-3 ni noma hio, ipo very advanced, hio ni hit to kill, ina maana inagona target direct na ina mlipuko kidogo, inafanya kinetic impact.
Ikataka kuangusha missile ni mpaka igonge hio missile na kuiharibu, ni utaalamu wa hali ya juu sana huo ambapo hata Iron dome haipo hivyo.
Iron dome yenyewe huwa ikakaribia target, inajilipua na kupelekea target kuharibika, interceptor ya iron dome ikikaribia kabisa target ina sensor, inajilipua na missile inaharibiwa. Lakini PAC-3 ni mpaka igonge missiles physically.
Ni kama mtu akulenge na manati, kipindi jiwe linakuja na wewe ulenge na manati ili kuzuia jiwe linalokuja, you can imagine unahitaji usahihi wa kiasi gani na shabaha ya kiasi gani. Hio ndio Patriot PAC-3. Iron dome haifikii hapo. Ina precision guidance system ya hali ya juu sana.
PAC-2 yenyewe ndio inalipuka karibu na target kama ilivyo iron dome.
Kwenye kulenga makombora yenye kasi ya juu sana PAC-3 sio mchezo.
Na Iran hivi sasa lengo lake kusababisha interceptor wanaishiwa, maana hata PAC-2 interceptor bei yake haijapoa ni $1 Million - 2 million usd.