Hoja nzuri, lakini pia US na Israel wamekutana kila mmoja akiwa na goals zake halafu wakajikuta njia ya kupita kufikia hizo goals ni moja, hivyo wanashirikiana. Na pia wakitimiza malengo hayo wote watakuwa katika nafasi nzuri sababu kila mmoja yupo vizuri tokana na ushirikiano wao wa ki uchumi, kijeshi na ki siasa.
Nikiwa na maana ya kwamba Israel akiwa vizuri kwenye nyanja zote, US hawezi hangaika kupoteza rasilimali zake ili kumsaidia.
Israel inataka sana ukiranja wa kikanda mashariki ya kati na nchi inayoinyima amani ni Iran, huku US akiwa na malengo zaidi ya ushindani wa kiuchumi. Na wote wanajikuta ili wafanikishe hayo ni kuivamia Iran kwa nguvu zao zote. Wote mchawi wao ni Iran, syndicate imesoma waivamie Iran.
Japo ni kweli US huwa anamsikiliza Israel, naamini US isingekuwa na maslahi yeyote ya kiuchumi kwa Iran, nadhani hata kama Israel ingepambana na Iran, US ingetoa msaada wa silaha na baadae kuwakalisha kusuluhisha na si kuingia mzima mzima kama hivi labda tu endapo ingeonekana Israel inapigwa imezidiwa.
Hivyo hawa jamaa wanachofanya ni uonevu, na China atakuwa mpuuzi akikaa kimya, Russia ndio kabisa wana akili za kutengeneza silaha na kupigana vita, lakini uwezo wa kiushawishi, siasa na hata utamaduni hao jamaa wana zero. Na hilo ndilo lilivunja USSR. Na hata leo hii wanazidiwa kete na EU na US.
Russia imesinzia, wakati wa USSR walipoteza wanasayansi vichwa, wakakimbilia