Trump na Europe pamoja na washirika wao wote ni wajanja sana, wanajifanya kama wamegombana, kumbe lao moja.
Hii vita ya tatu ya dunia wanaiendesha ki mkakati sana.
from no where:
1)Trump akaanza kuwatusi viongozi wa umoja wa ulaya
2)Trump anaitaka Green land
3)Mafaili ya Epstein(naskia putin ana picha mjongeo za trump na vibinti.)
4)Wahamiaji wakala deportation
Pamoja na mengine mengi hayatokei kwa bahati mbaya.
hizo ni geresha, kuna watu wanadanganywa na wanadanganyika ni urusi, China, Iran, North Korea.
Muhindi yeye ni double agent ndio maana umoja wa ulaya baada ya kujifanya wamegombana na trump wakampa dili kubwa la kupeleka wataalamu wengi umoja wa ulaya yote.
unaambiwa hili ni bonge moja la dili India kupata.
View: https://youtube.com/shorts/vGC0bhSMI88?si=kDGwebVTGzQHTjYj.
Sasa zamu ya muiran imefika, mwanzo walitaka kuanza nae, alivyojibu mapigo wakaona chizi mabomu huyu atatumaliza ngoja tujipange.
Us ili kujifanya kaamulia ugomvi akashambulia vinu vya nyukria, haikuwa bahati mbaya ile ilikua ni tactic ya kumpunguza nguvu Iran ili ikija phase ya pili(hii iliyoanza leo) asiwe na nguvu hata kama kaanza kutengeneza vingine.
Phase ya pili marekani katika kupasha pasha kabla ya mechi, akaamua kumchukua moduro ghetto kwake.
Na huu ni ujumbe kwa nchi ndogo ndogo zilizopo BRICS kama vile South Africa, Brazil kwamba nyie hakuna haja ya vita, natuma kikosi kinakuchukua(kwenye kundi hili ndio hata sisi tumo)
Sasa mechi imeanza leo baada ya maandamano kufeli.
Iran atapigwa vizuri tu, na atachagua mwenyewe akimbilie Russia kama Al asad au ajifiche mpaka atakapofikiwa
Hakuna China wala Russia atakaejaribu kukinga kifua zaidi ya maneno
China kawekewa Taiwan inamtazama vizuri tu.
Kiduku akijifanya hana akili nzuri kuna South Korea
Mrusi ambae alikua na afadhali, kasogezewa fupa lisiloisha Ukraine kila aking'ata wapi na wenzake China na North Korea wanajifunza kutokana na makosa ya Swahiba wao Russia.
Wakimalizana na Iran nadhani kituo kinachofuata atakua kiduku, kiduku akiguswa najua China na Russia wataingilia, na hapo watakua wamechelewa.
Umoja wa ulaya utaungana na Us