Iran siku ya jana na leo kafanya matusi sana dhidi ya intelligence ya Trump!
Kwanini?
Eeeeh bwana eeeh, jana Israel ilifanya shambulizi dhidi ya mitambo ya kuzalisha nishati ya gesi katika taifa la Iran.
Iran wala hawakulialia, ila walikuja na tangazo kwamba, miundombinu ya nishati ya Israel na washirika wote wa USA hapo mashariki ya kati itashambuliwa na jeshi la Iran.
Oyaaaah, Mungu si Athumani, jioni ikaingia, Waajemi wakaanza kutimiza ahadi waliyotoa.
Mitambo ya mafuta Kuwait ikapigwa, mitambo ya mafuta Saudi Arabia ikapigwa, Qatar nao hawajaachwa, mitambo ya nishati ya gesi imebondwa, leo wamemaliza kwa kuwatembelea Wazayuni, mitambo ya mafuta ya Haifa imelambishwa cheche.
Bila kusahau, leo ndege ya kivita inayopambwa sana na mashabiki wa USA, F-35 ilitaka kutamba kwenye anga la Iran, ikapapaswa.
Haya yote ni matusi, jeshi ambalo Trump anasema amelimaliza nguvu kwa asilimia 100 linatangaza kufanya mashambulizi maeneo specific, tena hayo maeneo yana ulinzi wa kutisha wa anga, bila kupepesa linafanya kweli mashambulizi na kuzifikia target, oyaaah hapa Trump ameyakanyaga.