Israel na Marekani zaishambulia Iran. Serikali ya Israel yatangaza hali ya hatari

Kwa kuongezea kidogo hapo kwamba marekani hadhuriki:
  • Anaathirika kwa kupunguza mzunguko na mahitaji ya dollar kwenye soko la dunia maana Iran anatoza kwa Yuan pale Hormuz. Na pia mafuta toka Ghuba yanauzwa kwa dollar, Hivyo Marekani anaumia
  • Kudhibitiwa kwa Hormuz na Iran, kuna muathiri Marekani kiushawishi duniani maana nchi nyingi zitaanza kutafuta weak points za Marekani na kujaribu kumtunia uko tuendako
  • Kufungwa kwa Hormuz kunatoa nafasi kwa Russia kufanya biashara ya mafuta na gesi bila kutumia nguvu kubwa tofauti na malengo ya marekani hapo awali
  • Mwisho wa siku Marekani atapoteza washirika wengi sana pale middle east maana kwa vita hii maeonyesha sio mtu wa kumtegemea kwenye suala la ulinzi na usalama wao
 
Kusema kweli sijui watu wanashindwaje kuona pattern ya michezo ya marekani na Israel kwa mataifa mengine yanayoonekana hayaendani na interest zao! Imefanyika HIVI Syria, Iraq, Yeemen, Lebanon, Somalia, Sudan na sasa wanaleta ujanja ule ule Iran lakini watu bado wanawakenulia meno hawa mashetani.
Hata kama watataka kutuaminisha kwa kutumia vifungu vya maandiko ya kwenye biblia kuwa Palestina ni ardhi yao ya ahadi, (ingawa hii nadharia inatia shaka sana) basi tujiulize Lebanon pamoja na Yemen wanataka nini?
 
Mnatumia kusafirisha makombora Mossad washatoa taarifa, chaguo ni lenu msimamishe mlanbwe mitama
Kwani si Trump alituambia kuwa wameteketeza makombora yote sasa hayo yanayo safirishwa ni yapi?
Mkubali mkatae hii vita walio vianzisha wamepoteza muelekeo kwa sasa wanafanya mambo kwa pupa kujaribu kupunguza aibu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…