Israel na Marekani zaishambulia Iran. Serikali ya Israel yatangaza hali ya hatari

Ha ha ha mkuu unafurahisha sana. Makao makuu ya jeshi yameisha huko Iran. Ndege za Israel zinatamba Tehran inakuwaje?
 
Kuua makamanda wakuu ndio kushinda vita??
2006 IDF iliua makamanda wakuu wote wa Hizbollah lakini bado Hizbollah imeshinda vita dhidi ya Israel.

-Ameshateuliwa kiongozi mpya Alireza Arafi. Iran ina mkakati mrefu wa succession sio nyepesi kama unavyodhani.
Ayatollah mpya katangazwa na msimamo wake ni ule ule.
Iran serikali yake inaongozwa KIITIKADI. Nadhani hili wengi hamlijui.
 

Sina tatizo na khamenei.
Hapa tunazungumzia Suala la Iran anatoboa au hatoboi.

Vita inakanuni zake.
Na Khamenei na wenzake wote wanazijua.

Iran wanajua fika hawana uwezo wa kumshinda Marekani. Hilo lipo wazi kimahesabu.

Ili Iran ashinda lazima apate washirika wakweli kabisa ili kumpa nguvu na ku share cost.

Ndege za Israel kama zinazurura hovyo juu ya anga la Iran unafikiri kuna nini hapo.

Yaani Israel wakisema wapige kipigo cha hasira kama wehu. Ni Siku tatu tuu kwa kutumia ndege kazi itakuwa imeisha.

Ila Hawawezi kufanya hivyo kwa sababu pia vita ni suala la kisaikolojia. Wanapiga kimkakati na pia kuwashirikisha na kuwashawishi raia wa IRAN wajiunge kuungausha utawala wa Ayatollah.
Lengo unajua ni nini?
 
Hizo bases za US zilizopigwa zilikuwa zina radars na vyombo ambapo vilitumika kutoa early warning hadi Israel.
Walitengeneza Integrated Air and Missile Defense (IAMD), Iran ikirusha makombora, tayari Qatar inaona, Kuwait, Bahrain n.k... hivyo wanafanya radar data sharing ama wana link na radar za Israel, hivyo Israel wanapata taarifa kuna missiles zipo njiani.

Kwa jinsi hali ilivyo, Israel itaharibiwa vibaya, na Iran imeamua kufa na Israel, hata waarabu wengi hapo wana kinyongo kuhusu Gaza bado, hata Qatar watakaa kimya.

Ndio maana Iran kwa hasira anatandika hizo kambi na anapiga si mchezo, maana hizo nchi walifahamu wanatumika na US na walikaa kimya.

Tel Aviv inaharibiwa vibaya kabla hata masaa 48 hayajafika, ni majanga makubwa.
 
Mwanzo walikuwa wanasema hawezi kufikiwa sasa kadikiwa yeye na wakuu wengine sio deal.
 
Na pia Israel ndo kamuua
 
Bro sasa unaongea hisia badala ya uhalisia.
Nakuacha na facts chache pia sitahitaji kujadiliana na wewe maana uko kihisia zaidi.
1.2006 Israel iliua makamanda wakuu wote wa hizbollah,ila Hizbollah ilifanikiwa kuwapiga Israel na kuwapokonya Bint jubeir.
2.1980 hadi 1988 Iran ilivamiwa na Iraq ikiwa na usaidizi wa Marekani viongozi wengi wa Iran waliuawa,Iran iliteua uongozi mpya ikapambana na kushinda vita.
3.2025 June Israel iliua asilimia 90 ya top millitary commanders na viongozi wakuu ila still Iran iliteua viongozi wapya na ikapambana na Israel na aliyeomba vita iishe ni Israel.

SIONGEI MAHABA KAMA WEWE KAA PEMBENI NIJADILI NA WANAOJIELEWA.
 
Mkuu unafuatilia kinachoendelea Tel Aviv, Tel Aviv inawaka moto.....

Kwa haya mashambulizi ikipita siku 10, Tel Aviv inakuwa Gaza..
Nafuatilia naona Iran anavyorusha missile hovyo pande zote. Anaharibu apartments,airports. Mwenzio analenga vitu muhimu vya kivita.
 
Netanyahu alishawahi sema yuko tayari kwa Israel kushambuliwa imradi tu Uongozi wa Iran ubadilishwe
 
Nafuatilia naona Iran anavyorusha missile hovyo pande zote. Anaharibu apartments,airports. Mwenzio analenga vitu muhimu vya kivita.
Kama analenga vitu muhimu vya kivita, kwanini asilenge huko Iran wanaporushia hayo makombora?
Israel kuna sheria kali sana sasa ya kudhibiti taarifa za kivita.. wananchi wanakamatwa na polisi..
 
Mwanzo walikuwa wanasema hawezi kufikiwa sasa kadikiwa yeye na wakuu wengine sio deal.

Aiseeh! Yaani ni aibu Sana.

Hapo watarusha makombora hovyohovyo bila mipango.
Ni kama mtu aje kwako akupige wewe Baba WA familia. Alafu watoto wako wakarushe mawe nyumbani kwako wakapasue vioo vya dirisha, au gari, wachome shamba lako.

Bado haiondoi ukweli kuwa Baba wa Familia amepigwa na familia yenu imepigwa.

Tatizo wengi hawajui nini maana ya vita.
Na kwenye vita kuna target ambazo zikipigwa itadaiwa umepigwa. Target ya Kwanza ni kiongozi mkuu na viongozi wa majeshi.
Simple.
 
Unajua wewe kwenye haya masuala ufahamu wako ni mdogo.

Kwa ujumla vita hupimwa kwa njia mbili kuu: Mosi, kwa malengo yake kutimia, na hapa huwa kwa mtizamo wa kisiasa au kijeshi. Mara nyingi kwa msingi huu vita hupimwa kwa; Je, malengo ya kisiasa yalifikiwa? Je, eneo au mamlaka waliyoyahitaji yalipatikana? Je, adui alisalimu amri?

Kwa mfano, katika WW2, washirika walihesabiwa washindi waliangusha utawala wa Hitler na Japan, hivyo kufanikisha lengo lao la kumwangusha. Katika kumwangusha huku walikufa sanaaa. Lakini lengo la vita lilitimia.

Wewe unachukulia kuuawa kwa kiongozi mkubwa wa nchi au wakubwa jeshini ni kama ushindi, nakushangaa! kwa sababu wewe unajiita mtu wa fasihi halafu historia hujui hali ya kuwa historia imethibitisha kuwa ukiua kiongozi ni tukio la kimkakati, siyo hitimisho la vita.

Kuuliwa kwa Ayatollah kwa mbinu za kijeshi inaitwa "decapitation". Lengo ni kuvuruga amri na udhibiti (command and control), kushusha morali ya wanajeshi, kusababisha mgawanyiko wa ndani na kuharakisha kusalimu amri.

Lakini inafanya kazi lini? Mbinu hii huwa ina mafanikio zaidi kama mfumo wa adui unategemea sana mtu mmoja (utawala wa mtu mmoja). Aidha, ikiwa hakuna mpango madhubuti wa kurithisha uongozi. Halikadhalika, jeshi la adui halina muundo thabiti.

Hii mbinu huwa inashindwa ikiwa kama; Mosi, kuna safu ya uongozi iliyoaandaliwa. Pili, Itikadi ni kali kuliko mtu binafsi. Tatu, Kifo cha kiongozi kinageuzwa propaganda ya kuhamasisha zaidi vita. Vita vya kisasa ni vya kimfumo, si mtu au watu pekee.

Inakubidi ufahamu vilevile tactical victory na strategic victory. Tactical victory ni ushindi wa kimbinu, ushindi wa eneo eneo dogo, muda mfupi. Tactical victory inaweza kuonekana kubwa, lakini isibadilishe mwelekeo wa vita. Strategic victory huu ni ushindi unaobadilisha mwelekeo mzima wa vita au kufanikisha malengo ya kisiasa ya vita.

Kilichofanyika kwa Iran ni tactical victory, ambayo pia ni decapitation strategy; yaani kukata kichwa cha uongozi ili kuvuruga mfumo wa adui. Kwa bahati mbaya mfumo wa Iran ni tofauti. Njia pekee inayofaa kwa kuung'oa ni kuingiza askari wa mapigano ya ardhini. Mbali na hapo hakuna chochote kitakachofanyika zaidi ya Marekani na Israel kufanya operesheni maalumu na kisha mchezo umeisha.
 

Sasa unafikiri Trump anapowaambia wananchi wachukue nchi yao unafikiri anamaanisha nini?
 
mashehe ubwabwa kwa kujiamini mpo vizuri na hicho ndicho kinachowaponza
 
Jamaa mnajua kunifariji kweli nyie. Aiseeeee
 
We jamaa bhana, video ya kwanza kabisa hapo ni IRAN, tena ni Tehran mji wao mkubwa
Acha kudanganya watu Kuanzia Iraq, Iran, Pakistan Hadi India kuna maandamano makubwa kumlilia Ayatollah.

Hii Iran, unambie kuna kiumbe kilitoka nje hapa kupinga? Tena ndani ya Iran utembee na bendera ya Israel? Kadanganye chekechea huko.

Your browser is not able to display this video.
 
Leta habari za uwakika hapa usite propaganda, sema wamekufa askari wangapi. Yaani mtu anakuja kukuzingira kwako na mameli ya kivita na anauwa kiongizi mkuu nchi na viongizi top wa ulinzi unashindwa kushambulia meli unaenda kupiga kambi ambazo makimbira enyewe wana ya intersect.
 
Mkuu unafuatilia kinachoendelea Tel Aviv, Tel Aviv inawaka moto.....

Kwa haya mashambulizi ikipita siku 10, Tel Aviv inakuwa Gaza..
iran anashambulia apartments tel aviv na hoteli za dubai.. yeye anachapwa strategic sites
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…