..Nadhani uko kinadharia zaidi.
..You are dealing with human beings, not stones.
..kwamba watu wana kumbukumbu, wana hisia, na wana akili zinazofanya tafakuri.
..Wanamkumbuka Dr.Bashiru jinsi alivyokuwa fedhuli na mwenye kiburi cha madaraka wakati akiwa Katibu Mkuu wa Ccm.
..Leo amefikwa na nini kiasi cha kiasi cha kuanza kuwazodoa watawala, na kutetea wanyonge?
..Je, tumuamini tu bila ya kumdadisi? Je, atetewe tu bila kwanza kukiri makosa yake, na kuwaomba radhi waliodhulumiwa wakati akiwa sehemu ya genge la watawala?
..Kuielewa hoja yangu labda nitoe mfano huu mdogo. Hivi mtu ambaye anajulikana kwa kumkashifu Mtume Muhammad, je ana uhalali siku yoyote ile atakayoamua aingie Msikitini?
..Je, waumini hawana haki ya kumhoji kama ame Silimu? Je, hatakiwi kuulizwa kama ametawadha kabla hajaingia Msikitini? Je, aachwe tu aingie Msikitini na viatu?
..Narudia tena, Dr.Bashiru atubu, aombe radhi, ajitenge na ufedhuli na unyanyasaji wa awamu ya 5. Baada ya hapo atakuwa na uhalali wa kutetea uhuru wa maoni.