Januari Makamba adai uchaguzi wa 2020 ulitugawa, watu walifungwa, walinyang'anywa pesa, na waliharibiwa biashara zao

Januari Makamba adai uchaguzi wa 2020 ulitugawa, watu walifungwa, walinyang'anywa pesa, na waliharibiwa biashara zao

Naona Wahusika wakubwa ndani ya Serikali wameanza kusema wenyewe juu ya kilichotokea wakati wa Uchaguzi wa 2020.Mh Makamba akiwa Italy akiongea na Watanzania amemwaga Mchele wote jinsi Uchaguzi wa 2020 Chini ya HAYATI MAGUFULI ulivyokuwa na Watu Walivyoumizwa na kudhulumiwa ili MAGUFULI ASHINDE.
Asante Makamba kwa taarifa hiyo tuna imani na Aliyempiga RISASI Mwanasiasa TUNDU LISSU tutamjua tu.Mwendazake Alipanda MBEGU ya CHUKI na AMEIVUNA
MUNGU siku zote ni hataki WATU WABAYA MUNGU ni FUNDI ameumaliza Mchezo kati ya Watanzania na MWENDAZAKE. Pumzika Mwendazake Umevuna ulichokipanda
uungwana ni maneno na matendo 🐒

ni umakini na ujasiri wa kiwango cha juu sana kwa taasisi na watu wake kujitathmini, kujisahihisha, kujirekebisha, kuziba nyufa, kuondoa kazoro na kuja na mawazo mapya, mipango mikakati mipya na kusonga mbele vizuri zaidi, kwa umahiri zaidi na kwa uhakika zaidi 🐒

Mungu Ibariki Tanzania
Tuepushe na Roho kujipa umuhimu zaidi ya wengine na kujihesabia haki 🐒
 
Naomba nisimuwekee maneno Makamba.

Maneno aliyoyazungumza ni tuhuma nzito kwa utawala wa Rais Magufuli.
Sasa kwani si Samia yupo? Majaliwa yupo? Mwigulu yupo? Aliyekufa ni mmoja tuu lakini wote wapo sasa hapa wana mdanganya nani? Na nyie mnajifariji kwa kupenda kusikia wanasema bila matendo? Hivi walio haribu uchaguzi si wapo? Nani kafa zaidi ya Magufuli?
Kwanini Sasa wasikubali Tume huru ya Uchaguzi kuvunja mzizi wa fitina?
 
1. Je, wanasiasa walifungwa?

2.Je, kuna walionyang'anywa fedha?

3. Je, kuna walioharibiwa biashara zao?

4. Je, shughuli za vyama vya siasa zilizuiliwa?

5. Je, uchaguzi haukuwa na makandokando?
Exactly!
Badala ya kumshambulia marope ni vzr kwanza kujibu hoja zake
 
Kwani hajulikani au wewe ndiye usiyemjua!!?
Kinachosubiriwa ni kuanza kutajana wao wenyewe.
 
Stieggler Ile pale 2225MW - tunaweza kusahau kabisa shida ya umeme tukitumia akili.
Tanzania ya viwanda na kuhamasisha uwekezaji wa viwanda - Sasa hivi wote tumerudi kwenye uchuuzi.
Daraja la juu pale busisi - Mwanza.
Ujenzi wa reli ya kisasa Dar - Mwanza.
Kuifanya shillingi kuwa stable - Sasa hivi shillingi Kila siku inayumba.
Kuleta nidhamu ya utendaji serikali.
Kulifufua shirika la ndege lililokufa.
Kuboresha usafiri ziwa Victoria.
Kufanya watu waiogope na kuiheshimu dola.
Ujenzi wa miundombinu Kila Kona ya nchi.
Ujenzi wa masoko ya kisasa maeneo mbalimbali.
Ujenzi wa hospitali za rufaa Kila mkoa.
Kuboresha huduma za afya Kwa kununua vifaa vya kisasa (VP MRI nzima pale Muhimbili?).
Kujenga smelter ya Dhahabu pale Mwanza.
BOT kuanza kununua dhahabu na kuweka reserve ( Vipi ile reserve bado IPO?).
Kudhibiti utoroshwaji wa madini.
Kuruhusu wachimbaji wadogo wadogo kupewa maeneo na kuchimba ( Sasa magiants wameanza kuhodhi maeneo na kufanya udalali Kwa Wazungu na wachina).
Kudhibiti matumizi ya hovyo ya serikali ( watu wanapishana angani tu Sasa hivi, na mijengo wananunua).

HAYO YOTE NDANI YA MIAKA SITA.
HATUTAKI BLAH BLAH TUNATAKA MATOKEO CHANYA.
So aliyosema Makamba ni uongo?
 
Ni uchaguzi wa mwaka gani uliwahi kuwaunganisha?

Uchaguzi wa 2015 ndiyo mgombea ubunge Alphonse Mawazo aliuwawa kama kibaka huko Geita!

Hakuna Tajiri amewahi kuharibiwa biashara kwa sababu ya siasa za uchaguzi kumzidi Mzee Tango kisa Mrema mwaka 1995.

Kama Makamba anamaanisha kweli si awashauri wenzie huko cabinet ipatikane katiba mpya na tume ya uchaguzi isiyojaa makada.
 
Naona Wahusika wakubwa ndani ya Serikali wameanza kusema wenyewe juu ya kilichotokea wakati wa Uchaguzi wa 2020.Mh Makamba akiwa Italy akiongea na Watanzania amemwaga Mchele wote jinsi Uchaguzi wa 2020 Chini ya HAYATI MAGUFULI ulivyokuwa na Watu Walivyoumizwa na kudhulumiwa ili MAGUFULI ASHINDE.
Asante Makamba kwa taarifa hiyo tuna imani na Aliyempiga RISASI Mwanasiasa TUNDU LISSU tutamjua tu.Mwendazake Alipanda MBEGU ya CHUKI na AMEIVUNA
MUNGU siku zote ni hataki WATU WABAYA MUNGU ni FUNDI ameumaliza Mchezo kati ya Watanzania na MWENDAZAKE. Pumzika Mwendazake Umevuna ulichokipanda
Hakuna kupumzika.
Yule lazima achomwe moto sn tu
 
Back
Top Bottom